Indonesia Itawatibu Majeruhi 2000 Kutoka Gaza
Habari:
Indonesia imetangaza kuwa itasafirisha kwa ndege majeruhi 2000 kutoka Gaza kwa matibabu katika kisiwa cha Galang. Msemaji wa urais alisema hatua hiyo inalenga misaada ya matibabu na sio makazi mapya, akisisitiza kwamba wagonjwa watarudi makwao baada ya matibabu yao kukamilika.
Maoni:
Indonesia imechukua hatua hii kwa matumaini ya kupunguza ukosoaji wa ndani kuhusu kushindwa kwake kutoa msaada madhubuti kwa Gaza. Nimefanya utafiti wa haraka kuhusu kisiwa cha Galang na nimegundua kuwa ni kisiwa cha mbali kiasi na hakina watu wengi, na pia nimegundua kuwa kinajulikana kihistoria kama kambi ya wakimbizi wa Kivietnam iliyoanzishwa katika miaka ya sabini na themanini. Pia nimegundua kuwa hakina miundombinu iliyoendelezwa ikilinganishwa na miji mikubwa ya Indonesia, na kwamba kwa sasa kinatumika kwa miradi ya serikali, kama vile hospitali za uwanjani au vituo vya karantini, kama ilivyotokea wakati wa janga la COVID-19, ambapo hospitali ya dharura ya Galang ilijengwa kutenga visa vya maambukizi. Ni aibu gani kumpeleka ndugu yako Muislamu aliyejeruhiwa, aliyefadhaika na aliyekata tamaa mahali kama hapo kana kwamba yeye ni duni na hastahili kupata aina bora za huduma ya afya au kana kwamba yeye ni janga ambalo hutaki lienee?!
Anayetaka kweli kuwasaidia watu wa Gaza lazima akomeshe mauaji ya aina zote, kijeshi, chakula na mengineyo, na lolote lililo chini ya hapo halizingatiwi kuwa msaada. Msaada gani huu wa kumlisha na kumtibu kisha kumrudisha katika hali aliyokuwa nayo?! Anayetaka kweli kuwasaidia watu wa Gaza lazima aharakishe majeshi mara moja, kwa kuwa chuma hakikatwi ila kwa chuma, na majeshi hayatohama chini ya tawala vibaraka na wasaliti zilizopo leo katika nchi za Kiislamu, hivyo imekuwa wajibu kwa kuzingatia (yasiyokamilika wajibu ila kwake basi ni wajibu) kuondoa tawala hizi na kusimamisha Ukhalifa Rashid wa pili juu ya manhaji ya utume, na hili ndilo hasa chama cha Hizb ut-Tahrir kinafanya kwa kufuata njia ya Mtume ﷺ katika kujenga dola ya kwanza ya Kiislamu, hivyo tunawakumbusha nyinyi Waislamu ikiwa kweli mnataka kuwasaidia watu wa Gaza.
Imeandikwa kwa ajili ya redio ya Ofisi ya Habari Kuu ya Hizb ut-Tahrir
Jaber Abu Khater