Je, haijafika wakati kwetu kushikamana na njia iliyonyooka na kuepuka njia zilizopinda?!
Habari:
Kufanyika kwa uchaguzi wa sita wa bunge baada ya mwaka 2003, mnamo 11 Novemba 2025.
Maoni:
Pamoja na misukumo yote ya kimedia ambayo huambatana na uchaguzi kwa kawaida, na vitendo vya kisiasa vinavyofanywa na wenye nguvu na matamko na upinzani ambao lengo lake ni kufunika uhalisia wa uchaguzi kama huu katika nchi za Waislamu na ikiwemo Iraq, na katika kivuli cha katiba na mifumo ambayo haitekelezi sheria ya Mwenyezi Mungu na wala haiiweki kama hakimu katika masuala yake, ni lazima kuweka mstari ulionyooka karibu na mistari iliyopinda, ili ukweli ubainike kutoka kwa ubatili, na halali kutoka kwa haramu, na zuri kutoka kwa baya, Mwenyezi Mungu amesema: ﴿Na kwamba hii ndiyo njia yangu iliyonyooka, basi ifuateni, wala msifuate njia nyingine, zikakutenganisheni na njia yake. Hivyo ndivyo alivyokuelezeni, ili mpate kumcha.﴾.
Hakika kujua hukumu ya kisheria kunahitaji kutimiza sababu yake, na sababu yake hapa ni kuchagua wajumbe wa baraza la wawakilishi, na asili ya kazi za baraza na mamlaka yake, na kisha kuiteremsha hukumu ya kisheria juu yake.
Na baraza la wawakilishi katika mfumo wa kidemokrasia hufanya kazi na majukumu muhimu zaidi: Kutunga sheria, kuipa serikali imani na kuiwajibisha na kuidhinisha bajeti kuu, kuapa kulinda katiba ya kibinadamu, kuidhinisha makubaliano na mikataba, na kumchagua rais wa nchi.
Ama uhalisia wa uchaguzi kisheria ni uwakilishi na niaba katika jambo ambalo uchaguzi unafanyika kwa ajili yake, na kwa hivyo hukumu ya sheria katika uchaguzi inachukua hukumu ya uwakala, ikiwa utawakilishwa katika kazi halali, basi uwakala huo utakuwa halali, na ikiwa utawakilishwa katika kazi haramu, basi uwakala huo utakuwa haramu.
Ama kutunga sheria ni kitendo ambacho haifai kwa Muislamu kukifanya, wala kutunga wala kupiga kura juu ya sheria kwa kutoa au kukubali hata kama sheria hii inakubaliana na hukumu ya Uislamu; uhalali wa sheria na marejeleo yake ni kuwa ina dalili kutoka kwa sheria, iwe watu wamekubaliana nayo au hawajakubaliana nayo, kwa hivyo kutunga sheria ni kwa Mwenyezi Mungu pekee na hakuna yeyote anayepaswa kumshirikisha Mwenyezi Mungu katika hilo, Mwenyezi Mungu amesema: ﴿Hukumu si ila ya Mwenyezi Mungu.﴾.
Ama kuipa serikali ya kilimwengu imani ambayo haihukumu kwa yale ambayo Mwenyezi Mungu ameyateremsha haifai kwa Muislamu, kama vile haifai kwake kuidhinisha makubaliano na mikataba inayotegemea sheria za ukafiri achilia mbali kuwa ni makubaliano ambayo yanamfanya kafiri awe na njia ya kuwadhuru watu na nchi, na Mwenyezi Mungu anasema: ﴿Wala Mwenyezi Mungu hatawapa makafiri njia ya kuwashinda Waumini.﴾.
Ama kuapa kulinda katiba na uaminifu kwa taifa, hakika katiba ni sheria iliyotungwa na wanadamu ambayo ni haramu kuhukumu nayo, na uaminifu haupaswi kuwa isipokuwa kwa Mwenyezi Mungu, basi vipi mbunge anaapa kwa Mwenyezi Mungu, juu ya kitabu cha Mwenyezi Mungu, kwamba atamuasi Mwenyezi Mungu na kuhukumu kwa asiyekuwa sheria yake?!
Ama suala la kuwajibisha, hakuna shaka kwamba ni hitaji muhimu na la lazima na ni moja ya kazi za kuamrisha mema na kukataza maovu na ni faradhi, lakini je, kuwajibisha katika baraza la wawakilishi kunafanyika kwa misingi ya Uislamu au kwa misingi ya katiba na sheria za kibinadamu?
Ama kuidhinisha bajeti ni batili kwa kila mwenye macho, bajeti inategemea kodi na mikopo ya riba kulingana na uchumi wa kibepari.
Na baada ya maelezo haya inakuwa wazi kwamba uchaguzi huu unafanyika kulingana na katiba ya kibinadamu ambayo inapingana na Uislamu, kwa hivyo unakuwa haramu, na ni ushahidi wa uongo unaolenga kuimarisha wazo la kutowezekana kwa mabadiliko, ambayo inatolewa picha na wajinga au waoga au wasomi wa watawala, na ina malengo mengine.
Lakini mabadiliko yako ndani ya uwezo wa umma wa Kiislamu ikiwa utamtegemea Mwenyezi Mungu na kushikamana na njia ya Mtume wake ﷺ, kisha ukiweka mkono wake katika mikono ya wanyofu na wao ni wengi, Alhamdulillah. Tunakualika kwenye hili jema na Mwenyezi Mungu ndiye anayefanikisha makusudio.
Imeandikwa na Idhaa ya Ofisi ya Habari Kuu ya Hizb ut-Tahrir
Dkt. Abdul Ilah Muhammad - Jimbo la Jordan