Kati ya Utawala wa Udhalili na Imamu Mlinzi
Habari:
Katika mahojiano maalum yaliyofanywa na kituo cha Al-Hadath siku ya Ijumaa, 2025/6/6 na Waziri wa Ulinzi wa Iraq Thabet al-Abbasi, alisisitiza umuhimu wa kuwepo kwa majeshi ya Marekani nchini Syria kutokana na kambi ya Al-Hawl, ambayo inajumuisha idadi kubwa ya shirika la Dola.
Maoni:
Bado watawala wasaliti na viongozi wajinga wanaomba suluhu kutoka kwa maadui zao na wanaomba mbwa mwitu kulinda mifugo yao! Hali hii inaonyesha udhaifu wa mifumo hii vibaraka, Amerika hii ambayo inasimama kama tegemeo lenye nguvu zaidi kwa taasisi ya Kiyahudi katika uhalifu wake huko Gaza na kuua wasio na hatia na kuzuia chakula kuwafikia, bali inawaua wanapotafuta tonge la chakula, je, inampata mtu yeyote akilini kwamba inamjali Muislamu yeyote bila kujali utaifa wake?!
Ombi hili, na kutoka kwa kiongozi wa kijeshi, linaonyesha tu usaliti au ujinga mkubwa, ni tendo gani la kibinadamu ambalo Amerika imefanya ambalo limewafadhili waliodhulumiwa?!
Je, ulimwengu wote haujaungua na moto wa ufisadi na uhalifu wake?
Je, si yeye anayeunga mkono taasisi ya Kiyahudi katika uhalifu wake wote huko Palestina, Syria na Lebanon...?
Je, si yeye aliyeharibu Iraq?
Je, si yeye anayeunga mkono wafisadi miongoni mwa wasaliti wa umma?
Na nani mwingine ila yeye anatangaza waziwazi kwamba anataka utajiri wa Waislamu kwa nguvu na bila haya?!
Wallahi, ni aibu na huzuni kwamba watawala wa Waislamu wana uoga huu na unyenyekevu huu, bali na usaliti huu.
Ukweli ni kwamba Amerika inainua fimbo nene, inayowakilishwa na shirika la Dola, mbele ya serikali ya Iraq ikiwa haitatii maagizo yake kuhusu wanamgambo wenye silaha wanaoungwa mkono na Iran, ili taarifa hii ije kuwashinikiza wanamgambo hao, na kumsihi Amerika kuipa serikali ya Iraq nafasi ya kutatua faili hili.
Ndio, Enyi Umma wa kheri na uongofu, hii ndio hali ya Waislamu baada ya kutokuwepo kwa dola ya Khilafa, dola ya utukufu; mataifa yametukimbilia kutoka kila upande, yakila miili yetu, na kupora utajiri wetu, na hakuna Imamu mlinzi wa kututetea, tunapigana nyuma yake na kujikinga kwake.
Amkeni enyi Waislamu kutoka usingizini mwenu na inukeni kutoka katika malazi yenu na simamisheni Khilafa iliyoongoka kwa mfumo wa Utume, na mumpatie Bay'ah Imamu mlinzi ambaye mnapigana nyuma yake na mnakijikinga kwake.
Imeandikwa kwa ajili ya Radio ya Ofisi Kuu ya Habari ya Hizb ut-Tahrir
Ahmed Al-Ta'i - Jimbo la Iraq