Uislamu uko mbali sana na majadiliano ya kidini
(Imetafsiriwa)
Habari:
Mnamo Julai 5, 2025, kuba jipya la ibada lilifunguliwa katika kanisa la "Amka na Uangaze" huko Tanzania, lililoko Kawi, nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam. Huduma hii inaongozwa na mwinjilisti Boniface Mwambosa, ambaye alijiweka kama "mtume," ambaye mahubiri yake mwaka 2020 yalisababisha vifo vya zaidi ya waumini 20 kutokana na mkanyagano, walipokuwa wakikimbilia kupakwa mafuta matakatifu.
Maoni:
Sherehe ya ufunguzi ilitumiwa kuendeleza maadili ya kidemokrasia na ya kilimwengu, ambapo Rais Samia alisisitiza umuhimu wa kudumisha mshikamano wa kitaifa, na akawahimiza Watanzania kuhifadhi amani na umoja imara nchini, huku taifa likijiandaa kwa uchaguzi mkuu mnamo Oktoba 2025.
Zaidi ya hayo, tukio kama hilo lilitumiwa kuendesha ajenda ya kidini hatari sana, kiasi kwamba hatua nyingi zinazowakilisha kampeni hiyo ya kishetani zilifuatiliwa kwa karibu na kuthibitishwa.
Sherehe hiyo ilishuhudia baadhi ya viongozi wa Kiislamu na wanasiasa wenye asili ya Kiislamu, pamoja na Waislamu wa kawaida, wakiomba na watu wasio Waislamu ndani ya kanisa, hata baadhi yao walitoa matamshi dhidi ya hukumu na mawazo ya Kiislamu.
Sherehe ya kuapishwa ilicheza jukumu muhimu, na ilitumiwa sana kama jukwaa la kuhubiri na kutoa wito wa mazungumzo ya kidini kati ya Uislamu na Ukristo kwa jina la mshikamano wa kijamii au kidini ndani ya nchi. Baada ya kushindwa kwa nchi za Magharibi kuwaondoa Waislamu kutoka kwa imani yao kupitia wamisionari, wanazuoni wa masuala ya Mashariki, kazi za kitamaduni na vyombo vya habari, upotoshaji wa kiakili na kisiasa, waligeukia mazungumzo ya kidini yaliyoanzishwa na Ufaransa mwaka 1932 kwa kutuma ujumbe wake Al-Azhar.
Lengo lao kuu la kampeni ya mazungumzo ya kidini ambayo inakuza nchi za kibepari ni kuzuia Uislamu kurudi katika masuala ya maisha kama mfumo kamili, kwani inatishia uhai wa kanuni yao na ustaarabu wa kibepari na kuharibu maslahi na ushawishi wao.
Wanabepari wa Magharibi wanafanya kazi kupitia mazungumzo ya kidini kufuta utamaduni wa Kiislamu kutoka kwa akili za Waislamu, na wanalenga kufanikisha hilo kwa kudhoofisha imani ya Waislamu katika utamaduni wao, vyanzo vyake na hukumu zake, na kutoegemea upande wowote hukumu za Kiislamu na kudhoofisha nguvu zao zilizopo katika kukabiliana na dhana za ustaarabu zisizo za Kiislamu. Bila kusahau mpango wa Magharibi wa kuuvua Uislamu sifa zake muhimu zaidi zinazouweka tofauti na dini nyingine, ambazo ni upande wa kijamii na kiuchumi, na muhimu zaidi upande wa kisiasa unaokumbatiwa na dola la Khilafa.
Waislamu nchini Tanzania na kwingineko wanapaswa kuwa waangalifu dhidi ya mpango huu mbaya wa kimataifa unaoendelea wa mazungumzo ya kidini, kiakili na kivitendo.
Ingawa Uislamu unaruhusu ushirikiano na wasio Waislamu, haujumuishi mshikamano wa kidini, na unakataza kabisa ushiriki wowote katika ibada za dini zingine. Dini ya kweli pekee ni Uislamu, ambayo Waislamu wanapaswa kushiriki katika kuihubiri ili kutekeleza hukumu zake zote chini ya dola la Khilafa.
#DiniYaHakiUislamuTu
Imeandikwa kwa ajili ya Idhaa ya Afisi ya Habari Kuu ya Hizb ut Tahrir
Saeed Beitumuwa
Mjumbe wa Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir nchini Tanzania