Kati ya Mchakato wa Uondoaji wa Vikosi vya Syria kutoka Al-Suwaida
Na Mchakato wa Miaka 48, 56 na 67 huko Palestina
Habari:
Mashahidi wa eneo hilo kutoka kwa watu wa kabila la Bedouin huko Al-Suwaida walisema kwamba vikundi vyenye silaha vilifanya ukiukaji, pamoja na mauaji na uhamishaji dhidi ya raia kutoka kwa makabila hayo katika idadi ya vijiji vya mkoa huo.
Hii inakuja saa chache baada ya uondoaji wa vikosi vya Wizara ya Ulinzi ya serikali ya Syria, ikifuatiwa na ukiukaji ambao mtandao wa Al-Rased unaofanya kazi katika mkoa wa Al-Suwaida uliandika idadi yao, pamoja na visa vya kuvamia nyumba, kufyatua risasi, na kuua raia. (Enab Baladi)
Maoni:
Hali hiyo hiyo inakumbukwa, wakati majeshi ya Kiarabu yalisonga mbele kusaidia watu wa Palestina ambao walikuwa wakipinga magenge ya Kizayuni ya Haganah na Irgun, na walikuwa wakiwashinda mara kwa mara hadi wakawalazimisha katika eneo la pwani. Majeshi haya yalikuja na lengo lililotangazwa la kuwasaidia watu wetu huko Palestina, na viongozi wao walikutana na viongozi wa waasi, na ombi lao lilikuwa kwamba waasi wakabidhi silaha zao na kujiondoa kutoka eneo la vita na kuacha kazi kwao. Waliingia katika vijiji na kuwaomba wakaazi kuondoka nyumbani kwao kwa sababu kutakuwa na vita kali katika vijiji hivi, mabondeni na tambarare ili kulinda maisha yao na damu yao. Waasi na wenyeji walijibu na kuanza uhamiaji mkubwa na kuhamisha makazi yao, vijiji, ardhi na mashamba, na wachache walibaki ambao walikataa kuacha nyumba zao na ardhi zao.
Lakini mshangao ulikuwa wakati makabiliano yalipoanza kati yao na magenge ya Kizayuni, ambapo majeshi haya yalijiondoa, yakiacha vijiji, mashamba na watu bila silaha au mlinzi wa kuwalinda! Wazayuni walianza kuchinja, kuchoma moto na kuharibu kila kitu.
Kile kilichoonekana ni picha ndogo ya hali ile ile iliyotokea katika miaka ya 48, 56 na 67... Kitu kilichopangwa na kutayarishwa kikamilifu na matokeo yake yamehesabiwa. Vikosi vya kijeshi na usalama vya Syria vilisonga mbele huko Al-Suwaida na kuendelea kusonga mbele, na mara tu joto la vita lilipoanza kuongezeka, amri za juu zilitolewa kwa uondoaji wa vikosi vya kijeshi na usalama kutoka Al-Suwaida, na vikosi hivi viliachwa chini ya "huruma" ya Wadrusi, ambao waliendelea kuwaua na raia kutoka kwa makabila; kunyongwa hadharani kwa wanawake, wanaume na watoto bila huruma, bila kujali mzee au mdogo, au mwanamke au mtoto mchanga, au mzee, na kuandikwa na video na upigaji picha wa moja kwa moja.
Je, vipi nia ya vikosi hivyo katika miaka ya 48, 56 na 67 na nia ya viongozi wa kijeshi na kisiasa mwaka 2025 huko Al-Suwaida ilikutana, wakati adui ni mmoja, mbinu yake haijabadilika, na mwelekeo wake ni thabiti kwamba haachi chochote, haheshimu Waislamu au ahadi?
Laana ya Mungu iwe juu ya wasaliti vibaraka wanaouza dini yao na damu ya taifa kwa faida ya muda mfupi ya ulimwengu.
﴿WAO NDIO ADUI, WAANGALIENI. ALLAH AWALAANI. WANAGEUZWAJE!﴾
Imeandikwa na Idhaa ya Afisi ya Habari Kuu ya Hizb ut-Tahrir
Salim Abu Subaitan