Anguko la Kiuchumi Sudan Ni Matokeo ya Sera Inayoagizwa na Benki ya Dunia
Habari:
Benki ya Dunia ilisema uchumi wa Sudan umepungua kwa asilimia 13.5 zaidi mwaka wa 2024, baada ya kupungua kwa karibu theluthi katika mwaka uliopita, huku umaskini uliokithiri unatarajiwa kuathiri 71% ya watu kutokana na kuendelea kwa mzozo. (Sudan Tribune, Juni 10, 2025)
Maoni:
Hii ni Benki ya Dunia ambayo inazitaka nchi kufuata sera zake za kibepari ambazo zinazifanya nchi kuwa watumwa, na kupora utajiri wao na kuzigharikisha katika umaskini, licha ya utajiri wao wa rasilimali na utajiri, inaamuru kufuata maangamizi, kisha inakuja kuhubiri na kuongoza, mfano wake ni kama shetani alipomwambia mwanadamu kana, na alipokana alisema mimi sina hatia na wewe!
Vita pekee siyo sababu ya anguko la uchumi kwa sababu tayari umeanguka kutokana na kufuata sera za Benki ya Dunia, na maelekezo ya Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) la kibepari ambalo linaitwa mageuzi ya kiuchumi, na kwa hakika ni anguko la kiuchumi; kwani njaa iliyoandaliwa kwa ajili ya watu wa Sudan ilianza tangu maelekezo ya kwanza, ambapo ilibadilisha mradi mkubwa zaidi wa kilimo wenye usimamizi mmoja duniani, mradi wa Al-Jazira, ilibadilisha kuwa historia, kisha maelekezo yakaendelea hadi Sudan ilipovuliwa mahitaji ya chini kabisa ya maisha bora ili kuwaridhisha mataifa ya kikoloni, na taasisi za fedha za kimataifa, na serikali zinazofuatana ambazo haziwezi kujitegemea katika uamuzi wao licha ya utajiri wa Sudan katika rasilimali za dhahiri na za ndani.
Mfumuko wa bei ambao umefikia 170% na anguko la pauni ya Sudan si matokeo ya udhaifu wa kiuchumi halisi bali ni maamuzi ya kisiasa yanayoagizwa na Shirika la Fedha la Kimataifa, ikiwa ni pamoja na kuachia thamani ya ubadilishaji, kuondoa ruzuku ya mafuta, kuongeza kodi na ada, na ubinafsishaji wa kile kilichosalia cha sekta ya umma ikiwa kuna kilichosalia cha kubinafsishwa. Na haya yote yanaenda katika kupunguza nakisi ya bajeti kwa gharama ya maskini ambao hawana mtu wa kuwasaidia na kusimama nao baada ya serikali kuwaacha hivyo wameathiriwa na umaskini na njaa kwa ajili ya ndoto ya kuongeza mapato ya kulipa madeni, na siyo kwa ajili ya kumtumikia mtu ambaye amekuwa mwathirika wa kumridhisha Magharibi ya kibepari.
Kwa upande mwingine, Uislamu ulisimamisha mfumo wa kiuchumi ambao ulitimiza mahitaji ya kila mtu aliyeishi chini ya kivuli cha dola yake, na msingi wa mfumo ni kuwahudumia watu mmoja mmoja, kwani Uislamu unaharamisha riba kabisa, na ndiyo msingi wa mfumo wa kibenki wa kimataifa ambao umezifanya nchi ambazo si kamili leo kuzama katika madeni, na kuwa chini ya utawala wa Shirika la Fedha la Kimataifa na Benki ya Dunia zikitekeleza maangamizi yake na mitego yake ya kiuchumi, na pia Uislamu ulifanya mafuta, gesi na madini kuwa mali ya umma, siyo mali ya dola, au makampuni binafsi, Mtume ﷺ alisema: «Watu wanashirikiana katika vitu vitatu: maji, malisho, na moto». Kwa hiyo, kuuza mafuta na gesi na kupata faida kutokana nazo pamoja na kuachia bei zake na kubinafsisha rasilimali ni uvamizi wa mali ya umma na uhalifu dhidi yake na si mageuzi ya kiuchumi kama wanavyodai. Ama mfumuko wa bei unaotokana na kupanda kwa bei za bidhaa, au kutokana na kuchapisha sarafu bila akiba na kuwa sarafu ni karatasi isiyo na thamani basi hiyo ni janga jingine, na pia inapingana na hukumu za Kiislamu na ni wizi wa juhudi za watu na akiba zao, huku Uislamu ukifanya fedha kuwa dhahabu na fedha kwa sababu zina thamani ya asili.
Hii ni tone katika bahari ya mfumo wa kiuchumi katika Uislamu ambao hali za watu hazitabadilika isipokuwa kwa kuutekeleza kikamilifu na kwa ukamilifu pamoja na mifumo mingine ya Kiislamu katika Dola ya Khilafa Rashidah ya pili juu ya njia ya Utume ambayo wakati wake umekaribia.
Imeandikwa kwa ajili ya Radio ya Ofisi ya Habari Kuu ya Hizb ut-Tahrir
Ghada Abdul Jabbar (Um Awaab) - Wilaya ya Sudan