Uelewa Unahitajika Leo Kuliko Wakati Wowote
Habari:
Watumiaji wa mitandao ya kijamii nchini Yemen na nchi zingine za Kiislamu waliitikia kwa furaha habari za Iran kushambulia taasisi ya Kiyahudi jioni ya Ijumaa, 2025/6/13.
Maoni:
Kitu kinachofurahisha mioyo yetu zaidi ni kuona adui mkuu wa Waislamu, taasisi ya Kiyahudi, akishughulikiwa vikali, na Waislamu wamekuwa wakitarajia tangu kuanza kwa uchokozi wa kikatili dhidi ya ndugu zetu huko Gaza, taifa litakalowasaidia hawa wanyonge na kusimama kidete dhidi ya mauaji ya kimbari dhidi yao, lakini usaliti na uhafidhina wa watawala wa Kiislamu ulikuwa mkubwa zaidi na mshtuko mkubwa zaidi katika mioyo, kana kwamba matukio haya yaliandaliwa na Mwenyezi Mungu ili kuwafichua na kuchochea hisia na akili za Waislamu kutafuta suluhisho bora na la pekee la kusaidia Uislamu na Waislamu.
Mzozo kati ya Iran na taasisi ya Kiyahudi sio mzozo kati ya Uislamu na ukafiri, lakini ni mzozo wa ushawishi na maslahi. Taasisi ya Kiyahudi inaona kuwa Iran ndiyo inayoshindana nayo katika ushawishi na udhibiti wa nchi za Kiislamu na hata katika kuwaua, na zote mbili hazivuki mipaka iliyowekwa na bibi yao Amerika. Hapa, umma haupaswi kutosheka na hisia, lakini lazima ujue maadui zake na ujifunze kutoka kwa hila na njama zote ambazo umepitia, na kukata uelewa bandia ambao mkoloni hupanda katika akili zetu na kuondoa ujinga, na hii haiwezekani isipokuwa kwa uelewa sahihi ambao unatokana na kuelewa ukweli kwa usahihi na kuunganisha uelewa huu na dhana za Uislamu.
Mwenyezi Mungu ameandaa sababu, na labda huu ni uchungu wa umma kuamka kutoka katika uzembe wake na kujua kwamba kipimo pekee ni kutumia sheria ya Mungu. Je, mtu ambaye hahukumu kwa yale ambayo Mungu ameyateremsha anawezaje kuusaidia Uislamu na Waislamu?! Na kila mtu atambue kwamba furaha ya kweli itakuwa ni kuanzishwa kwa dola ya pili ya Khilafa Rashidah kwa misingi ya Utume ambayo itatekeleza Uislamu, kuunganisha umma, na kuhamasisha majeshi kung'oa taasisi ya Kiyahudi kutoka mizizi yake. Chama pekee ambacho kina mradi wa dola hii na katiba yake kutoka katika Qur'ani na Sunnah ni Hizb ut-Tahrir, kwa hivyo kuweni pamoja na wale walio waaminifu kama itikio la amri ya Mwenyezi Mungu na kwa uhakika wa ushindi wake.
Mwenyezi Mungu amesema: ﴿Enyi mlio amini! Itikieni wito wa Mwenyezi Mungu na Mtume anapo kuita kwenye jambo lile ambalo litakupa uhai. Na jueni kwamba Mwenyezi Mungu huingilia baina ya mtu na moyo wake, na kwamba kwake Yeye mtakusanywa.﴾
Imeandikwa kwa ajili ya Idhaa ya Afisi ya Habari Kuu ya Hizb ut-Tahrir
Sadiq Al-Sarari - Wilaya ya Yemen