Ulaya Inaendelea Kuunga Mkono Mauaji ya Kimbari huko Gaza
(Imetafsiriwa)
Habari:
Mauaji ya kimbari yanaendelea kwa miaka miwili. Hata hivyo, Umoja wa Ulaya bado ni mshirika mkuu wa kibiashara wa taasisi ya Kiyahudi, na biashara kati yao inafikia Euro trilioni 42. Licha ya kauli mbiu tupu kuhusu kuitambua dola la Palestina, Ulaya inaendelea kusafirisha silaha kwa Wayahudi. Habari zilizovuja ambazo gazeti la Information la Denmark lilipata zinafunua kwamba Agosti iliyopita, serikali ya Denmark ilituma vipengele vya silaha kwa ndege zilizotumiwa kuua watoto huko Gaza. Pia, Mahakama Kuu ya Uholanzi iliamua kutoiingilia usafirishaji wa serikali ya Uholanzi wa vipuri vya ndege za kivita za F-35 kwa Wayahudi.
Maoni:
Kinyago ambacho Magharibi ilitumia kutawala ulimwengu kimefunuliwa - kinyago cha kile kinachoitwa haki za binadamu na wazo kwamba sisi ni wema na wastaarabu wakati wengine ni waovu - kabisa. Magharibi imefanya juhudi kubwa za kudumisha koloni lake la kisasa la walowezi huko Palestina, ikitambua kwamba kuanguka kwake kutakuwa mwisho wa utawala wake juu ya nchi za Kiislamu. Taasisi ya Kiyahudi ni ishara ya ushindi wa Magharibi dhidi ya Uislamu, na ikiwa taasisi hii haramu itaanguka, itakuwa ishara kwamba nchi za Kiislamu zinaelekea kwenye ufufuo.
Hii itatoa umma wa Kiislamu ujasiri usioelezeka, na kuusukuma mbele kuelekea ushindi wa mwisho dhidi ya ukoloni wa Magharibi.
Kwa hivyo, hakuna bei ambayo Magharibi haiko tayari kulipa ili kuweka taasisi ya Kiyahudi iendelee kuwepo. Wametoa pesa na kile kilichosalia cha uaminifu wao mdogo ili kuihifadhi.
Lakini hii haitadumu kwa muda mrefu. Ulimwengu wote umetambua kwamba Magharibi ni mnyama tu, na Waislamu wameanza kuchukua hatua kwa haki dhidi ya tawala za wasaliti na za kidhalimu.
Umma uko hai, na ni suala la muda tu kabla ya kurejesha heshima ya ulimwengu na kuthibitisha kwamba uongozi unawezekana bila unyanyasaji, umwagaji damu au ukoloni, lakini kwa mawazo na maadili ya Uislamu.
Imeandikwa na Idhaa ya Afisi ya Habari Kuu ya Hizb ut-Tahrir
Tim Abu Laban