Watawala Waislamu Kibaraka Ni Walinzi wa Maslahi ya Mkafiri Mwenye Kukalia
Habari:
Waziri wa Mambo ya Ndani wa Iraq ametoa uamuzi wa kuwaondoa madarakani maafisa wakuu watano wa usalama katika wilaya ya Tuzkhurmato, baada ya kukanyaga bendera ya Amerika wakati wa sherehe za Ashura, na picha zao zilienea katika idadi ya vyombo vya habari na mitandao ya mawasiliano.
Karim Shukur, mbunge katika Bunge la Iraq kutoka kambi ya Muungano wa Kitaifa wa Kikurdi kwa wilaya ya Tuzkhurmato, alithibitisha habari hiyo kwa mtandao wa habari wa Rudaw siku ya Jumatatu, Julai 7, 2025, na akasema: "Wakati wa sherehe za Ashura, maafisa hawa walikanyaga bendera ya Amerika, na kwa hivyo Waziri wa Mambo ya Ndani wa Iraq, Abdul Amir al-Shammari, alitoa uamuzi wa kuwaondoa." (Mtandao wa Rudaw)
Maoni:
Baada ya ndege zisizo na rubani zisizojulikana zililenga idadi ya rada katika maeneo kadhaa, na kutayarisha shambulio linalotarajiwa dhidi ya viongozi watiifu, Waziri wa Mambo ya Ndani wa Iraq alitoa uamuzi wa kuwaondoa madarakani maafisa wakuu watano wa usalama katika wilaya ya Tuzkhurmato, baada ya kukanyaga bendera ya Amerika wakati wa sherehe za Ashura, na picha zao zilienea katika idadi ya vyombo vya habari na mitandao ya mawasiliano ya kielektroniki.
Hatua hii inavutia sana, kwani inatoa dalili mbili:
Kwanza: Kujitolea kwa vyombo vya serikali katika mstari wa Kimarekani katika kuondoa zulia chini ya miguu ya Iran na wale wanaoiunga mkono kutoka kwa watu binafsi na vyeo.
Pili: Ujumbe kwa wengine kutoka kwa hawa kwamba jambo hilo ni zito na sio mchezo, na yeyote atakayejaribu kupinga atapata kuondolewa huku, ikiwa sio kuondolewa kimwili.
Hii ndiyo hali halisi ya mifumo hii kibaraka, walinzi wa maslahi ya mabwana zao makafiri na mapanga makali juu ya shingo za watu wao.
Enyi Waislamu: Asili kwa wote ni kuzingatia kile ambacho Mwenyezi Mungu ameamrisha, sio maagizo ya Magharibi wala matamanio ya kimadhehebu machafu ambayo yanatafuta kuvunja safu za Waislamu, na Mwenyezi Mungu amekataza ushabiki kupitia ulimi wa Mpendwa Mtume Muhammad, rehema na amani zimshukie, akisema: «SIO KATIKA SISI YULE ANAYEITIA USHABIKI» kama alivyokataza kuwafuata Mayahudi na Wakristo, kama alivyosema: ﴿MAYAHUDI WALA WAKRISTO HAWATAKURIDHIA KAMWE MPATAPOFUATA MILA YAO. SEMENI: UONGOFU WA MUNGU NDIYO UONGOFU. NA KAMA UKIFUATA MATAMANIO YAO BAADA YA YALE YALIYOKUFIKIA KATIKA ILIMU, HAUTAPATA MDHAMINI WALA MSAIDIZI KWA MUNGU.﴾.
Haijuzu kunyenyekea kwa batili haijalishi ni kwa namna gani, bali ni kujisalimisha tu kwa yale ambayo Mwenyezi Mungu ameyaamrisha, kwani ndani yake kuna utulivu, uthabiti na ushindi, kwa hivyo hakuna wokovu kwetu wala hali yetu haitengemae isipokuwa kwa kurudi kwenye njia ya Mwenyezi Mungu na kuishikilia.
﴿MKIWA NUSURU MUNGU, ATAWANUSURU﴾
Imeandikwa kwa Ajili ya Redio ya Afisi ya Habari Kuu ya Hizb ut Tahrir
Wael Al-Sultan - Jimbo la Iraq