Palestina Inasubiri Ukombozi na Siyo Kusimamisha Uchokozi na Kuondoa Mzingiro Pekee!
Habari:
Rais wa Yemen Al-Mashat akihutubia watu wetu huko Gaza: Msimamo ni ule ule na utaendelea hadi uchokozi usimamishwe na mzingiro uondolewe kwenu, haijalishi ukubwa wa changamoto.
Maoni:
Hotuba ya Mahdi Al-Mashat, Mkuu wa Baraza Kuu la Kisiasa la mamlaka ya Houthi, kwa watu wa Gaza, ilikuja ndani ya hotuba aliyoitoa kutoa rambirambi kwa familia za wale waliouawa na mashambulizi ya Kiyahudi katika mji mkuu Sana'a siku ya Alhamisi 2025/8/28, ambayo ilimuua Waziri Mkuu wa Sana'a Ahmed Ghaleb Al-Rahwi pamoja na idadi ya mawaziri wa serikali yake.
Vitendo vya Wahouthi kuhusiana na Palestina ni sehemu ya sera ya upotezaji ambayo wanaitumia kwa wafuasi wao nchini Yemen katika mazingira ya kukosa uangalizi wa masuala yao, na kuwafanya watu wa kawaida waamini kuwa wako katika jihad na kuwasaidia watu wa Gaza, huku uongozi wao ukijua kwamba kurusha kombora au ndege isiyo na rubani, na hotuba ya kiongozi wao kila wiki, na mkutano wao katika uwanja wa Sab'in kila Ijumaa alasiri, haitasimamisha uchokozi wala kuondoa mzingiro, sembuse kuikomboa Palestina kutoka kwa Wayahudi na kuing'oa kutoka mizizi yake.
Suala la Palestina ni suala la Waislamu wote, na sio suala la watawala wao ambao wameiuza kwa bei rahisi wakitumia mbinu zao za ujanja na chafu kama vile kuwadanganya watu mara moja, kutumia nguvu mara nyingine, na kuanzisha uhusiano wa kawaida mwishowe, wakikimbilia radhi za Magharibi na hawatapata radhi zao, kwa mujibu wa kauli ya ukweli Mtukufu na Aliye juu: ﴿Na hawatakubali Mayahudi wala Wakristo mpaka uifuate mila yao. Sema: Hakika uongofu wa Mwenyezi Mungu ndio uongofu. Na kama utafuata matamanio yao baada ya kukujia ujuzi, huna mlinzi wala msaidizi mbele ya Mwenyezi Mungu﴾.
Hitimisho, ukombozi wa Palestina na nchi zote za Waislamu zilizokaliwa kwa mabavu, Ee Mahdi Al-Mashat, unategemea kuwepo kwa dola kwa Waislamu wote ambayo inahamasisha majeshi na kuandaa vita dhidi ya Wayahudi, kwa mujibu wa kauli ya Mtume, rehema na amani zimshukie, katika hadithi iliyosimuliwa na Abu Hurairah, radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, katika Sahih Al-Jami': «Saa haitasimama mpaka Waislamu wapigane na Wayahudi, na Waislamu watawaua, hata Myahudi atajificha nyuma ya jiwe na mti, na jiwe au mti utasema: Ee Muislamu, Ee mja wa Mwenyezi Mungu, huyu Myahudi yuko nyuma yangu, njoo umuue. Isipokuwa Gharqad, kwa hakika ni mti wa Wayahudi». Dola hiyo ni dola ya haki na uadilifu, Khilafah Rashidah ya pili kwa njia ya Utume ambayo ilitabiriwa na mkweli mwaminifu katika hadithi iliyosimuliwa na Hudhaifa bin Al-Yaman, radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake: «Kisha itakuwa Khilafah kwa njia ya Utume» basi kufanya kazi ya kuisimamisha ni wajibu wa lazima, kwa sababu kile ambacho wajibu hautimii isipokuwa kwacho, basi ni wajibu, na hiyo ndiyo njia halali ya kisheria ya kuikomboa Palestina na kuwasaidia watu wake, na Mwenyezi Mungu ndiye msaidiwa.
Imeandikwa kwa ajili ya idhaa ya Ofisi Kuu ya Habari ya Hizb ut-Tahrir
Abdullah Al-Qadi - Wilaya ya Yemen