Hukumu ya Mtajiki Aliyefukuzwa kutoka Uswidi Kifungo cha Miaka 8 kwa Kujiunga na Hizb ut-Tahrir
(Imetafsiriwa)
Habari:
Nchini Tajikistan, mwanaharakati Farhod Najmotov, aliyefukuzwa kutoka Uswidi, amehukumiwa kifungo cha miaka minane kwa tuhuma za kushiriki katika shughuli za Hizb ut-Tahrir. Hii iliripotiwa na Huduma ya Tajik ya Radio Free Europe. Mmoja wa jamaa za mwanaharakati alisema: "Tunakataa hukumu hii, lakini hatukukata rufaa kwa mahakama ya rufaa ili kuepuka kusababisha matatizo ya ziada."
Inakumbukwa kwamba Farhod Najmotov na binti zake watatu walifukuzwa kutoka Uswidi mnamo Desemba 27, 2024. Walipowasili Dushanbe, alikamatwa mara moja, na binti zake walipelekwa kwa jamaa zao. Mnamo 2019, familia yake ilihamia Ukraine, lakini baada ya kuanza kwa uvamizi kamili wa Urusi, walihamia Gothenburg, Uswidi. Chanzo kiliiambia Radio Ozodi: "Farhod Najmotov aliomba hifadhi ya kisiasa huko mara kwa mara, lakini kila mara ombi lake lilikataliwa." Nchini Tajikistan, Hizb ut-Tahrir ilipigwa marufuku chini ya uamuzi wa Mahakama Kuu mnamo 2001.
Maoni:
Hii sio kesi ya kwanza ambapo waomba hifadhi wa Tajik wamehukumiwa kifungo kirefu nchini Tajikistan baada ya kufukuzwa kutoka Ulaya. Baada ya kufukuzwa kutoka Ujerumani, Abdullah Shamsiddin, mwana wa mpinzani wa Tajik na mwanachama wa Chama cha Uamsho wa Kiislamu nchini Tajikistan, Shamsiddin Saidov, alihukumiwa kifungo cha miaka saba. Nchi mbalimbali za Ulaya zimeshuhudia operesheni kama hizo za kufukuzwa na kukabidhi watu kwa muda mrefu.
Mwelekeo huu wa kuwakabidhi wanaharakati wa kisiasa kwa madikteta ili kuwaangamiza, unaonyesha tena unafiki wa maneno ya wanasiasa wa Magharibi kuhusu kulinda maadili na uhuru wao wa kiliberali. Kwa kweli, wako tayari kuachana na maadili haya yaliyotangazwa katika fursa ya kwanza, haswa linapokuja suala la kutishia Uislamu wa kimisingi. Katika kukabiliana na upanuzi wa Uislamu wa kimisingi, nchi za Magharibi za kidemokrasia rasmi na udikteta wa Mashariki huungana na kushikamana; kuratibu matendo yao na kusaidiana. Waislamu, ikiwa nchi za Magharibi zinawahitaji, ni wafanyakazi kimya kimya ambao watafidia kupungua kwa idadi ya watu wao. Kwa hivyo, kila Muislamu anayeishi Magharibi na anakataa kuungana kiotomatiki yuko hatarini.
Waislamu hawapaswi kuweka matumaini yao kwa nchi za Magharibi ili kuwaokoa kutoka kwa udikteta, hii ni mtego na mchezo wa "polisi mwema na polisi mbaya", madhalimu katika nchi zetu ni zao la wakoloni wa Magharibi.
Imeandikwa kwa ajili ya Redio ya Ofisi ya Habari Kuu ya Hizb ut-Tahrir
Muhammad Mansour