Hofu ya Kimaadili Nchini Denmark: Wakati Thamani za Kiislamu Zinapopinga Ufisadi wa Kimaadili wa Kidenmaki
(Imetafsiriwa)
Habari:
Katika siku za hivi karibuni, Waislamu nchini Denmark wamekumbana na ukosoaji mkali kwa kushiriki vikumbusho vya Kiislamu kwenye mitandao ya kijamii kuhusu sherehe za kila mwaka za kuhitimu kutoka shule za sekondari, ambazo mara nyingi huhusisha mchanganyiko wa jinsia, unywaji wa pombe hadharani, na tabia chafu. Machapisho hayo yaliwapongeza wahitimu, na kuwashauri vijana Waislamu kukaa mbali na tabia ambazo zinapingana na maadili ya Kiislamu.
Hili lilisababisha majibu makali kutoka kwa wanasiasa na wanahabari wa Denmark, pamoja na shutuma za "itikadi kali" na "udhibiti wa kijamii," na hata kutishia maisha ya kikazi. Wanasiasa, akiwemo waziri wa ujumuishaji, waliwakosoa Waislamu kwa kutokubali utamaduni wa unywaji pombe nchini Denmark, wakidai kuwa ni "sehemu ya maadili yetu."
Maoni:
Ghadhabu juu ya ushauri rahisi wa Kiislamu inafichua mengi zaidi kuhusu wanasiasa wa Denmark kuliko inavyofichua kuhusu Waislamu. Kilichoanzisha tabaka la kisiasa na vyombo vya habari sio chuki, uchochezi, au kulazimisha, lakini maoni ya maadili yaliyokita mizizi katika Uislamu ambayo yalihoji kanuni za kijamii na kuwashauri Waislamu wasishiriki katika sherehe za hiari, na hii pekee ilionekana kuwa haikubaliki na iliharamishwa.
Hii ndiyo kiini cha ulimwengu huria: huvumilia maoni yote, isipokuwa yale yanayotokana na vyanzo vya mbinguni na kupinga misingi yake. Waislamu wanapoeleza tu imani yao kwamba pombe na mchanganyiko wa jinsia ni makosa, kinyago cha uvumilivu huanguka. Uhuru wa kujieleza unakuwa pendeleo kwa sauti za kilimwengu pekee. Ama wengine, lazima wawe wamejumuishwa au kunyamazishwa na maafisa wa serikali. Lengo ni rahisi: tabia mbaya ni takatifu, na ulevi ni thamani takatifu ya Denmark, ingawa unywaji wa pombe, kulingana na wataalam na ripoti nyingi, ni tatizo kubwa miongoni mwa vijana wa Denmark, ambao wanashikilia rekodi ya Ulaya ya unywaji wa pombe miongoni mwa vijana. Hata hivyo, wanasiasa hao hao ambao wanawashambulia vijana Waislamu kwa kuwaonya dhidi ya ulevi, wamekaa kimya kabisa kwa miezi ishirini huku mauaji ya kimbari yakitokea Gaza. Hasira yao ilikuwa wapi wakati watoto walikuwa wanachinjwa? Mahubiri yao ya maadili yalikuwa wapi wakati hospitali zilipokuwa zikishambuliwa na familia nzima kuzikwa chini ya vifusi? Ukimya wao unaongea zaidi ya hasira yao ya kuchagua.
Kwa vijana wote Waislamu wanaohitimu mwaka huu: Tunawapongeza kutoka mioyoni mwetu. Sio tu kwa mafanikio yenu ya kitaaluma, bali kwa msimamo wenu juu ya utambulisho wenu wa Kiislamu katikati ya shinikizo kubwa la kijamii, nyinyi ni fahari ya taifa hili. Kukataa kwenu kutii viwango visivyo vya kimaadili sio ulegevu, lakini ni kanuni, ujasiri, na hitaji la dharura. Kamwe msiaibike na Uislamu, hamko peke yenu, taifa lote liko pamoja nanyi. Msiache vitisho vyao na dhihaka zao zipite kwenu, kwani ni ishara za udhaifu wao, sio udhaifu wenu. Simameni imara, mwingiliane na jamii kwa hekima na ujasiri, na bebeni Uislamu wenu kwa heshima. Hatimaye, matukio haya yanatukumbusha tena kwamba Uislamu sio tu imani ya kibinafsi, lakini ni njia kamili ya maisha. Umefika wakati wa kufanya kazi kwa bidii kwa ajili ya mfumo wa kisiasa ambao unalinda maadili yetu na kuonyesha imani yetu; dola ambayo inajumuisha Uislamu kama rehema kwa wanadamu, mfumo huu ni Khilafah kwa msingi wa Utume.
Imeandikwa kwa ajili ya idhaa ya Ofisi ya Habari Kuu ya Hizb ut-Tahrir
Ibrahim Al-Atrash