Uzbekistan Yaidhinisha Sheria ya Kuadhibu Ufundishaji wa Dini ya Kiislamu kwa Watoto
(Imetafsiriwa)
Habari:
Baraza la Seneti la Uzbek limeidhinisha sheria inayotoa adhabu ya jinai kwa kufundisha dini kwa watoto wadogo bila ruhusa au elimu inayofaa. Adhabu ya matendo haya sasa inaweza kuwa kifungo cha hadi miaka mitatu.
Baraza la Seneti katika Baraza Kuu la Uzbekistan liliidhinisha, katika kikao kilichofanyika Juni 25, sheria inayoongeza uwajibikaji kwa elimu haramu ya dini kwa watoto wadogo. Hati hiyo imewasilishwa kwa rais kwa ukaguzi.
Mkuu wa Kamati ya Sayansi, Elimu na Huduma za Afya katika Baraza la Seneti, Bahrom Abdullayev, alisisitiza kwamba serikali inafanya kazi ya kimfumo ili kuhakikisha ulinzi wa kuaminika wa haki na maslahi halali ya watoto, na kuunda mazingira yanayofaa kwa ukuaji wao wa kina. Alisisitiza "umuhimu maalum wa kuunda ufahamu na utamaduni wa kisheria kwa watoto, pamoja na kuunda hali zote muhimu kwa wao kupata elimu nzuri, ambayo inachangia ukuaji wao wa kimwili, kiakili, kiroho na kimaadili".
Kulingana na yeye, wakati huo huo katika miaka ya hivi karibuni, jamhuri imeshuhudia ongezeko la visa vya elimu haramu ya dini kwa watoto wadogo, na katika suala hili, marekebisho yanafanywa kwa Kifungu cha 229-2 cha Sheria ya Jinai (ukiukaji wa taratibu za kufundisha mafundisho ya kidini).
Maoni:
Ikumbukwe kwamba, tofauti na maandishi ya awali, ambapo kitendo kama hicho kiliadhibiwa na faini ya kiutawala au kifungo cha hadi siku 15, sasa kinakabiliwa na dhima ya jinai mara moja ikiwa mtu aliyefunzwa ni mdogo.
Idhini ya sheria hii inaendeleza mbinu ya Mirziyoyev ya kuimarisha udhibiti wa mwamko wa Kiislamu, na kurejesha nchi, kimsingi, kwa mazoea ya enzi ya Rais wa zamani Karimov, anayejulikana kwa sifa yake mbaya.
Kama inavyojulikana, Huduma ya Usalama wa Kitaifa mara kwa mara hufanya uvamizi katika kile kinachoitwa "hujurat", ambayo ni shule za kidini za siri za kibinafsi ambazo zilionekana Uzbekistan wakati wa enzi ya Soviet.
Ikumbukwe kwamba sheria kama hiyo ilitolewa kwa mara ya kwanza mnamo 1998. Sheria ya "Uhuru wa Dhamiri na Mashirika ya Kidini" iliweka vikwazo vikali kwa shughuli za kidini. Hasa, haikuruhusiwa kufundisha dini isipokuwa katika taasisi za elimu ya kidini zilizosajiliwa rasmi, na baada ya kupata elimu maalum. Katika mwaka huo huo, Kifungu cha 229-2 cha Sheria ya Jinai ya Uzbekistan kiliingizwa, ambayo ilitoa dhima ya jinai kwa "kufundisha dini kinyume na taratibu za kisheria".
Marufuku hii na kifungu cha jinai vilitumika mara kwa mara katika muongo wa kwanza wa karne ya 21 na mwanzoni mwa muongo wa pili, ambayo ilizua ukosoaji wa watetezi wa haki za binadamu, kwani ilizuia uhamishaji wa maarifa ya kidini hata ndani ya familia, ambayo ni kwamba watu walishtakiwa hata kwa kuwafundisha watoto wao Uislamu.
Wakati Mirziyoyev alipoingia madarakani, mazoea haya yalisitishwa kwa muda, lakini sasa yamerejeshwa.
Imeandikwa kwa ajili ya redio ya Ofisi Kuu ya Habari ya Hizb ut-Tahrir
Muhammad Mansour