Hakika Imamu ni ngao
Habari:
Rais wa Marekani Donald Trump alitoa matamshi ya kushtua akitangaza kwamba ameielekeza Wizara ya Vita ya Marekani kujiandaa kwa operesheni yoyote ya kijeshi inayoweza kufanyika nchini Nigeria, kwa madai ya kuwalinda Wakristo dhidi ya makundi ya Kiislamu yenye silaha. Waziri wa Vita wa Marekani alisisitiza katika taarifa ya ziada: kwamba Amerika haitasimama mikono mitupu mbele ya kile alichokiita ugaidi wa Kiislamu unaotishia Wakristo, akiiomba Nigeria kuchukua hatua ama kuwalinda, au tutaingilia moja kwa moja kuangamiza magaidi wa Kiislamu.
Wakati wachambuzi waliona kuwa hotuba ya Marekani inaonyesha upendeleo wa kidini wa wazi chini ya kivuli cha kupambana na ugaidi. Matamshi ambayo yalizua wimbi kubwa la ukosoaji na wengi waliona kama mfano wa sera ya Magharibi inayotegemea kuwalinda wafuasi wake kwa jina la ubinadamu, huku ikinyamaza kimya mbele ya damu ya Waislamu inayomwagika huko Palestina, Lebanon, Syria, Uyghur, Burma, Kashmir, Afrika ya Kati na kwingineko. (2025/11/3)
Maoni:
Je, haijafika wakati kwa Waislamu kujifunza kutokana na misimamo ya Magharibi na viongozi wake?! Huyu hapa Rais wa Ulaikishaji anaacha ulaikishaji wake ambao anauimba usiku na mchana na anaapa kuwatetea Wakristo kwa jeshi lake, si kwa sababu nyingine ila ni kwa uadui wao na chuki yao kwa Uislamu na Waislamu. Na wakati Waislamu wanachinjwa mashariki na magharibi mwa dunia, hausikii neno kutoka kwa watawala na viongozi na majeshi ambayo yameapa kuwalinda!
Tukio hili linaonyesha utata wa wazi kati ya yule ambaye anamiliki dola inayompelekea kuunga mkono itikadi yake, hata ikiwa ni batili, na kupigana na isiyo kuwa hiyo, na umma wa Kiislamu ambao umetenganishwa na Magharibi kafiri na watawala wake waliowekwa juu yao ambao wameonja unyonge na utegemezi dhahiri kwa Magharibi.
Kukosekana kwa Khalifa ambaye anautetea Uislamu na Waislamu ndio chanzo cha ugonjwa, na umma hautarejesha utukufu wake isipokuwa pale utakapokuwa na mtu wa kuwaongoza kwa Uislamu na kukusanya utengano wao chini ya bendera yake. Ama wale watawala watiifu kwa Magharibi kafiri, wao ndio sababu ya udhaifu na upotevu, na hakuna jema litatarajiwa kutoka kwao kwa umma wao maadamu wanafuata nyayo za mabwana zao.
Na hivyo, maneno ya Trump na msimamo wa Marekani ya Kisalibi sio chochote ila kioo cha hali halisi iliyogeuzwa, somo linaloeleweka kutoka kwa taarifa ya Trump na Wizara yake ya Vita sio katika tishio lake, bali katika wivu wao kwa wale wanaowaona kuwa ni watu wa dini yao, hata kama hawakubaliani naye, kinyume na kuachwa na wale wanaodhaniwa kuwa ni wasimamizi wa Waislamu kwa umma wao. Hiyo ndiyo tofauti kati ya umma ambao una Imamu anayepiganwa nyuma yake, na umma ambao umeachilia mbali Imamu wake na hivyo kupotea katika upepo wa mataifa. Magharibi ina wivu kwa dini yao, na Waislamu hawana mlinzi wa kuwawivu nao. Na kati ya wivu na uzembe, mizani ya nguvu inabaki ikielemea kwa yule ambaye anamiliki utashi, umoja na mamlaka, basi yuko wapi Mu'tasim ambaye atawalinda Waislamu?! Mtume wetu ﷺ alisema: «Hakika Imamu ni ngao anayepiganwa nyuma yake na anaogopwa kwa ajili yake».
Tukio hili linafichua umma kuwa tupu kutoka kwa uongozi wa kweli unaobeba itikadi yake kisiasa ambayo inatafsiri maneno ya Nabii ﷺ: «Muislamu ni ndugu wa Muislamu, hamdhulumu, wala hamtelekezi, wala hamsalimishi». Lakini Waislamu leo wameachwa kama mawindo ya mvutano wa nguvu kubwa, wanatawaliwa na mifumo iliyowekwa kutumikia maslahi ya Magharibi, sio maslahi yao na dini yao, na wamelemaza kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu ﴿Na wakiomba msaada kwenu katika dini, basi ni juu yenu kuwasaidia﴾. Basi wapi msaada kwa watu wetu huko Gaza na Palestina yote, Lebanon, Syria na nchi zote za Waislamu?! Na nani atakayenyanyua bendera ya kuwatetea wanaodhulumiwa kama alivyoinyanyua Ali na Omar wakifuata mfano wa Mtume wa Mwenyezi Mungu ﷺ na wakifanya kazi kwa misingi yake.
Kukosekana kwa dola yenye kuongoza ambayo inawalinda Waislamu na kuunganisha safu zao ndio jeraha kubwa zaidi katika mwili wa umma na jeraha halitapona isipokuwa pale umma utakapopata tena ufahamu wake na heshima yake, na kufanya kazi na Hizb ut-Tahrir kuanzisha tena maisha ya Kiislamu katika uhalisia wa maisha kwa kuanzisha dola ya Khilafah Rashidah, basi kukataa utegemezi na kuamka kwa misingi ya dini yake na uadilifu wake, basi inarudi kwake yule ambaye anabeba upanga wake kwa uaminifu, uadilifu na huruma.
Imeandikwa kwa ajili ya Redio ya Afisi ya Habari Kuu ya Hizb ut-Tahrir
Saif Marzouq - Wilaya ya Yemen