Njaa Ghaza: Umoja wa Mataifa na Nguvu za Dunia Zina Wajibika
(Imetafsiriwa)
Habari:
Kuanzia Agosti 22, 2025, Uainishaji Jumuishi wa Awamu za Usalama wa Chakula (IPC) ulitangaza rasmi hali ya njaa (Awamu ya 5) huko Gaza. Kulingana na uainishaji, takriban watu 640,000 wanakabiliwa na "viwango vya janga la ukosefu wa uhakika wa chakula" (Awamu ya 5), watu milioni 1.14 wako katika hali ya "hatari" (Awamu ya 4), na watu 396,000 wako katika hali ya "mgogoro" (Awamu ya 3).
Maoni:
Licha ya kuwepo kwa mashirika mengi ya Umoja wa Mataifa, ikiwa ni pamoja na Shirika la Chakula na Kilimo (FAO), UNICEF, Mpango wa Chakula Duniani, Shirika la Afya Duniani, na idadi kubwa ya mashirika yasiyo ya kiserikali yanayohusiana nayo, mashirika haya yameshindwa kupunguza kile kinachochukuliwa, kwa kweli, mpango wa kisasa wa mauaji ya kimbari. Kwa miongo kadhaa ya uzoefu katika kukabiliana na njaa duniani kote, mashirika haya hayajatangaza kuwepo kwa mgogoro wa maisha, wala hayajaingilia kati kwa ufanisi kuzuia kuenea kwa kifo cha njaa. Kukataa kwa ulimwengu kutaja uhalifu huo mauaji ya kimbari, na mwelekeo wake wa kulaumu kwa njia isiyo wazi hali ya vita au sera za serikali ya Kiyahudi, kunaonyesha kushindwa kwa maadili na kivitendo. Kushindwa huku si jambo jipya katika historia. Njaa kama vile Njaa ya Viazi ya Ireland (1845-1852), Njaa Kuu ya Ukraine (1932-1933), Njaa Kuu ya China (1959-1961), na njaa nyingi za India (1770, 1782, 1788, 1837, 1876, na 1943) ziliongezeka kutokana na nguvu za kikoloni ambazo sera zao ziliweka kipaumbele udhibiti, faida na mamlaka juu ya uhai wa mamilioni. Leo, taasisi ya Kiyahudi na Amerika, pamoja na serikali za kikanda zinazoshirikiana, kama vile Misri, Jordan, Uturuki na zinginezo, zinarudia mtindo huu. Matendo yao ikiwa ni pamoja na kudondosha misaada ndogo na mara nyingi yenye madhara yanalenga kuendeleza utumwa badala ya kupunguza mateso.
Kuto walisha wenye njaa huko Gaza sio tu suala la kisiasa; bali ni wajibu muhimu wa kibinadamu na kimaadili. Kama Mwenyezi Mungu anavyotukumbusha katika Hadith Qudsi «Hakika Mwenyezi Mungu anasema Siku ya Kiyama: Ewe mwanaadamu! Nilikuwa mgonjwa na hukunitembelea! Akasema: Ee Mola wangu! Vipi nikutembelee na Wewe ndiye Mola wa walimwengu? Akasema: Hukujua kwamba mja wangu fulani alikuwa mgonjwa na hukumtembelea! Hukujua kwamba lau ungemtembelea ungenikuta kwake! Ewe mwanaadamu! Nilikuhitaji chakula na hukunilisha! Akasema: Ee Mola wangu! Vipi nikulishe na Wewe ndiye Mola wa walimwengu? Akasema: Hukujua kwamba mja wangu fulani alikuhitaji chakula na hukumlisha! Hukujua kwamba lau ungemlisha ungelikuta hilo kwangu! Ewe mwanaadamu! Nilikuhitaji maji na hukunyweesha! Akasema: Ee Mola wangu! Vipi nikunyweshe na Wewe ndiye Mola wa walimwengu? Akasema: Mja wangu fulani alikuhitaji maji na hukumnywesha! Hukujua kwamba lau ungemnywesha ungelikuta hilo kwangu».
Kulisha wenye njaa na kuwalinda wanyonge sio tu wajibu wa kimaadili kwa Waislamu, lakini ni kigezo cha ulimwengu cha ustaarabu. Kupuuza wenye uhitaji, huku tukidai kutoa msaada kupitia njia za urasimu ambazo zinashindwa kuwafikia waliodhulumiwa, ni usaliti wa utu wa binadamu na kukataa jukumu letu mbele ya Mwenyezi Mungu.
Vizuizi vya kupeleka misaada Gaza ni dhahiri: vizuizi vya mpaka, mzingiro wa kijeshi, na serikali zinazoshirikiana zinazotekeleza sera zilizochorwa miongo kadhaa iliyopita chini ya mamlaka ya kikoloni - mistari iliyochorwa na Sykes Mwingereza na Picot Mfaransa mnamo Mei 16, 1916. Jukumu liko hasa kwa watawala na askari wanaodhibiti mipaka kuruhusu chakula, misaada ya matibabu na vifaa muhimu kuwafikia wahitaji. Familia za wale wanaoweka vizuizi hivi pia wanabeba jukumu la kimaadili, pamoja na jamii katika nchi za Kiislamu na ulimwengu mpana zaidi ambao unavumilia dhuluma hii.
Mwenyezi Mungu anatuambia katika Qur'ani Tukufu: ﴿Akasema Isa bin Mariam: Ewe Mwenyezi Mungu, Mola wetu! Tuteremshie meza kutoka mbinguni iwe sikukuu kwa wa kwanza wetu na wa mwisho wetu, na ishara itokayo kwako. Na uturuzuku, na Wewe ndiye mbora wa wanao ruzuku. Akasema Mwenyezi Mungu: Hakika Mimi nitaiteremsha kwenu, lakini atakaye kufuru miongoni mwenu baada ya haya, basi Mimi nitamwadhibu adhabu ambayo simuadhibu yeyote katika walimwengu﴾.
Wafuasi wa Isa, amani iwe juu yake, walitumia uingiliaji kati wa kimungu kupeleka riziki wakati wa dhiki. Vile vile, umma wa Kiislamu leo unatoa wito wa msaada kwa watu wa Gaza. Hata hivyo, maombi lazima yaambatane na matendo. Ukombozi wa kweli haumo katika maombi pekee, bali katika uhamasishaji wa kupinga mzingiro na kuondoa mifumo hii inayoshirikiana.
Yeyote anayefanya uzembe huku ndugu zake wakifa, asifikiri kwamba anastahili rehema. Siku ya Kiyama, wale walioahidiwa shahada watashuhudia uzembe wa wale ambao wangeweza kuleta mabadiliko. Kulisha wenye njaa, kutoa makazi, na kuwalinda waliodhulumiwa sio chaguo, bali ni wajibu kwa kila dhamiri inayodai kuthamini ubinadamu, na haswa kwa watawala ambao wana uwezo na mamlaka ya kufanya hivyo.
Imeandikwa kwa Redio ya Ofisi ya Habari Kuu ya Hizb ut-Tahrir
Ibrahim Ahmed