Kuanza kwa Majadiliano ya Sharm El-Sheikh
Habari:
Imepangwa kuwa leo Jumatatu, majadiliano ya mchakato wa kubadilishana wafungwa yataanza kulingana na pendekezo la Rais wa Marekani Donald Trump huko Sharm El-Sheikh, huku harakati ya Hamas ikitangaza kuwasili kwa ujumbe wake nchini Misri, huku habari kutoka kwa Wayahudi zikieleza kutokuwepo kwa mkuu wa ujumbe wao na wajumbe wa Marekani Steve Witkoff na Jared Kushner katika mazungumzo ya leo ili wajiunge kesho ikiwa kutakuwa na maendeleo.
Maoni:
Je, inawezekana kwamba nchi kubwa, zikiongozwa na Marekani, zinasonga mbele kwa msukumo wa huruma na rehema kuelekea kile kinachotokea kwa watu wetu huko Gaza? Na je, maamuzi na mikataba yao itakuwa na suluhisho la kichawi kwa matatizo yetu sisi Waislamu?
Ukweli unaonyesha kuwa nchi hizi haziendeshwi na hisia, bali na maslahi na sera za kimkakati. Ikiwa huruma ndiyo ingekuwa msukumo wa kweli, nchi hizo zisingeliunga mkono utawala wa Wayahudi tangu kuanzishwa kwake, wala kuzipatia silaha na vifaa, huku zikijua kuwa vifaa hivi vinatumika kuua na kuwafukuza Waislamu. Je, baada ya historia hii ndefu ya msaada na usaidizi, inawezekana kuamini kwamba nchi hizi kweli zinataka kusimamisha vita dhidi ya umma wa Kiislamu?
Maamuzi na mikutano yao si chochote ila njia za kulinda ushawishi na maslahi yao, si kuokoa wanaodhulumiwa au kuunga mkono wanyonge. Na kile wanachotangaza kuhusu nia ya kusitisha mapigano huko Gaza si chochote ila aina ya udanganyifu wa kisiasa, unaokusudiwa kuonyesha huruma hadharani, huku wakificha uharibifu na maangamizi kwa umma.
Kukimbilia kwa watawala wa Kiislamu nyuma ya mipango ya viongozi wa Magharibi, wakiongozwa na Trump, ni ushahidi wazi kwamba mipango hii si chochote ila njama zilizopangwa dhidi ya Uislamu na Waislamu, na inalenga kuondoa kila mradi wa Kiislamu, na kuufanya Uislamu kuwa dini iliyofungwa ndani ya misikiti ambayo haivuki kuta zake.
Watawala hawa, tangu kafiri mkoloni alipowaweka juu ya shingo za umma, hawajali chochote ila kuwafuatilia waaminifu kutoka kwa watoto wa Waislamu, ambao wanatafuta ukombozi kutoka kwa mifumo ya utegemezi na kujenga utawala unaozingatia sheria na haki ya Mungu.
Kinachotokea leo cha mikutano na makongamano yanayofanyika chini ya usimamizi wa mawakala wa Magharibi, kama vile mikutano ya Sharm El-Sheikh inayoongozwa na utawala wa Sisi, si chochote ila maandalizi ya utekelezaji wa maamuzi yanayokusudiwa kuondoa Uislamu kutoka kwa maisha ya umma, na kuimarisha mifumo ya ukafiri na sheria zake katika nchi za Waislamu chini ya jina la watoto wa Ibrahimu na kuanzisha uhusiano wa kawaida na utawala wa Wayahudi. Hata inaonekana kama mfano wa ustaarabu unaotarajiwa! Lakini ukweli ni kwamba uhusiano huu wa kawaida si chochote ila daraja kuelekea kudhoofisha na kuuvunja umma.
Makongamano haya, ingawa kauli mbiu za huruma na kusimamisha vita zinatolewa, lakini ndani yake kuna maana zote za udanganyifu na maangamizi. Na kile kinachosemwa kuhusu kusitisha mapigano huko Gaza ni kama kumlisha mnyama anayechinjwa kabla ya kupelekwa machinjioni; heshima ya kimuundo inayotangulia uharibifu wa kweli.
Mwenyezi Mungu amesema: ﴿NA LIKUKUMBENI UBAYA WOWOTE, WATAUFURAHIA. NA MKISUBIRI NA MKAJICHUNGA, HAKIWA DHURU HILA YAO KITU. HAKIKA MWENYEZI MUNGU YU MWENYE KUYAZUNGUKA WAYATENDAYO﴾, basi subirini enyi watu wa Gaza, na imara enyi umma wa Kiislamu, kwani hila haijalishi itazidi vipi, haitashinda ahadi ya Mungu, na dhuluma haijalishi itachukua muda gani, hatima yake ni kutoweka. Na kwa Mungu ndiko tunakolalamika, naye ndiye msaidizi bora.
Imeandikwa kwa ajili ya redio ya Ofisi ya Habari Kuu ya Hizb ut-Tahrir
Abdul-Azim Al-Hashlamoun