Uongozi wa Pakistani unaandaa mkutano wa kikanda wa ulinzi
ili kuendeleza maslahi ya Amerika badala ya kuhamasisha kuisaidia Gaza
Habari:
Kitengo cha habari cha jeshi la Pakistani, Uhusiano wa Umma wa Jeshi, kilitangaza mnamo Julai 26, 2025 kwamba Pakistani ilikuwa imeandaa mkutano wa wakuu wa majeshi wa ulinzi wa kikanda huko Islamabad, kwa ushiriki wa viongozi wakuu wa kijeshi kutoka Merika, Kazakhstan, Kyrgyzstan, Tajikistan, na Uzbekistan. Taarifa ya kitengo cha habari ilisema kwamba "tukio hili la pande nyingi ni hatua muhimu kuelekea kuimarisha ushirikiano wa kiusalama wa kikanda, diplomasia ya kijeshi, na mazungumzo ya kimkakati kati ya nchi zinazoshiriki." Mkutano huo ulifanyika chini ya kauli mbiu ya "Kuimarisha uhusiano, kuhakikisha amani," na ulilenga kukuza ushirikiano wa kiusalama, kuendeleza programu za mafunzo, na kubadilishana mazoea bora katika kukabiliana na ugaidi na juhudi zingine za ulinzi na usalama.
Maoni:
Watawala wa Pakistani wamethibitisha tena kujitolea kwao kwa maono ya kikanda ya Amerika kwa kuandaa mkutano muhimu wa kiusalama wa kikanda uliowajumuisha viongozi wa majeshi ya Waislamu kutoka Pakistani na nchi za Asia ya Kati chini ya usimamizi wa Amerika. Wakati majeshi ya Waislamu yanahamasishwa kuchukua hatua za haraka kuokoa Gaza na kung'oa chuki ya Wayahudi, kamanda wa jeshi la Pakistani anashughulika na mkutano unaokusudiwa kuelekeza eneo hilo kuelekea ajenda ya Amerika, kupitia kupambana na kile kinachoitwa "Uislamu wa kisiasa" kwa njia iliyoratibiwa chini ya kivuli cha kupambana na ugaidi na itikadi kali.
Mkutano huu ni mpango wa kipekee ulioanzishwa na kamanda wa jeshi la Pakistani, uliowakutanisha viongozi wa kijeshi kutoka Asia ya Kati na Kamandi Kuu ya Amerika. Amerika iliwakilishwa na Jenerali Michael E. Kurilla, kamanda wa Kamandi Kuu ya Amerika. Mkutano huo ulilenga kuimarisha kujitolea kwa malengo matatu makuu ya Amerika katika eneo hilo: kukabiliana na ugaidi, utulivu wa kikanda, na uratibu wa kijeshi, kama inavyoonekana wazi katika taarifa ya mkutano. Mihimili hii mitatu inaunda kiini cha malengo ya Kamandi Kuu ya Amerika, na Pakistani ni msingi mkuu wa kufanikisha malengo haya.
Ili kuelewa harakati za Amerika na umuhimu wa Pakistani katika muktadha huu, ni muhimu kusoma mandhari pana ya kijiografia na kisiasa:
Kwanza: Asia ya Kati na Kusini ni mikoa miwili mikuu ya Kiislamu ambapo nguvu ya binadamu kutoka Asia Kusini hukutana na utajiri wa nishati wa Asia ya Kati. Afghanistan ni daraja linalounganisha mikoa hiyo miwili. Kwa sababu ya eneo la kimkakati, idadi ya watu, na rasilimali asili, ushindani wa kimkakati kati ya Amerika, Urusi, na Uchina umeongezeka katika mikoa hii, ambapo mashindano yanazingatia upatikanaji wa nishati, madini muhimu, na korido za kuunganisha. Kwa sababu ya udhaifu wa Urusi kama matokeo ya vita virefu na Ukraine, Amerika na Uchina zimekuwa wahusika muhimu katika Asia ya Kati na Kusini. Licha ya kujiondoa kwa Amerika kutoka Afghanistan baada ya kushindwa vibaya na Taliban, imeingia tena katika eneo hilo kupitia mawakala wake waaminifu katika taasisi ya kijeshi ya Pakistani.
