Khilafa kwa Ajili ya Ulimwengu Usio na Jumuiya ya Nchi za Atlantiki ya Kaskazini (NATO)
(Imetafsiriwa)
Habari:
Wakuu wa nchi na serikali wanachama wa Jumuiya ya Nchi za Atlantiki ya Kaskazini walikutana The Hague, Uholanzi, Juni 24 na 25.
Maoni:
Tamko la Mkutano wa The Hague lililotolewa na wakuu wa nchi na serikali za Jumuiya ya Nchi za Atlantiki ya Kaskazini, lilijumuisha taarifa zifuatazo: "Katika kukabiliana na vitisho na changamoto kubwa za kiusalama, haswa tishio la muda mrefu linaloletwa na Urusi kwa usalama wa Ulaya na Atlantiki na tishio linaloendelea la ugaidi, washirika wamejitolea kutenga 5% ya Pato la Taifa kwa mahitaji ya ulinzi ya kila mwaka na matumizi ya usalama na ulinzi hadi 2035. Ahadi hii itatuwezesha kutimiza majukumu yetu ya kibinafsi na ya pamoja chini ya Kifungu cha 3 cha Mkataba wa Washington. Uwekezaji huu utahakikisha kuwa tunamiliki vikosi, uwezo, rasilimali, miundombinu, utayari wa mapigano na uthabiti unaohitajika kwa majukumu matatu ya msingi ya kuzuia na ulinzi, kuzuia na kusimamia migogoro, na usalama shirikishi."
Katika mkutano wa The Hague wa Jumuiya ya Nchi za Atlantiki ya Kaskazini, Urusi na ugaidi ziliibuka kama vitisho muhimu zaidi, wakati suala lingine muhimu lilikuwa ahadi ya nchi wanachama kutenga 5% ya Pato la Taifa kwa matumizi ya usalama na ulinzi.
Jumuiya ya Nchi za Atlantiki ya Kaskazini ni shirika la kijeshi linalotumiwa na Marekani kwa maslahi yake binafsi. Hivi sasa, Marekani inaona kwamba Urusi, China na Ulaya, pamoja na neno ugaidi katika tangazo lake, zinatishia ulimwengu.
Katika muktadha huu, Marekani inataka kutumia Jumuiya ya Nchi za Atlantiki ya Kaskazini (NATO) kulinda maslahi yake dhidi ya Uislamu na Waislamu, Urusi, na kwa muda mrefu, China.
Kwa shinikizo kutoka Amerika, nchi wanachama wa NATO zimejitolea kuongeza matumizi yao ya usalama na ulinzi hadi 5% ya Pato la Taifa.
Pato la Taifa lililojumuishwa la nchi wanachama 32 wa NATO ni karibu dola trilioni 50. Nchi wanachama hutumia trilioni 1 na milioni 250 kwa usalama na ulinzi kila mwaka. Katika mkutano wa The Hague, Marekani ililenga kuongeza idadi hii hadi dola trilioni 2.5 kwa ahadi ya nchi wanachama.
Kwa hivyo, nchi wanachama wa NATO wataingia katika mbio za silaha, na nchi zilizo na tasnia ya ulinzi na silaha za hali ya juu, haswa Merika, zitanufaika na hali hii. NATO pia itakuwa na nguvu katika uwanja wa ulinzi na usalama. Ukweli ni: shirika la kimataifa la kijeshi linalojumuisha nchi 32, lenye silaha za kisasa na majeshi yenye nguvu zaidi ulimwenguni, nani anaweza kukabiliana nalo, na anawezaje kukabiliana nalo? Nani anaweza kupigana na nguvu kubwa kama NATO?
Marekani inataka kudumisha utawala wake ulimwenguni kwa kutumia nguvu hii kubwa, NATO, kwa maslahi yake binafsi. Kwa sababu hii, NATO ni moja ya vitisho muhimu zaidi kwa Waislamu na wanadamu, ambayo lazima iharibiwe, ivunjwe, izuiwe na kupigwa vita. Kwa hivyo nani anaweza kupigana na NATO na kuipunguza nguvu? Jibu pekee na la kweli ni Khilafa.
Ikiwa Waislamu wanaweza kuunganisha nafasi yao ya kati na umuhimu wake wa kijiografia na kimkakati ulimwenguni, utajiri wao na rasilimali zao za ndani na za nje, na idadi yao ya karibu watu bilioni mbili, na majeshi yao makubwa yaliyo na silaha za hali ya juu na zilizoorodheshwa ulimwenguni, na mradi wa kisiasa kama vile Khilafa, watakuwa nguvu kubwa inayoweza kupigana na NATO na kuipunguza nguvu. Khilafa ndio nguvu na chaguo pekee la kukomboa Waislamu na wanadamu wote kutoka kwa utawala wa wakoloni﴿لِمِثْلِ هَذَا فَلْيَعْمَلْ الْعَامِلُونَ﴾.
Imeandikwa kwa ajili ya Idhaa ya Afisi ya Habari Kuu ya Hizb ut-Tahrir
Ramzi Aziz