Amerika Yaweka Vikwazo kwa Mamlaka ya Abbas na Jumuiya ya Wayahudi Yabariki
Habari:
Marekani Alhamisi ilitangaza kuweka vikwazo kwa maafisa wa mamlaka na shirika la ukombozi na kukataa kuwapa visa vya Amerika kama adhabu kwa kuuingiza mgogoro wao na jumuiya ya Wayahudi katika medani ya kimataifa, na waziri wa mambo ya nje wa jumuiya ya Wayahudi aliishukuru Amerika kwa hilo akisema: "Mamlaka ya Palestina lazima ilipe gharama ya uchochezi wake dhidi yetu." (Alarabiya, 2025/7/31)
Maoni:
Idara ya ujasusi ya Mamlaka ya Abbas haachi kuwaita Wapalestina na kuwahoji kwa tuhuma za uchochezi dhidi ya jumuiya ya Wayahudi, hii ni baada ya kukamilisha kazi kubwa ya ujasusi katika kubaini silaha yoyote ya Kipalestina ambayo inaweza kutumika dhidi ya uvamizi, na kazi hii inaendelea, bali vyombo vya usalama vya Mamlaka ya Abbas vilipigana na wapiganaji katika kambi ya Jenin na kumwadhibu mtu yeyote miongoni mwa wanachama wake aliyekataa kujiunga na kazi hii chafu, na watu wanalalamika kuhusu kubanwa kwa misikiti na kuzuia wahubiri kuzungumzia mauaji ya Wayahudi huko Gaza. Mamlaka ya Abbas inathibitisha katika kila kona kwamba ni miongoni mwa matoleo machafu zaidi ya tawala za Kiarabu vibaraka kwa usaliti na aibu, na inafanya yote hayo kwa matumaini kwamba itakubaliwa na Amerika na jumuiya ya Wayahudi.
Lakini mabwana wa mamlaka huko Washington na Tel Aviv wanakiri hilo tu wakati linaendana na mipango yao, katika hatua yake ya kwanza, mamlaka ilipata sherehe huko Washington na kwa Wayahudi badala ya vitendo vyake vya kuwatiisha watu wa Palestina, na hizo zilikuwa mahitaji ya hatua hiyo, lakini kwa kuwa matukio ya tarehe 7 Oktoba 2023 yalithibitisha kwamba watu wa Palestina hawawezi kunyenyekea na kutiishwa na kwamba daima wanapata njia yao ya kupigania na kudai haki zao, thamani ya Mamlaka ya Abbas imeanguka licha ya mafanikio yake ya wazi katika baadhi ya maeneo ya Ukingo wa Magharibi, na jumuiya ya Wayahudi ilikataa kuirejesha Ukanda wa Gaza.
Na leo, jumuiya ya Wayahudi inatangaza wazi kukataa kuanzishwa kwa dola la Palestina ambalo liliudanganya shirika la ukombozi kulianzisha baada ya miaka 5 ya makubaliano ya Oslo mwanzoni mwa miaka ya tisini, na utawala wa Trump unatangaza uungaji mkono wake kwa hatua hizi za jumuiya ya Wayahudi, bali ilieleza kukataa kwake madai ya baadhi ya nchi za Magharibi kama vile Ufaransa kutambua dola la Palestina, ingawa halitoi wala halicheleweshi chochote katika kivuli cha udhibiti kamili wa jumuiya ya Wayahudi juu ya Ukingo wa Magharibi, kana kwamba Amerika na jumuiya ya Wayahudi wanamwambia Abbas na vibaraka wake jukumu lenu limekwisha, kwa hivyo ikaanza kuwaadhibu kwa kisingizio cha kuuingiza mgogoro katika medani ya kimataifa, ilhali umeingizwa katika medani ya kimataifa tangu mwaka 1948, yaani tangu kuanzishwa kwa jumuiya ya Wayahudi.
Huu ndio mwisho wa msaliti ambaye hajali watu wake na taifa lake, lakini kina cha usaliti kwa Mamlaka kinaipelekea kutoa huduma zaidi na zaidi za kiusalama ili Amerika na jumuiya ya Wayahudi zifanyie marejeo vikwazo vilivyowekwa kwa maafisa wake, na kwamba njia ya Mamlaka na watu wa Palestina imefungwa kabisa.
Imeandikwa kwa ajili ya idhaa ya Ofisi Kuu ya Habari ya Hizb ut-Tahrir
Bilal Al-Tamimi