Farao wa Misri Anaimba Amani ya Haki na Ujasiri!
Habari:
Rais wa Misri al-Sisi alisema katika hotuba aliyoitoa katika kumbukumbu ya vita vya Oktoba "Amani ya haki na ujasiri kati ya Misri na Israel imemaliza mzunguko wa kisasi, imevunja ukuta wa uadui na kufungua ukurasa mpya katika historia" (Mtandao wa Rasd, 06/10/2025)
Maoni:
Hakika, ikiwa hauna haya, basi fanya unachotaka! Huyu Farao anazungumzia amani ya haki na ujasiri na taifa la Kiyahudi, wakati taifa hili linaonyesha uchafu na ukatili ambao hata wanyama wakali hukataa na kujiepusha nao, wameharibu Gaza kabisa na kuifanya kuwa magofu, na wamemwaga damu ya mamia ya maelfu ya watu wake. Vipi Farao wa Misri anaweza kuzungumzia makubaliano ya amani ya haki na ujasiri na taifa kama hilo?!
Anasema kuwa amani hii imemaliza mzunguko wa kisasi na kuvunja kizuizi cha uadui kati ya watu wa Misri na Wayahudi, je, Farao huyu amefungua mipaka na Gaza kwa Wamisri ili kuona kwa macho yake jinsi watakavyofanya taifa la Wayahudi kuwa kitu cha zamani?
Al-Sisi anasema uongo huku akijua kwamba anasema uongo kwa kudai kwamba uadui na kisasi vimeisha baada ya kufikia makubaliano ya amani na taifa la waliokasirikiwa, hawaheshimu makubaliano au mkataba wowote na kila wanapopata nafasi wanakiuka makubaliano na kuvunja ahadi, na mifano ya hiyo ni mingi, iwe zamani au sasa, na kabla ya muda mfupi Netanyahu, adui wa Mungu, alikuwa akizungumza na kutangaza "Israeli Kubwa" ambayo inajumuisha Syria, Lebanon, Misri, Iraq na sehemu za Uturuki. Hii inaonyesha bila utata kwamba hali ya uadui na kisasi kwa Wayahudi haijaisha, lakini imeisha tu kwa Wazayuni kama al-Sisi na kundi la watawala duni ambao kwa kweli wameandika ukurasa mpya katika historia uliojaa aibu, udhalilishaji na njama.
Imeandikwa na Idhaa ya Ofisi Kuu ya Habari ya Hizb ut-Tahrir
Walid Bleibel