Alsudani Aelezea Mashambulizi dhidi ya Qatar Kama "Tukio la Kushtusha" na Kutoa Wito wa Kutangazwa "Muungano wa Kiislamu"
Habari:
Waziri Mkuu Mohammed Shia al-Sudani alilaani Jumapili, Septemba 14, 2025, shambulio la Israel dhidi ya Qatar, akitoa wito wa kuanzishwa kwa muungano wa Kiislamu wa pamoja kukabiliana na uchokozi. Katika taarifa iliyoandikwa na "Baghdad Leo", Alsudani alielezea shambulio hilo kama tukio la kushtusha na ukiukaji wa sheria na kanuni zote za kimataifa, akisisitiza kwamba linathibitisha mbinu ya fujo ya serikali ya uhalifu ya Israel. Alizingatia shambulio hili kama ukiukaji dhidi ya nchi dada na tishio kwa usalama wake na usalama wa nchi zote za kanda. Katika muktadha wa kukabiliana na tishio hili, Alsudani alitoa wito wa kutangazwa kwa muungano wa kisiasa, kiusalama na kiuchumi wa Kiislamu kwa nchi za Kiislamu, akibainisha kuwa hakuna kinachozuia nchi za Kiislamu kuwa na muungano katika mfumo wa kikosi cha pamoja cha usalama kwa ajili ya ulinzi. Waziri Mkuu alionya kwamba "uchokozi hautasimama Qatar" akisisitiza kwamba nchi za Kiislamu zina "rasilimali kadhaa ambazo zinaweza kuwekezwa ili kukabiliana nazo," akiongeza kuwa "serikali ya Israel imedharau kila kitu na kile kinachotokea Gaza kwa zaidi ya miaka miwili ni mauaji ya kimfumo." (Baghdad Leo)
Maoni:
Tukio la kushtusha ni jambo la dharura ambalo mtu, kikundi au taifa hushangazwa nalo bila kuwa tayari kwa jambo hili, na kusababisha usumbufu katika tabia zao. Ikiwa hawana msingi wa kimsingi wa kiitikadi kwa kila fikra, na matibabu na suluhisho za shida za maisha, watabaki katika maisha yasiyo na utulivu.
Suala la shambulio la chombo cha Kiyahudi dhidi ya Qatar na wito wa Alsudani wa kutangazwa kwa muungano wa Kiislamu kukabiliana na uchokozi, linatuongoza kwa swali muhimu, nalo ni: Je, uchokozi wa Wayahudi dhidi ya nchi ya Kiislamu ni jambo jipya?! Au ilianza tangu kutangazwa kwa kuanzishwa kwa chombo cha Kiyahudi mnamo mwaka 1948, bali tangu kuangushwa kwa dola ya Waislamu, Ukhalifa wa Ottoman na kugawanywa kwake katika zaidi ya nchi hamsini dhaifu na kulazimisha mamlaka ya Uingereza juu ya Palestina na kisha kuikabidhi kwa viumbe duni zaidi vya Mungu, Wayahudi, kulingana na vita vya maigizo kama vile vilivyotokea mwaka 1948, 1956 na 1967, na kuundwa kwa Shirika la Ukombozi la Palestina na Jumuiya ya Nchi za Kiarabu ili suala la kukabidhi Palestina liwe rasmi, na pia kuundwa kwa Shirika la Ushirikiano wa Kiislamu ambalo limepotoshwa akili kutoka kwa suluhisho la kweli kwa shida zote za Waislamu, ambayo kwa sababu hiyo Palestina ilipotea na watawala wasiojali kitu kwao ila uadui na uvunjaji wa ahadi walitawazwa juu ya shingo za Waislamu?
Kwa hivyo, ni muhimu kwa kila Muislamu kurekebisha dira yake na kufanya kazi na wale wanaofanya kazi kurejesha maisha ya Kiislamu kwa kuanzisha dola ya Ukhalifa kulingana na mtaala wa Unabii, ambayo inakusanya majeshi, inaondoa mipaka bandia kati ya Waislamu, inaachilia nchi za Kiislamu zilizokaliwa, haswa ardhi ya Isra na Mi'raj, inalinda mipaka, na kueneza haki na ustawi katika sehemu zote za ulimwengu. Mwenyezi Mungu Mtukufu amesema: ﴿Na hatukukutuma ila uwe rehema kwa walimwengu﴾.
Iliandikwa kwa ajili ya Redio ya Ofisi Kuu ya Habari ya Hizb ut-Tahrir
Abdullah Abdul Hamid - Jimbo la Iraq