Ukhalifa au Ukoloni: Chaguo Muhimu kwa Umma katika Afghanistan na Pakistan
(Imetafsiriwa)
Habari:
Kwa lengo la kumaliza mzozo uliopo kati ya Afghanistan na Pakistan, kufuatia makubaliano ya kusitisha mapigano nchini Qatar, mkutano ulifanyika Istanbul, ambapo pande hizo mbili zilisistiza kuendelea kusitisha mapigano, na kukubaliana kufanya mkutano wa ngazi ya juu mnamo Novemba 6 kujadili njia za kivitendo za utekelezaji wake. Imepangwa kuwa wakati wa mkutano huu, utaratibu maalum wa kufuatilia na kuthibitisha utekelezaji wa makubaliano utatungwa, ambao utahakikisha kudumisha amani, na kuruhusu uwezekano wa kumwadhibu mhalifu.
Maoni:
Juhudi hizi hazitasababisha amani ya kudumu isipokuwa Waislamu wa Afghanistan na Pakistan wasimame kwenye mstari wa mbele wa kiitikadi na kisiasa, na hata kijeshi, na wasiache suala lao mikononi mwa wakoloni au washirika wao kama vile Qatar na Uturuki, bali kwa Uislamu na hukumu zake. Mikutano inayofanyika ndani ya mfumo wa maagizo, njama na maslahi ya nguvu za kikoloni, katika hali nzuri zaidi, ni marudio ya muda tu ya kusitisha mapigano; na hatimaye, ni kifuniko cha kuendelea kwa ushindani wa kikoloni juu ya ardhi, rasilimali na njia za kiuchumi, pamoja na kuwa jaribio la kuzuia kuamka na umoja wa umma wa Kiislamu katika eneo hilo.
Umuhimu wa suala hili unajitokeza kwa ukweli kwamba Asia Kusini imekuwa uwanja wa mapambano kwa maslahi ya nguvu za kikoloni za kimataifa. Afghanistan, yenye rasilimali zake nyingi za madini na eneo lake muhimu la kijiografia na kisiasa, na Pakistan, yenye njia zake na bandari zake za kimkakati, zina jukumu muhimu katika milinganyo ya kijiografia na kiuchumi ya eneo hilo. Amerika - katika ishara ya uondoaji wa vikosi vyake kutoka Afghanistan, kukabidhi silaha kwa wingi kwa Taliban, na kuacha kambi ya Bagram, ambayo ina eneo la kijiografia na kimkakati wa kufuatilia Uchina na Urusi - inataka kuishinikiza serikali ya Taliban na kuilazimisha kukubali masharti yake. Kwa upande mwingine, Uchina, kwa uwekezaji mkubwa, haswa katika mfumo wa Ukanda wa Kiuchumi wa China na Pakistan, inataka kuanzisha mtandao wa miundombinu ya kufikia masoko ya ulimwengu, mtandao ambao utaunganisha eneo hilo na uchumi wake.
Katika kukabiliana na ushawishi huu, Amerika inatafuta mipango sambamba ya kudumisha utawala wake wa kiuchumi na kiusalama katika eneo hilo, na wakati huo huo inajaribu kuiondoa serikali ya Afghanistan kutoka kwenye mzunguko wa ushawishi wa Uchina na Urusi na kuizuia kuwa nguvu yenye ushawishi katika umma wa Kiislamu. Ushindani kati ya Amerika na Uchina kwa ushiriki wa India tegemezi kwa Amerika unalenga kuifanya Afghanistan kuwa adui wa Pakistan na karibu na India, na kugeuza eneo hilo kuwa uwanja wa ushindani wa kikoloni, ambapo miradi ya kiuchumi ni zana za utawala wa kisiasa na udhibiti wa rasilimali za umma.
Kwa hivyo, mikutano ya muda mfupi na mrefu ya serikali hizi kutatua mzozo wa Afghanistan na Pakistan haitatatua tatizo hili kamwe. Mradi sera ya Marekani katika eneo hilo inaendelea kuunda mvutano kati ya Pakistan na Afghanistan; na mradi mzunguko fulani ndani ya jeshi la Pakistan, ambao unaishinikiza Amerika chini ya jina la "kupambana na ugaidi" au "kuishinikiza Taliban," unabaki madarakani; na mradi makundi yenye silaha yanaendelea kuwepo katika eneo hilo na kupinga sera za ukandamizaji na za kidunia za serikali; na mradi mstari wa Durand uliowekwa unaendelea kuwepo katika eneo hili; na mradi serikali za kitaifa, kwa kuzingatia maslahi yao finyu na ya kikundi, zinafanya siasa dhidi ya kila mmoja, tatizo hili halitatatuliwa kamwe.
Hata hivyo, mzizi wa mzozo hauzuiliwi kwa michezo ya kijiografia na kisiasa, bali unatoka kwa ugonjwa wa kiitikadi na kisiasa unaowakilishwa na kugawanyika kwa umma katika nchi na mipaka bandia iliyojengwa juu ya utaifa na ubaguzi wa rangi. Mradi Waislamu wa Afghanistan na Pakistan wanaendelea kufafanua utambulisho wao kwa misingi ya mipaka ya kitaifa ya kikoloni, na kupuuza utambulisho wa Kiislamu kama umma mmoja, na hawatakata mikono ya wakoloni kutoka eneo hilo, hakuna makubaliano yoyote yatakayodumu. Umoja wa kiitikadi, kisiasa na kijiografia wa nchi hizi mbili lazima uundwe kwa misingi ya utiifu kwa Mungu, Uislamu na Waislamu, sio kwa misingi ya maslahi ya muda mfupi ya taifa au makubaliano na wakoloni.
Suluhisho la kweli liko katika nguzo tatu za msingi:
Kwanza, kukatisha kabisa utegemezi kwa nguvu za kikoloni na kusitisha ushirikiano wa kiuchumi, kijeshi na kiintelijensia nazo.
Pili, kujenga upya uchumi wa kikanda kwa misingi ya usimamizi wa rasilimali za umma na kuendeleza miundombinu huru.
Tatu, uhamasishaji wa kiitikadi, kisiasa na kijeshi ili kuondoa utaifa na kufufua ufahamu wa umma mmoja.
Wasomi, wanazuoni, vyama na taasisi lazima ziwe kitovu cha juhudi za kurejesha siasa kwa misingi ya Uislamu. Mfumo pekee unaounganisha nguzo hizi ni mfumo wa kisiasa unaozingatia sheria za Kiislamu na umoja wa umma, mfumo ambao unaondoa mipaka bandia, na hauruhusu miradi ya kikoloni kulazimisha utawala wake juu ya muundo wa utegemezi kati ya nchi. Kuanzishwa kwa Khilafah Rashidah ndiyo njia ya kweli ya kuokoa eneo hilo kutoka kwenye makucha ya ukoloni, na kurejesha mamlaka kwa umma. Njia hii inahitaji kujitolea, ufahamu na utashi wa kisiasa, na hakuna njia nyingine ya ukombozi isipokuwa hiyo.
Imeandikwa kwa ajili ya Idhaa ya Ofisi Kuu ya Habari ya Hizb ut-Tahrir
Yusuf Arsalan
Mwanachama wa Ofisi ya Habari ya Hizb ut-Tahrir katika Wilaya ya Afghanistan