Marekani Yataka Kurekebisha Ramani ya Njia ya Mgogoro wa Yemen kwa Kuwavua Silaha Wahouthi
Habari:
Shinikizo kutoka Marekani na Saudi Arabia kwa Wahouthi kurekebisha ramani ya njia inajumuisha kuwavua silaha Wahouthi. (Gazeti la Al-Akhbar la Lebanon, 4 Novemba 2025).
Maoni:
Saudi Arabia ilikuwa imefichua ramani ya njia kati yake na Wahouthi kwa baraka za Amerika inayohusiana na kusitisha mapigano, kufungua barabara na viwanja vya ndege, na kulipa mishahara, kisha kuanza mazungumzo ya kisiasa yanayoongoza kwa kuunda serikali kwa usawa na serikali ya Rashad al-Alimi, lakini serikali ya Al-Alimi ilikataa kwa kuwa inawapa Wahouthi karibu theluthi mbili ya mapato ya mafuta na marupurupu mengine.
Na tena mazungumzo yamerudi kuhusu kufufua mchakato wa amani nchini Yemen, na Wahouthi walisema wako tayari kutekeleza ramani hiyo ya njia, na vile vile waziri wa mambo ya nje wa Saudi Arabia, Faisal bin Farhan, alirudia kwamba ramani ya njia iko tayari kutekelezwa. Wakati viongozi wa Baraza la Urais la Yemen na waziri wake wa mambo ya nje wanasema haifai tena na wanadai suluhisho la kisiasa kulingana na marejeleo yao matatu, ambayo ni: Mpango wa Magharibi unaoitwa Mpango wa Ghuba, ambao chini yake marehemu Ali Abdullah Saleh aliondolewa madarakani, na matokeo ya Mkutano wa Kitaifa wa Mazungumzo, uliofanyika chini ya uangalizi wa Magharibi na kusababisha mfumo wa utawala wa shirikisho katika mfumo wa jamhuri ya kidemokrasia iliyoanzishwa kwa uhuru, uwezeshaji wa wanawake, na kupambana na ugaidi, na rejeleo la tatu ni azimio la Umoja wa Mataifa 2216 ambalo linawaona Wahouthi kama wanamgambo walioteka nyara serikali! Lakini Saudi Arabia na Wahouthi wanashikilia ramani ya njia ya Amerika ambayo haikutaja marejeleo hayo.
Katika muktadha huo huo, Baraza la Ushirikiano la Ghuba lilisititiza kwamba suluhisho nchini Yemen linapaswa kuzingatia marejeleo matatu bila kuathiri umoja wa Yemen, ikiashiria kukataa kwao mradi wa kugawanya Yemen, ambao unaungwa mkono na Baraza la Mpito, lililoanzishwa na UAE mnamo 2017.
Na tukirudi kwenye mazungumzo juu ya kurejea kwa mchakato wa kisiasa, gazeti la Al-Akhbar la Lebanon lilifichua kuwa kuna marekebisho ambayo yatafanywa na Amerika na Saudi Arabia ambayo yanajumuisha kuwavua silaha Wahouthi, na inaonekana kuwa marekebisho haya yatakuwa ili serikali ya Al-Alimi, inayoungwa mkono na Uingereza, ikubali. Huku ushindani wa kimataifa ukiendelea kwa ushawishi nchini Yemen, watu huko wanabaki chini ya mamlaka ya mgawanyiko wa kijeshi na kisiasa kati ya Saudi Arabia na UAE, ambao unawakilisha ushindani kati ya Amerika na Uingereza kwa ushawishi na utajiri nchini Yemen. Tawakkol Karman alionyesha ushindani huo akitoa maoni yake kuhusu ufunguzi wa uwanja wa ndege wa Mokha, unaoendeshwa na mwanachama wa Baraza la Urais, Tariq Saleh, na unaoendeshwa chini ya ushawishi wa UAE, akisema kwamba yeye ni wakala wa wakala (akimaanisha Tariq Saleh na UAE kama wakala wa Uingereza), na akasema kwamba Uingereza ilijenga uwanja wa ndege wa Aden, nyumba na hospitali huko kwa ajili ya kutumikia askari wake na kuacha makazi mengine yakivurugika, yaani, bila kujaliwa lolote, ikimaanisha kile wanachokifanya leo huko Mokha, ambako walijenga uwanja wa ndege huko kwa ajili ya kutumikia maslahi yao ya kijeshi, wakati miji yenye watu wengi haipati uangalizi wowote!
Na kilichopo ni kwamba viongozi hawa wa ndani wanaiachia nchi, masuala yake, na mali zake kwa mawakala wanaoidhibiti kwa niaba ya kafiri wa Magharibi, na wanawadanganya watu kwa itikadi za kimadhehebu, kikanda, na hata za kidini ili kuficha uhalifu wao dhidi ya nchi na watu.
Uislamu umeamrisha kutokuruhusu makafiri kudhibiti na kutawala nchi zetu. Mwenyezi Mungu anasema: ﴿Na Mwenyezi Mungu hatowapa makafiri njia ya kuwashinda Waumini﴾, na Mtume ﷺ alisema: «Hakika sisi hatuombi nuru kwa moto wa washirikina», yaani hatuwatumii kutatua masuala yetu, na Uislamu umefanya mamlaka kuwa ya Mwenyezi Mungu pekee bila mshirika yeyote kutoka kwa wanadamu katika kupanga maisha, kuunda mfumo wa utawala ndani yake, na sheria zote zinazolinda damu ya Waislamu, mali zao, na kusimamia masuala ya maisha yao kulingana na hukumu za Uislamu katika utawala, uchumi, siasa za kigeni, fedha, elimu, na zinginezo, na si kama vile watawala wa Waislamu wanafanya leo kwamba wamewafanya makafiri wa Magharibi kuwa watawala wa nchi, utawala na mifumo ya maisha, wakiidhibiti mali na mamlaka, na kuwaweka watu, ambao ndio wamiliki wa nchi na mali zake, katika umaskini uliokithiri, uharibifu na vita vinavyoendeshwa kutoka mbali na askari wa ndani!
Enyi watu wa Yemen: Hakika mfumo wa Khilafa ndio mfumo ambao Mola wenu amewaridhia, na si mfumo wa jamhuri, shirikisho la kidemokrasia, wala mfumo wa kimadhehebu, wala mfumo wa kifalme. Kusimamishwa kwa Khilafa ni jambo linalowezekana na linalopatikana, bali wakati wake umefika baada ya utawala wa kidhalimu tunaoishi nao leo. Lakini hatua ya kwanza kuelekea Khilafa iko katika kutowachukua viongozi hawa wa ndani, kaskazini na kusini, kama watawala, bali wao ni wanyang'anyi wa utawala kwa uwezeshaji kutoka kwa kafiri wa Magharibi ili iwe rahisi kwake kupora mali, kutawala nchi, njia zake, na bandari zake za kimataifa katika mfumo wa ushindani wa kikoloni kati ya nchi zao.
Basi njooni tufanye kazi na Hizb ut Tahrir kusimamisha Khilafa Rashidah ya Pili kwa njia ya Utume ili Mola wenu Subhaanahu wa Taala akuridhieni na mpate utukufu wa dunia na Akhera. Mwenyezi Mungu anasema: ﴿Hakika Sisi tutawanusuru Mitume wetu na wale walio amini katika uhai wa dunia na siku watakapo simama mashahidi﴾.
Imeandikwa kwa ajili ya Idhaa ya Afisi ya Habari Kuu ya Hizb ut Tahrir
Abdul Aziz Al-Hamid - Wilaya ya Yemen