Katika Maadhimisho ya Miaka 76 ya Ukoloni: Turkestan Mashariki Yaiomba Umma wa Kiislamu Msaada
Habari:
1 Oktoba: Maadhimisho ya 76 ya Uchina kuikalia Turkestan Mashariki.
Maoni:
Ilikuwa mwaka 1949 wakati Uchina ilipoikalia Turkestan Mashariki na tangu wakati huo hadi leo imekuwa ikifanya uhalifu mbaya zaidi dhidi ya watu wake kulingana na kile kilichovuja kutoka maelfu ya nyaraka zinazolaani na kufichua uhalifu wa Uchina, ambayo inajibu matendo hayo kwa kusema kwamba inapinga ugaidi.
Uchina imeandaa kambi ambazo inawahifadhi watu wa Turkestan na inadai kuwa ni kambi za urekebishaji na elimu na kupambana na ugaidi. Kambi ambazo watu wa Turkestan wanang'olewa kutoka katika utamaduni wao wa Kiislamu na kupandikizwa utamaduni wa ukafiri na ukomunisti. Inafanya kazi ya kuibadilisha jamii hii kuwa sehemu ya Uchina isiyoamini Mungu na kupambana na Uislamu.
Katika Turkestan Mashariki na katika miongo hii mirefu, Waislamu wameteseka sana kutokana na kukamatwa kwa wanawake na kuvuliwa khimaa zao na kuwashambulia na kuwabaka na kuwalazimisha kutoa mimba na kuwanyima waume na watoto wao. Watoto hawakuokoka uhalifu wa Uchina, ambayo inafanya kazi ya kuwanyima familia zao na kuwafanyia usafi wa akili na kuwarekebisha kwa kuwashibisha utamaduni wa Uchina wa kikomunisti usioamini Mungu. Kwa hivyo inatafuta kuzima kizazi kijacho cha Waislamu na kukigeuza kuwa kizazi kisichoamini Mungu ambacho hakina uhusiano wowote na Uislamu na watu wake.
Katika hatua mpya ambayo inakuja ndani ya mpango kamili unaoongozwa na Chama cha Kikomunisti cha China chini ya kauli mbiu ya "Uislamu wa Kichina unaoendana na Ujamaa", Maulamaa na wahubiri walikamatwa na Misahafu ilichomwa na misikiti ilibomolewa na kubadilishwa kuwa baa na kumbi za starehe, na pia walifuta maneno ya Kiarabu na alama za kidini kutoka maeneo ya umma.
Katika juhudi kubwa za kung'oa utambulisho wa watu ambao bado wamekuwa wakipinga na hawajisalimishi kwa miongo kadhaa, Uchina imeongeza njia za kuwatesa watu wa Turkestan Mashariki na imefanya ubunifu katika njia za kuwatesa ili waache Uislamu. Licha ya kile wanachopata, watu hawa wanasimama dhidi yake na silaha ya itikadi yao, uvumilivu wao na imani yao. Watu hawa ambao Misahafu yao ya Qur'ani imechomwa moto, lakini mioyo ya watoto wao imejaa Qur'ani na wana ihifadhi. Watu hawa ambao wanashikilia dini yao kama mshika bara moto, wanaungua na aina zote za mateso na dhuluma na wanaliomba umma wa Kiislamu uinuke kuwasaidia na kuwaokoa kutoka kwenye makucha ya joka hili baya. Je, kuna anayejibu?
Katika maadhimisho haya ya 76, Shirika la Mashirika ya Turkestan Mashariki ya Kimataifa, kwa kushirikiana na mashirika mengine 17, liliandaa maandamano makubwa ya kupinga mbele ya Ubalozi Mdogo wa China huko Istanbul, kuonyesha kwa nguvu kukataa kwao uvamizi na mauaji ya kimbari, na kusisitiza msimamo wao dhidi ya mkoloni Mchina. Je, kwa maandamano kama haya mauaji haya ya kimya kimya yatakomeshwa? Je, Uchina itaacha mikono yake kutoka kwa watu wa Turkestan kwa maandamano au kususia bidhaa?
Kinachotokea katika Turkestan Mashariki ni mauaji ya kimya kimya ya watu wanaosema "Mola wangu ni Allah", mauaji yanayoongezwa kwa kile kinachotokea Gaza, Myanmar, Kashmir na nchi nyingine za Waislamu. Inatafsiri mauaji ya kimbari ambayo umma wa Kiislamu unakabiliwa nayo kwa damu baridi na mbele ya macho ya ulimwengu, na hakuna wa kulia kwa watoto wake, kwani wao ni kama mayatima kwenye meza za watu wabaya.
Je, watoto wa umma wa Kiislamu hawajatambua kwamba dini yao na ustaarabu wao ndivyo vinavyolengwa na Magharibi makafiri na vibaraka wao? Je, wametambua kwamba ni vita vya ustaarabu: ustaarabu wa Magharibi makafiri unajitahidi sana kuangamiza ustaarabu wa Uislamu na unafanya kazi ya kuuzima. Mko wapi enyi watoto wa umma waaminifu, enyi mnaoshuhudia kwamba hapana mola apasae kuabudiwa kwa haki ila Allah na kwamba Muhammad ni mjumbe wa Allah? Mko wapi wakati hawa wanawasili usiku wao kwa mchana wao wakipanga na kupigana na dini yenu?! Ni lini damu ya wivu kwa ajili ya dini ya Allah itachemka katika mishipa yenu ili mnyanyuke kama mtu mmoja mnainusuru dini ya Allah na kuinua bendera yake na kulipiza kisasi kwa maadui zake?!
Imeandikwa kwa ajili ya redio ya Ofisi Kuu ya Habari ya Hizb ut-Tahrir
Zina Al-Samet