Gaza Inateseka kwa Njaa Lakini Watawala wa Kiislamu Wamebaki Viziwi, Bubu na Vipofu!
(Imetafsiriwa)
Habari:
Mgogoro wa njaa huko Gaza, katika kivuli cha uvamizi wa chombo cha Kiyahudi, umefikia "hatua muhimu," kulingana na wataalam na wafuasi wa mtandao wa NBC News, ambapo idadi ya vifo inatarajiwa kuongezeka sana ikiwa Wapalestina hawapati msaada wa haraka. Walionya kuwa watoto wengi wanaookoka utapiamlo watakabiliwa na matokeo mabaya maishani. Keren Lanning, mkurugenzi mkuu wa dharura katika Kamati ya Uokoaji ya Kimataifa, shirika la kibinadamu lenye makao yake makuu nchini Marekani, alisema "nafasi ya kuzuia vifo vya halaiki inapungua kwa kasi, na kwa wengi imechelewa." Shirika la Afya Duniani limeonya kuwa "afya na ustawi wa kizazi kijacho kizima" viko hatarini.
Maoni:
Chombo cha Kiyahudi, kinachoungwa mkono na Amerika, kinabeba jukumu kubwa kwa njaa ya halaiki huko Gaza. Tangu 2007, kiliweka mzingiro wa nchi kavu, anga na baharini dhidi ya Gaza, na hivyo kuzuia kuingia kwa chakula, mafuta na vifaa vya matibabu kwa watu wa Gaza. Katika ukatili wake, inabomu mashamba, maeneo ya uvuvi na vituo vya maji. Imethibitika kuwa chombo cha Kiyahudi kinatumia njaa kama njia ya kuwaadhibu watu wa Gaza na kumshinikiza Hamas kwa kufanya maisha yasiweze kuvumilika. Jeshi lake liliendelea na uhalifu wake kwa kushambulia misafara ya misaada ya chakula, ambayo inapingana na kile kinachoitwa sheria ya kimataifa ya kibinadamu.
Matumizi ya njaa kama mbinu ya vita ni uhalifu chini ya Kifungu cha 8 cha Mkataba wa Roma wa Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu. Cha kushangaza ni kwamba mahakama hii haijamshtaki rasmi au kutoa hati za kukamatwa kwa jeshi la Kiyahudi hadi sasa. Watu wenye njaa wa Gaza wanaachwa kwa Amerika na Wayahudi, kana kwamba sio wa taifa tukufu ambalo dini na ubinadamu wao hauruhusu mtu mmoja kuwa na njaa? Kimsingi, kulisha mwenye njaa sio tu tendo la hisani katika Uislamu; Ni kanuni ya msingi ya imani, inayoonyesha kujitolea kwa Muislamu kwa uwajibikaji wa kijamii, huruma na kujitahidi kumpendeza Mwenyezi Mungu. Nabii ﷺ alisema: «SI MUUMINI YULE ANALALA AKISHIBA NA JIRANI YAKE ANA Njaa».
Inashangaza kwamba watu wa Gaza wana njaa, wakati watawala wa Kiislamu kote katika nchi za Kiislamu wamebaki viziwi, bubu na vipofu! Wamechukua ukimya huu wa aibu kwa sababu wanatii matakwa ya Amerika ambayo yanatimiza matakwa ya Wayahudi. Katika muktadha huu, serikali ya Misri, Uturuki, Iran na Saudi Arabia zinashirikiana katika kutekeleza mipango mibaya ya Kiyahudi, kama vile kuzingirwa kwa Gaza, kwa lengo la kuvunja utashi wa watu wa Gaza, na kuwatiisha taifa zima la Kiislamu katika hali ya kukata tamaa kabisa. Na majeshi ya Waislamu yajue kwamba Mwenyezi Mungu atawahukumu kwa hali ya Gaza Siku ya Kiyama, na ukimya hautawaokoa kutokana na ghadhabu ya Mungu. Msimamo pekee wa Kiislamu ambao lazima uchukuliwe ni kuvunja mzingiro, na kuandamana ili kukomboa Gaza yote na Palestina.
Imeandikwa kwa Idhaa ya Afisi ya Habari Kuu ya Hizb ut Tahrir
Shaban Muallim
Mwakilishi wa Habari wa Hizb ut Tahrir nchini Kenya