Kuunganisha QSD katika taasisi za dola ya Syria.. Kosa la kisiasa lenye matokeo hatari
Habari:
Waziri wa Mambo ya Nje wa Syria, Asaad al-Shibani, alisema Jumamosi 2025/10/18, kwamba kutokuwepo kwa vikosi vya Syria vya Kidemokrasia ndani ya taasisi za dola kunazidisha pengo kati yao na dola. Aliongeza katika mahojiano na Al-Ikhbariya ya Syria kwamba Rais Ahmed al-Shara anataka vikosi vya Syria vya Kidemokrasia viwe sehemu muhimu ya mustakabali wa Syria.
Maoni:
Kukubali kwa serikali ya Syria kujiunga kwa vikosi vya Syria vya Kidemokrasia, vinavyojulikana kwa kifupi kama "QSD", na muundo wa dola ni kosa kubwa la kisiasa, ambalo halionyeshi akili ya mtu wa dola, kwani wanamgambo hawa wa kujitenga wenye mawazo ya kikafiri yanayopingana na dini hawawakilishi utamaduni wa watu wa Syria, na sio sehemu ya mapinduzi ya Syria, wala hawaelezei mapambano ya watu wa Syria katika juhudi zao za kukombolewa kutoka kwa minyororo ya utawala uliopita wa Assad, lakini kinyume na hayo, QSD ilikuwa msaada kwa utawala wa wahalifu, kwani iliwapa silaha tangu mwaka 2012 kupambana na mapinduzi, na kuzuia udhibiti wa waasi juu ya maeneo ya mashariki mwa Syria, na wapiganaji wengi waaminifu waliuawa mikononi mwao wakati wa miaka ya mapinduzi, na hata baada ya kuanguka kwa Assad, na la mwisho ni tukio la vitongoji vya Ashrafiya na Sheikh Maqsoud mnamo 2025/10/7, ambapo wanachama kadhaa wa usalama wa ndani wa Syria waliuawa na kujeruhiwa katika shambulio la wanamgambo kwenye vizuizi vya serikali katika eneo hilo.
Kushughulika na QSD kama mshirika anayewezekana katika utawala wa nchi ni kuhalalisha vitendo vyake vya uhalifu dhidi ya watu katika maeneo yake ya ushawishi huko Hasakah, Raqqa na Deir Ezzor, kutoka kwa kukamatwa kwa uonevu, utekaji nyara wa wasichana kuwasajili kijeshi, ukiritimba wa utajiri, na kulazimisha mawazo ya kujitenga na Umaksi katika elimu, ambazo ni vitendo ambavyo mashirika ya haki za binadamu huandika mara kwa mara. Na mtu anayetazama vitendo hivi anaviona havina tofauti na vitendo vya utawala uliopita wa Assad, na kutoka hapa waasi wanaona QSD na utawala kama pande mbili za sarafu moja. Kwa hivyo, kuunganisha wanamgambo hawa katika taasisi za dola ni sawa na kukubali kuunganisha Kitengo cha Nne na Ujasusi wa Anga (ambao ni wa genge la Assad hapo awali) katika taasisi za jeshi na usalama.
Hakuna shaka kwamba serikali ya Syria inashughulika na QSD kwa njia ya kujumuisha na kukubalika kutokana na hamu ya Amerika, kwa sababu QSD inaitumikia, na ni mshirika wake katika kupambana na Uislamu, kwa hivyo inataka kuwatuza kwa kuifanya nguvu ya asili katika chombo cha utawala. Lakini kile ambacho watawala wa Syria wanapaswa kutambua ni kwamba Amerika kwa hatua hii hailengi kufikia utulivu nchini Syria na kusimamisha vita kama inavyodai, lakini inataka kudhoofisha dola kwa kukusanya vitalu vinavyopingana katika mamlaka, na kwa kufanya hivyo inahakikisha kuwa hakuna mamlaka yenye nguvu itakayoibuka nchini Syria, na inaweza wakati wowote inapotaka kuhamasisha QSD kujiondoa serikalini, na kuunda mivutano na vita ambavyo vinavunja mgongo wa nchi na kuwachosha watu wake.
Chaguo pekee katika kushughulika na QSD ni chaguo la kijeshi, kwa hivyo serikali lazima iondoe wanamgambo hawa kwa nguvu, na iokoe watu wa mashariki mwa Syria kutoka kwa maovu yao, bila kujali hasira au kuridhika kwa Amerika, kwani hairuhusiwi kuwa na maoni, ushawishi au jukumu lolote nchini Syria, kwani ni nchi ambayo inachukuliwa kuwa rejeleo katika uhalifu, na mfano katika uharibifu, na msaada wake kwa Bashar ulikuwa sababu kuu za kuendelea kwake hadi 2024, kwa hivyo watawala wa Syria wanapaswa kuwapa mgongo, na wakumbuke vizuri kile Rais wa zamani wa Misri Hosni Mubarak alisema siku moja "Anayejifunika kwa Amerika yuko uchi".
Imeandikwa kwa Radio ya Afisi ya Habari Kuu ya Hizb ut-Tahrir
Ahmed Saad