Mfuriko U hai na Unaendelea
Habari:
Wapatanishi wanatia saini makubaliano ya Trump ya kusitisha mapigano huko Gaza. (Oktoba 13, 2025 BK)
Maoni:
Operesheni ya Mfuriko wa Al-Aqsa haikuwa tukio la kupita tu na kuishia na makubaliano ya mhalifu Trump na nyuma yake dola ya ukafiri Amerika, mfuasi rasmi wa chombo cha Kiyahudi, bali ni cheche iliyowaka katika mioyo ya Waislamu na kufungua akili na mioyo yao na wakaona udhalili na unyonge wa watawala wao wasaliti na wakatambua unafiki wa wadai wa ubinadamu na haki za wanawake na watoto, na waliamini kwamba sheria na mikataba ya kimataifa si chochote ila silaha kwa makafiri dhidi ya Uislamu na Waislamu.
Operesheni hii imefichua kwamba jambo ambalo Magharibi kafiri hulihofia na kulitia wasiwasi zaidi ni Waislamu kutoka nje ya utiifu wao, kwa hivyo walifanya kazi kwa bidii kwa nguvu zao zote na silaha zao zote na kwa ugaidi wote, ukatili na uhalifu kuharibu Gaza na kuua wanawake na watoto mbele na masikioni mwa ulimwengu kwa lengo moja, nalo ni kuzima kiungo hiki hai katika mwili wa umma, wakipuuza kanuni za ustaarabu wao ambao unakaribia kutoweka, kwa idhini ya Mwenyezi Mungu.
Kuamka kwa umma kunatisha mfumo wa kimataifa, na ukhalifa ndio hofu ambayo inawasumbua, na yale ambayo Gaza imeonyesha ya uvumilivu, subira na imani kwa Mungu licha ya hofu na mauaji, imewatisha zaidi na kutambua kuwa kinachotokea ni hadithi ya utukufu, kwa hivyo kusimama imara mbele ya nguvu kubwa ni wakati muhimu katika historia.
Lazima tutambue kikamilifu kwamba vita dhidi ya Waislamu haitasimama, na kwamba makafiri hawaoni amani isipokuwa kwa kukosekana kwa Uislamu, kwa hivyo watafanya kazi na mipango na njia zote kutushughulisha na kutukatisha tamaa na vita, hila na njama ili tubaki umma uliogawanyika ambao hauna uamuzi, na jambo la muhimu zaidi leo ni kufanya kazi kwa bidii ili kuondokana na mfumo wa kimataifa na zana zake na kujitenga nao na kujitolea katika njia ya kuunganisha umma na kuanzisha ukhalifa wa pili juu ya mfumo wa unabii ambao unalinda haki za Waislamu na kulipiza kisasi kwa maadui zao.
Imeandikwa kwa Redio ya Ofisi ya Habari Kuu ya Hizb ut-Tahrir
Sadiq Al-Sarari - Jimbo la Yemen