Masomo Kutoka kwa Kushindwa kwa Demokrasia Kubwa Zaidi Duniani katika Haki za Wanawake Waislamu
(Imetafsiriwa)
Habari:
Gazeti la Indian Express lilichapisha makala yenye kichwa "Wakati Kutokuwepo Kunazungumza Zaidi ya Uwepo: Wanawake Waislamu na Bunge la India". Makala inazungumzia upungufu mkubwa wa uwakilishi wa wanawake Waislamu katika Bunge. Tangu muhula wa kwanza wa Lok Sabha (Bunge la Kidemokrasia la India) mwaka 1952, kumekuwa na wanawake Waislamu kumi na nane tu walio hai katika mabaraza. Upungufu huu wa uwakilishi umeandikwa katika kitabu kipya kilichoandikwa na mwandishi wa habari Rashid Kidwai na mtaalamu wa sayansi ya siasa Ambar Kumar Ghosh, kiitwacho "Waliopotea kutoka Bungeni: Wanawake Waislamu katika Lok Sabha", kilichochapishwa na Juggernaut (2025). Waandishi wanasisitiza kutambua kwao jinsi uwakilishi huu mara nyingi ni wa ishara tu. Kwa vyama vingi vya siasa, kumteua mwanamke Mwislamu kulikuwa ishara tu badala ya kuwa na athari na ushawishi halisi. Miongoni mwa mada muhimu zinazochunguzwa na kitabu hicho ni uhusiano wa wasiwasi kati ya kuonekana na mamlaka. Mbunge Mwislamu anaweza kuvutia umakini wa vyombo vya habari, lakini linapokuja suala la kufanya maamuzi halisi, kuchagua wagombea, kuweka vipaumbele vya sera, na nafasi za mawaziri, wanawake Waislamu mara nyingi huwekwa pembezoni waziwazi, na waandishi wanaeleza kuwa "uwakilishi wa kidemokrasia" haumaanishi uwezeshaji.
Maoni:
Sisi wanawake Waislamu hatupaswi kushangaa tunaposhuhudia mwisho wa enzi ambayo uzoefu wa nadharia ya kisiasa ya kiliberali unahitaji ushahidi wa sumu yake. Haiwezekani tena kupata tiba iliyopotea kwa muda mrefu ya uwezeshaji katika shimo jeusi la demokrasia. Tumeona udanganyifu wa "ujumuishaji" kwa jinsi ulivyo, udanganyifu wa ahadi za uongo na matamshi ya Kiislamu yanayopotosha. Kufikia madaraka daima humaanisha kuwatumikia mabwana zako wa kilimwengu na kuacha uhusiano wako na Mwenyezi Mungu.
Wanawake wanaunga mkono ukimya kuhusu unyanyasaji na mauaji ya kimataifa na ya ndani ya wanawake Waislamu ambao wanaishi kwa hofu ya kueleza utambulisho wao na uaminifu wao kwa Mwenyezi Mungu.
Sisi wanawake Waislamu hatupaswi kamwe kusahau kwamba tuna uwezeshaji wa kweli kutoka kwa Mwenyezi Mungu pekee, na kwamba sauti zetu, usalama wetu, na heshima yetu daima zimehifadhiwa chini ya kivuli cha Khilafa. Hatujawahi kuhitaji vuguvugu la haki za wanawake, na tulikuwa tunawalinda wanawake wasio Waislamu kwa maadili yetu matukufu. Haki za kiuchumi na kijamii ni takatifu na ziko wazi katika Surah An-Nisa; ﴿Na nusu ya walichoacha wake zenu ni yenu ikiwa hawana mtoto. Na ikiwa wana mtoto basi ni robo ya kile walichoacha, baada ya wasia waliousia au deni. Nao wana robo ya mliyoacha ikiwa hamna mtoto. Na ikiwa mna mtoto basi wao wana thumni ya mliyoacha, baada ya wasia mliousia au deni. Na ikiwa mwanamume au mwanamke anarithiwa hali ya kuwa hana wazazi wala mtoto, naye ana ndugu mwanamume au ndugu mwanamke, basi kila mmoja katika hao ana sudusi. Na ikiwa wao ni zaidi ya hao, basi wanashirikiana theluthi, baada ya wasia uliousiwa au deni lisilo dhuru. Huu ni wasia kutoka kwa Mwenyezi Mungu. Na Mwenyezi Mungu ni Mjuzi, Mpole.﴾.
Tukizingatia pekee kurudisha Uislamu katika maisha ya kisiasa, hatutabaki tumefarakana katika korido za ajenda ya kilimwengu ambayo inataka tu kumfanya mwanamke Mwislamu wa kweli asionekane na ashindwe.
Imeandikwa kwa Idhaa ya Afisi ya Habari Kuu ya Hizb ut Tahrir
Umrana Muhammad
Mjumbe wa Afisi ya Habari Kuu ya Hizb ut Tahrir