Marekani Inaandaa Njama Mpya Baada ya Umma Kufichua Njama Yake ya Awali na Kuibatilisha
Habari:
Makundi yenye silaha ya Rohingya yameanza kuajiri watu kutoka kambi za wakimbizi huko Cox's Bazar kushiriki katika mapigano dhidi ya Jeshi la Arakan katika Jimbo la Rakhine. Ripoti iliyotolewa na Kundi la Kimataifa la Migogoro, iliyopewa jina la "Bangladesh/Myanmar: Hatari za Uasi wa Rohingya," ilifichua kwamba makundi ya Rohingya yamekuwa na shughuli nyingi zaidi baada ya ushindi wa Jeshi la Arakan dhidi ya Jeshi la Myanmar huko Rakhine, na kwamba yamekubali kushirikiana dhidi yake, ingawa jeshi hili linawakilisha Wabuddha wengi katika eneo hilo. (Gazeti la Business Standard, Juni 18, 2025)
Maoni:
Kinachoitwa njia ya kibinadamu ya jimbo la Rakhine nchini Myanmar, ilikuwa mradi wa Kimarekani kabisa, uliolenga kuyumbisha serikali ya kijeshi nchini Myanmar inayoungwa mkono na Uingereza. Mpango huu uliundwa kimsingi kuwafukuza serikali ya Tatmadaw kutoka maeneo ya Kyaukpyu na Sittwe, ngome za mwisho za utawala wa kijeshi katika Jimbo la Rakhine. Lakini, kwa sababu ya Mwenyezi Mungu na kisha kutokana na msimamo thabiti wa watu wa Bangladesh, ikiwa ni pamoja na vikosi vya jeshi, dhidi ya mradi huu, neno njia ya kibinadamu limekuwa sawa na "tishio kwa usalama wa taifa la Kibengali" na "ulaghai mchafu wa Marekani." Kwa hivyo Amerika ililazimika kufikiria upya mpango wake, na ikageukia kuongeza mwelekeo wa Kiislamu kwenye eneo hilo ili kupata huruma ya maoni ya umma wa Kibengali, na kuitumia katika michezo yake mibaya ya kijiografia.
Jeshi la Arakan, ambalo linawakilisha Wabuddha wengi katika Jimbo la Rakhine, ndio kiini cha vita vya uwakala vinavyopiganwa na Amerika dhidi ya utawala wa kijeshi, wakati Kundi la Uokoaji la Waislamu wa Rohingya linawakilisha wachache katika jimbo hilo. Hata hivyo, makundi yote mawili yanahusiana na Marekani chini ya "Sheria ya Burma ya Umoja kupitia Uwajibikaji Mkali wa Kijeshi 2022" ambayo inajumuisha waziwazi kuunga mkono upande wowote unaopinga utawala wa kijeshi. Mnamo 2023, sheria hii ilijumuishwa katika Sheria ya Uidhinishaji wa Ulinzi wa Kitaifa wa Marekani, ili kutoa fedha na msaada wa vifaa vya kijeshi kwa mtu yeyote anayepigana na serikali ya kijeshi.
Baada ya Marekani kutambua kufichuliwa kwa mpango wake kuhusiana na njia ya kibinadamu, iligeukia kuwezesha jukumu la makundi yenye utambulisho wa Kiislamu ili kurejesha uungwaji mkono wa maoni ya umma wa Kibengali. Katika muktadha huu, tunaona ongezeko la ghafla la shughuli za uajiri ndani ya kambi za Rohingya. Haishangazi kwamba Amerika itatumia kila njia inayowezekana kutekeleza mipango yake mibaya katika Ghuba ya Bengal. Lakini, umma wa Kiislamu lazima ujitenge na mipango hii. Lazima itambue kwamba uasi wowote wa silaha - hata ukiitwa jihad - chini ya usimamizi na msaada wa moja kwa moja kutoka Amerika au nchi yoyote ya kikafiri, hautasuluhisha shida zake zozote. Uzoefu uliopita huko Syria, Kurdistan, Balochistan, Kashmir, na kwingineko, umeonyesha kuwa upinzani haukuleta ushindi au heshima kwa umma, lakini damu ya Waislamu ilimwagwa kwa faida ya kafiri mkoloni. Ikiwa ni lazima kutoa dhabihu ya damu na roho, basi dhabihu hii iwe ya kweli kwa ajili ya sababu safi ya Kiislamu.
Kwa kuongezea, Waislamu wa Bangladesh lazima waachane na mtazamo wa kitaifa kuelekea Waislamu wa Rohingya. Utaifa ndio sumu hatari ambayo imevunja umoja wa umma wa Kiislamu na kuifanya iwe rahisi kwa maadui zake. Waislamu lazima watafakari juu ya mafanikio ya mababu zao ambao waliunganisha makabila na rangi tofauti chini ya bendera ya "La ilaha illa Allah Muhammad Rasul Allah" kuunda taifa moja lenye kuogopwa. Kwa hivyo, Rohingya hawapaswi kuonekana kama wakimbizi au wageni, lakini kama ndugu katika dini, na wanapaswa kukumbatiwa kama Ansar wa Madina walivyokumbatia wahajiri wa Makka. Maslahi ya Waislamu nchini Bangladesh hayawezi kutenganishwa na maslahi ya Rohingya, bali ni moja, na lazima yaunganishwe chini ya uongozi wa Khalifa mwadilifu. Mwenyezi Mungu alisema: ﴿Hakika huu ni umma wenu, umma mmoja, na Mimi ndiye Mola wenu Mlezi, basi niabuduni﴾. Khalifa pekee ndiye anahakikisha ukombozi wa kweli wa Arakan, na anazikomboa nchi za Kiislamu kutoka kwa uvamizi wa kikafiri, na pia anazikomboa mioyo na akili za Waislamu kutoka kwa mawazo ya kikafiri kama vile utaifa na ulaikini. Hapo tu ndipo njama za kichwa cha ukafiri; Amerika, zinaweza kubatilishwa kabisa.
Imeandikwa kwa Radio ya Afisi ya Habari Kuu ya Hizb ut Tahrir
Risat Ahmed - Wilaya ya Bangladesh