Pili: Kurudi kwa utawala wa Republican unaoongozwa na Trump mwenye kiburi kumefungua njia kwa uongozi wa jeshi la Pakistani kuchukua jukumu kubwa zaidi katika mipango ya kikanda ya Amerika. Utawala wa Biden umepunguza kiwango cha ushiriki wake na maslahi yake na Pakistani baada ya kujiondoa kutoka Afghanistan isipokuwa ushirikiano katika kupambana na Uislamu. Trump alikutana na kamanda wa jeshi la Pakistani, Jenerali Asim Munir, wakati wa chakula cha mchana katika hatua isiyo ya kawaida wakati wa ziara yake Amerika. Munir pia alikutana na Waziri wa Mambo ya Nje wa Amerika, Marco Rubio, na maafisa wengine wa Amerika kupata miongozo yake mipya.
Kuandaa viongozi wa ulinzi wa nchi za Asia ya Kati baada ya mikutano hii ya ngazi ya juu kati ya Pakistani na Merika kunaonyesha kwamba Pakistani iko tayari kuelekeza Asia ya Kati na Kusini kwa mujibu wa maslahi ya Amerika. Kuna uwezekano kwamba mashaka ya Urusi na Uchina kuelekea Pakistani yataongezeka baada ya matukio haya. Mbali na kuhakikisha ushirikiano wa kiusalama wa kikanda chini ya usimamizi wa Amerika, Pakistani inaharakisha kasi ya miradi ya uunganisho wa kikanda kama vile njia mpya za biashara na usafiri. Kwa mfano, Pakistani, Afghanistan, na Uzbekistan hivi karibuni zilitia saini mkataba wa mfumo wa pande tatu kuhusu mradi wa reli. Miradi mingine inayoendelea katika hatua tofauti ni: bomba la gesi (Turkmenistan - Afghanistan - Pakistani - India), mradi wa reli unaopitia Afghanistan, mradi wa CASA-1000 wa kusafirisha umeme kati ya Asia ya Kati na Kusini, na mradi wa TUTAP wa kuunganisha nishati kati ya Turkmenistan, Uzbekistan, Tajikistan, Afghanistan, na Pakistani. Miradi hii yote inaungwa mkono na Amerika na inalenga kukata uhusiano wa nchi za Asia ya Kati na Urusi na Uchina kupitia Pakistani.
Inasikitisha kwamba Merika na nguvu zingine kubwa zinatumia vibaya maeneo ya Kiislamu yaliyo matajiri kwa rasilimali za nishati, madini, na uwezo wa kijeshi. Kuanguka kwa Khilafah mikononi mwa Magharibi kafiri mwaka 1924 BK kulisababisha kuvunjwa kwa nguvu ya Umma wa Kiislamu na kuigawanya katika nchi bandia. Pamoja na kuvunjika huku, Magharibi ililazimisha wasomi tawala waliohusiana nayo kiitikadi, walio na upeo mdogo na ambao ni kikwazo cha kuunganisha nchi za Waislamu chini ya Khilafah. Uongozi wa kijeshi wa Pakistani hautofautiani na taasisi zingine za kilimwengu katika nchi za Kiislamu. Lau kama ingekuwa na nia ya kweli na maono ya uaminifu, ingeunganisha nishati katika Ghuba na Asia ya Kati na nguvu ya binadamu katika Asia Kusini chini ya Khilafah. Bado inawezekana, na imekuwa ya haraka zaidi kutokana na udhaifu wa Amerika na utegemezi wake kwa Pakistani kutekeleza majukumu yake ya kikanda. Muhimu zaidi, Umma uko tayari kwa mabadiliko makubwa.
Kwa hivyo, wale walio waaminifu katika taasisi ya kijeshi ya Pakistani wanapaswa kuharakisha kuanzisha Khilafah ili nguvu ya Umma irejeshwe, na kukomesha mauaji na uvamizi katika ardhi za Waislamu. Khilafah ijayo itaunganisha viongozi wa majeshi ya Waislamu kuchukua hatua za ukombozi wa Palestina na Kashmir badala ya kupoteza muda katika mikutano mitupu inayotumikia ajenda za kigeni. Mtume ﷺ alisema: «Hakika Mwenyezi Mungu amenikunjia ardhi nikaona mashariki yake na magharibi yake, na hakika umma wangu utafikia utawala wake yale niliyokunjiwa mimi.» Sahih Muslim. Na Mwenyezi Mungu Mtukufu amesema katika Qur'ani Tukufu: ﴿Yeye ndiye aliyemtuma Mtume wake kwa uongofu na dini ya kweli ili aipe ushindi juu ya dini yote, japokuwa washirikina watachukia.﴾.
Imeandikwa kwa ajili ya idhaa ya Ofisi ya Habari Kuu ya Hizb ut-Tahrir
Muhammad Saljuq - Wilaya ya Pakistani