Kibali cha Marekani Sio Kigezo cha Uamuzi wa Kisiasa wa Umma wa Kiislamu
(Kimetafsiriwa)
Habari:
Mnamo Julai 17, 2025, gazeti la Dawn lilimnukuu Reuters: "Ikulu ya White House ilitangaza Alhamisi kwamba hakuna ziara iliyopangwa ya Rais wa Marekani Donald Trump nchini Pakistan kwa sasa kufuatia ripoti nyingi kuhusu ziara hiyo. Mapema leo, baadhi ya vituo vya televisheni vya ndani, vikinukuu vyanzo, viliripoti kwamba Trump anatarajiwa kuizuru Pakistan mwezi Septemba. Vituo vya habari viliripoti kwamba Trump pia atazuru India baada ya kuwasili Islamabad mwezi Septemba. Vituo hivyo baadaye viliondoa ripoti zao." (Dawn News)
Maoni:
Taasisi ya kijeshi ya Pakistani inaamini kwamba tawala za Republican za Amerika zina huruma na zinakaribisha Pakistani kwa ujumla, kinyume na tawala za Kidemokrasia ambazo zinafuata sera ya uhasama. Kwa mfano, Rais Biden hakukutana na kiongozi yeyote wa Pakistani. Pia hakupiga simu na Waziri Mkuu yeyote wa Pakistani, Imran Khan na Shehbaz Sharif, wakati wa urais wake wa miaka minne. Hilo lilionekana kama dharau nchini Pakistani.
Kamanda wa jeshi la Pakistani, Asim Munir, na makamanda wengine wa kijeshi, wanaamini kwamba kurejea kwa Trump Ikulu ya White House kuliiwezesha Pakistani kupata fursa ya kurekebisha uhusiano wake na Amerika, ambao ulikuwa umeganda wakati wa utawala wa Biden, ambaye alikabidhi usimamizi wa uhusiano na Pakistani kwa Pentagon. Katika muktadha huu, Asim Munir aliweka mkakati wa kumridhisha Trump, kwani imejulikana sana miongoni mwa viongozi wa kitaifa na wakuu wa nchi kwamba anapenda viongozi wanaomsifu, wanatii matakwa yake, na kumsaidia kupata kibali cha msingi wake wa uchaguzi.
Ili kupata uungwaji mkono wa Trump, Asim Munir alikubali ombi la Trump la kukamatwa kwa mpangaji mkuu anayedaiwa wa shambulio la uwanja wa ndege wa Kabul mnamo Agosti 2021, ambalo liliwaua wanajeshi kumi na tatu wa Amerika na kumkabidhi. Ikizingatia maslahi ya kibiashara ya Trump katika sarafu fiche, Pakistani ilitangaza kuundwa kwa Baraza la Sarafu Fiche la Pakistani, na Mkuu wa Baraza hilo, Bilal bin Thaqib, alitembelea Ikulu ya White House na kufanya mkutano wa kina na Robert Ho Haines, Mkurugenzi Mtendaji wa Baraza la Rasilimali Dijitali la Trump. Hii ilifuatiwa na ziara ya Jenerali Asim Munir katika Ikulu ya White House na kukutana na Trump, ambapo aliahidi kuunga mkono mpango wa Amerika wa kujenga Mashariki ya Kati mpya.
Majenerali wa Pakistani pia wanafahamu maslahi ya Amerika katika madini adimu ya ardhini, na wanatoa wito wa uwekezaji wa Amerika katika sekta ya madini ya Pakistani. Pakistani pia ilitangaza haraka nia yake ya kujadiliana na utawala wa Trump na kufikia makubaliano ya kibiashara baada ya Trump kutangaza kutoza ushuru wa asilimia 29 kwa Pakistani. Pakistani pia ilimteua Trump rasmi kwa Tuzo ya Amani ya Nobel kwa kutambua "busara yake bora ya kisiasa"! Hili ni tangazo ambalo lilizua hasira kubwa dhidi ya watawala wa Pakistani. Sasa, watawala wa Pakistani wanatumai ziara ya Trump nchini Pakistan, na wanaichukulia kuwa mafanikio na heshima kubwa kwao!
Ni usaliti mkubwa, aibu na dharau kwa watawala wa kijeshi wa Pakistani kuharakisha kumtumikia Amerika na rais wake Trump, kwa matumaini ya kupata kibali chao. Sera hii ya maridhiano wanayoifuata kuelekea Amerika inapingana kabisa na maoni ya umma ya Pakistani. Waislamu wa Pakistani wanamchukia Trump na wanamwona, yeye na mtangulizi wake Biden, kama wauaji wa Gaza. Waislamu wa Pakistani walishtuka walipoona kamanda wao wa jeshi akila chakula cha mchana na rais wa Amerika, ambaye anasimamia na kuunga mkono shambulio la chombo cha Kiyahudi dhidi ya Iran.
Tofauti kati ya watawala wa Pakistani ambao wanaharakisha kutumikia maslahi ya Amerika, na Waislamu wa Pakistani ambao wanataka kupigana na Amerika na washirika wake India na chombo cha Kiyahudi kinachokalia ardhi, ni wazi kwa kila mtu. Pakistani iko tayari kwa mapinduzi. Waislamu wa Pakistani, kama Waislamu kila mahali, walishtushwa na mauaji ya Gaza, na wanawalaumu watawala wa Waislamu kwa kushindwa kwao kukusanya majeshi yao ili kukomboa Palestina na kuwasaidia ndugu zao.
Kuna hamu kubwa nchini Pakistani ya kuwaondoa watawala wake vibaraka wa Amerika. Mapinduzi ya Syria na Bangladesh yamewapa Waislamu wa Pakistani tumaini la uwezo wao wa kuwaondoa watawala wao. Kipengele pekee kinachokosekana kwa mapinduzi nchini Pakistani dhidi ya watawala hawa ni uamuzi wa vikosi vya jeshi vyenye nguvu vya Pakistani kuchukua hatua kwa uthabiti kwa niaba ya maoni ya umma nchini Pakistani na kupitisha uongozi mpya na maono mapya kwa Pakistani, bila utumwa kwa Amerika na utegemezi kwa mfumo wake wa kimataifa. Ushindi wa hivi majuzi wa Pakistani dhidi ya India umeipa jeshi ujasiri katika uwezo wake. Nguvu zake zinatosha kujenga Mashariki ya Kati mpya kulingana na umoja wa nchi zote za Kiislamu chini ya Khilafa Rashidun ya pili kwa njia ya Utume. Hili ndilo dira tunalowaalika Waislamu wote kufanya kazi kwa ajili yake. Mwenyezi Mungu alisema: ﴿Enyi mlio amini! Itikieni wito wa Mwenyezi Mungu na Mtume anapo kuwaiteni kwenye lile linalo kuhuisheni﴾.
Imeandikwa kwa Idhaa ya Afisi ya Habari Kuu ya Hizb ut Tahrir
Yahya Malik - Wilaya ya Pakistani