Katika mfumo wa kibepari hakuna mashirika ya kibinadamu kwa maana ya kibinadamu
Habari:
Kituo cha Metro cha Uangalizi wa Uhuru wa Uandishi wa Habari huko Sulaymaniyah, kilitangaza siku ya Jumapili, Septemba 7, 2025, kwamba watu wenye silaha walishambulia ofisi iliyokuwa na idadi ya mashirika ya ndani na ya kimataifa, katika tukio ambalo walielezea kama "ukiukaji mbaya" wa sheria za kimataifa, wakionya kwamba mashambulizi haya yanaweza kugeuza eneo la Kurdistan kuwa "mazingira yasiyo salama" kwa kazi ya mashirika ya kimataifa.
Kituo hicho kilisema katika taarifa iliyopokelewa na Shirika la Habari la Shafaq, kwamba "ofisi ya (Baya) iliyoko katika eneo la Sarjanar katika mji wa Sulaymaniyah, karibu na nyumba ya Lahor Sheikh Jangi na hoteli ya Lala Zar, inajumuisha mashirika kadhaa ya kitamaduni, kimazingira na ya kimataifa, pamoja na: Shirika la Berdedar la Maendeleo ya Vijana, Baya Agency, Art Plus, Walinzi wa Maji wa Iraq na Kurdistan, na shirika la (UPP) la Italia".
Taarifa hiyo ilionyesha kuwa "shambulio lililolenga ofisi iliyokuwa na mashirika ya ndani na ya kimataifa na kuchukua mali zao na kuzipeleka mahali isipojulikana, halina msingi wowote wa kisheria na ni ukiukaji wazi wa sheria za kimataifa za haki za binadamu, na pia linazuia kuendelea kwa kazi ya mashirika haya, na linatishia kuifanya eneo la Kurdistan kuwa eneo hatari kwa kazi ya mashirika ya kigeni". (Shafaq News, 2025/9/7)
Maoni:
Mkoloni Mmarekani hakutosheka na kuangusha utawala wa Iraq, bali alidhibiti kikamilifu viungo vyote vya serikali, akaweka mfumo wake wa kisiasa wa shirikisho kulingana na madhehebu na utaifa, akaweka katiba yake, na akaongeza mashirika yanayoitwa ya kiraia na kibinadamu, ambayo kwa kweli ni mashirika yenye lengo la kulazimisha utamaduni wake, zaidi ya hayo ni mashirika ya kijasusi.
Kituo cha Metro kilianzishwa Agosti 2009 kwa mpango wa waandishi wa habari na watetezi wa haki za binadamu huko Sulaymaniyah, na kwa msaada wa Taasisi ya Uandishi wa Habari wa Vita na Amani ya Marekani, na Taasisi ya Republican ya Kimataifa inayofadhiliwa na serikali ya shirikisho ya Marekani, na wengi wa wajumbe wa baraza lake wanatoka Chama cha Republican, na Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani. Pia inapata msaada kutoka kwa mashirika ya kimataifa, ikiwa ni pamoja na Shirika la Misaada ya Watu wa Norway, na Shirika la Usaidizi wa Vyombo vya Habari vya Kimataifa.
Haya ndiyo mashirika wanayoyaita ya kibinadamu; mashirika ya kisiasa yanayosaidia mkoloni kulazimisha utawala wake na yanatii sera ya mataifa ya kibepari, kama ilivyo kwa Umoja wa Mataifa na Shirika la Fedha la Kimataifa.
Kwa hivyo ikiwa tunataka ukombozi, hatuwezi kuishia tu na kuondoka kwa mkoloni, lakini ni lazima tukombolewe kutoka kwa mashirika yote yanayomtegemea chini ya jina lolote. Hapo awali, umma ulitoa dhabihu kubwa ili kumtoa mkoloni kutoka Algeria, Libya na nchi zingine za Waislamu, lakini matokeo yalikuwa nini? Matokeo yake ni kwamba nchi za Waislamu zilibaki zikikaliwa katika mfumo wao wa kisiasa, kiuchumi na kiutamaduni, na zilibaki mateka wa Magharibi kafiri na mfumo wake mbovu wa kibepari.
Enyi Waislamu: Ukombozi wote ni kwa kung'oa mfumo wa kibepari kwa aina zake zote na mashirika yake, na kuanzisha utawala wa Kiislamu na mifumo yake yote ya kisiasa, kiuchumi na kiutamaduni, katika dola moja na imamu mmoja, na wakati huo tu tunaweza kutangaza kwamba nchi za Waislamu zimekombolewa.
Imeandikwa kwa ajili ya Radio ya Ofisi ya Habari Kuu ya Hizb ut-Tahrir
Ahmed Al-Tai - Jimbo la Iraq