Watawala wa Kiislamu Wanatoa Msaada wa Kijasusi kwa Maadui wa Umma na Wanafanya Njama Dhidi ya Masuala Yake Muhimu
Habari:
Middle East Eye ya Uingereza: Kambi za kijeshi ambazo Imarati ilianzisha katika visiwa vya Yemen zinawezesha kubadilishana kijasusi kati ya taasisi ya Kiyahudi na Abu Dhabi. (Kituo cha Televisheni cha Belqees, 4 Oktoba 2025).
Maoni:
Satellaiti zimefichua uanzishwaji wa kambi kadhaa za kijeshi na Imarati katika visiwa vya Yemen ambavyo imekuwa ikividhibiti tangu ilipoingia Yemen mwaka 2016 kwa kisingizio cha kupambana na Wahouthi. Tangu wakati huo, imekuwa ikizingatia uwepo wake katika visiwa, pwani za Yemen, bandari na miji ya pwani, licha ya ukweli kwamba Wahouthi hawapo katika maeneo hayo, ambayo inafichua malengo halisi ya uwepo wake wa kijeshi huko, ambayo ni kushindana na ushawishi wa Saudi na Amerika nchini Yemen ili Amerika isitawale ushawishi na utajiri nchini.
Satellaiti zimefichua kambi za kijeshi na maeneo ya kutua ndege yanayoweza kupokea ndege za kivita za hali ya juu katika visiwa hivyo, na Middle East Eye hivi karibuni ilifichua kwamba kambi hizi za kijeshi zinawezesha taasisi ya Kiyahudi kubadilishana kijasusi na Abu Dhabi! Jambo linaloashiria ushirikiano wa kijeshi na kijasusi kati yake na Imarati.
Hii inathibitisha kwamba watawala wa Waislamu ni wasaliti kwa umma wao na wanafanya njama dhidi yake kwa faida ya adui wa Mwenyezi Mungu na adui yake, taasisi ya Kiyahudi ambayo Uingereza ilipanda katika eneo hilo na iliyokumbatiwa na Amerika na Magharibi yote nyuma yake leo.
Kwa hivyo, haifai kwa watu wa Yemen kushirikiana na kufanya kazi na Imarati, wala na vyombo vya usalama na kijeshi ambavyo imeanzisha nchini, kama vile vile vinavyoitwa wasomi na mikanda ya usalama. Bali, haifai hata kushughulika na vyama ilivyoanzisha kama vile Baraza la Mpito, au na maafisa walio chini yake! Kwa sababu miamala hii ni msaada na uwezeshaji wa kazi ya Imarati nchini, ambayo inachukuliwa kuwa utekelezaji wa ajenda za Magharibi na ushirikiano wa kijeshi na kijasusi na maadui wa umma, na katika muktadha huu, tamko la Baraza la Mpito, ambalo lilianzishwa na Imarati, la utayari wake wa kuanzisha uhusiano wa kawaida na taasisi ya Kiyahudi!
Enyi watu wetu wa Yemen: Njia ya ukombozi kutoka kwa dhuluma ya ukoloni, kurejesha utajiri na kukomesha umwagaji damu haitakuwa kwa kufuata viongozi hawa ambao usaliti wao umefichuliwa, bali kwa kufuata mradi wa Uislamu kwa kuanzisha Khilafa Rashidah kwa njia ya Utume, ambayo inatawala kwa sheria ya Mwenyezi Mungu na kuwafukuza makafiri wakoloni na wasaidizi wao wa ndani kutoka nchini na kuwaokoa watu kutoka kwa uovu wao na njama zao. Mwenyezi Mungu amesema: ﴿Na hakika Mwenyezi Mungu atamsaidia yule anayemsaidia Yeye. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye Nguvu, Mwenye kushinda.﴾
Imeandikwa kwa ajili ya Idhaa ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut-Tahrir
Abdul Aziz Al-Hamid - Wilaya ya Yemen