Pakistan Inatekeleza Tena Mradi wa Kimarekani Dhidi ya Afghanistan!
(Imetafsiriwa)
Habari:
Mashambulizi ya anga yaliyofanywa na ndege zisizo na rubani za jeshi la Pakistan katika mikoa ya Khost na Nangarhar nchini Afghanistan yalisababisha vifo vya watoto watatu kutoka familia moja na kujeruhi wengine watano, wakiwemo wanawake na watoto.
Maoni:
Matukio ya hivi karibuni katika eneo hilo yanaonyesha kuwa Pakistan imeanzisha tena mradi mpya chini ya uongozi wa Marekani kuhusu Afghanistan. Mradi huu, ambao ni muendelezo wa sera ya Washington iliyoimarika ya kukandamiza harakati zozote za Kiislamu huru katika eneo hilo, sasa unatekelezwa kwa nguvu na uratibu mkubwa zaidi. Hatua za hivi karibuni za kijeshi, kidiplomasia na kiintelijensia za Pakistan zinaonyesha kuwa imechukua jukumu la chombo cha shinikizo kwa Afghanistan.
Ziara za hivi karibuni za kamanda wa jeshi la Pakistan, Asim Munir, kwenda Amerika, pamoja na mikutano ya ngazi ya juu kati ya maafisa wa Marekani na Pakistan huko Islamabad - sanjari na ombi la Washington la kurejesha vifaa vya kijeshi vilivyosalia kutoka Afghanistan - ni sehemu ya mradi huu. Muda mfupi baada ya mikutano hii, jeshi la Pakistan lilifanya mashambulizi ya anga katika maeneo ya mpakani ya Afghanistan, ambayo yanaonyesha jinsi makubaliano ya siri yanavyobadilika haraka kuwa operesheni. Mashambulizi dhidi ya maeneo ya Harakati ya Taliban Pakistan karibu na mpaka wa Afghanistan yanaimarisha uwezekano wa ushirikiano wa kijasusi wa Marekani. Wakati huo huo, Marekani inaweza kutoa motisha mpya za kifedha kwa Pakistan kwa kuwezesha tena sehemu ya Mfuko wa Msaada wa Muungano kwa ajili ya operesheni za kupambana na ugaidi. Wakati huo huo, maafisa wa Pakistan, ikiwa ni pamoja na kamanda wa jeshi, wanasisitiza jukumu la Pakistan katika kupambana na Uislamu, wakitaka kuwasilisha picha nzuri ya ushirikiano huu mpya kwa Washington.
Lengo kuu la mradi huu ni wazi: kuishinikiza Taliban, kuzuia harakati za Kiislamu katika eneo hilo, na kusukuma mwelekeo wa kijeshi wa Pakistan kuelekea magharibi ili kuwahakikishia India, na kuzuia kuibuka kwa mabadiliko yoyote makubwa ambayo yanaweza kuleta changamoto kwa mfumo wa kimataifa unaotawaliwa na nchi za magharibi. Tena, chini ya kauli mbiu ya kulinda maslahi ya kitaifa, Pakistan imejiunga na mradi ambao utachochea tu ukosefu wa utulivu zaidi, kuongeza muda wa vita vya uwakilishi, na kudhoofisha Umma wa Kiislamu.
Ikiwa mwelekeo huu utaendelea, harakati za Kiislamu katika eneo hilo zitakabiliwa na vitisho si kutoka kwa adui wa kigeni, bali kutoka kwa jirani kibaraka. Njia pekee ya kukabiliana na hali hii ni kupitia mabadiliko ya kisiasa na kijiografia katika eneo hilo kwa kuanzisha Khilafah Rashidah badala ya kushikilia kile kinachoitwa "sera za kitaifa" za Pakistan.
Imeandikwa kwa ajili ya Idhaa ya Afisi ya Habari Kuu ya Hizb ut Tahrir
Yusuf Arsalan
Mwanachama wa Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilaya ya Afghanistan