2025-07-02
Jarida la Ar-Raya:
Jibu la Swali
Uchokozi wa Taasisi ya Kiyahudi dhidi ya Iran na Matokeo yake
Swali:
Al-Arabiya ilichapisha kwenye tovuti yake mnamo 2025/6/27: (Vyanzo 4 vya kuaminika vilisema kuwa utawala wa Rais Donald Trump ulijadili uwezekano wa kuisaidia Iran kupata hadi dola bilioni 30 ili kujenga mpango wa nyuklia wa kuzalisha nishati kwa madhumuni ya kiraia. Vyanzo viliongeza kuwa mazungumzo haya yaliendelea wiki hii baada ya makubaliano ya kusitisha mapigano kufikiwa. Maafisa wa utawala wa Trump walithibitisha kuwasilisha mapendekezo kadhaa, ambayo ni mapendekezo ya awali na yaliyokuzwa na kipengele kimoja kisichobadilika ambacho hakiwezi kujadiliwa ambacho ni "kusimamisha kabisa urutubishaji wa uranium wa Iran"). Trump alikuwa ametangaza kuanza kutumika kwa usitishaji mapigano aliyopendekeza kati ya Iran na taasisi ya Kiyahudi, (Netanyahu alisema kuwa alikubali pendekezo la Trump. Shirika la habari la Reuters pia lilimnukuu afisa mkuu wa Iran akisema kwamba Tehran ilikubali kusitisha mapigano kupitia usuluhishi wa Qatar na pendekezo la Amerika. Al-Jazeera, 2025/6/24). Haya yote yalitokea baada ya vikosi vya Trump mnamo 2025/6/22 kushambulia vituo vya nyuklia vya Iran, na baada ya taasisi ya Kiyahudi kuzindua uchokozi mpana wa ghafla dhidi ya Iran tangu 2025/6/13. Swali hapa ni kwa nini taasisi ya Kiyahudi ilifanya uchokozi huu wa ghafla, ambao haifanyi isipokuwa kwa amri ya Amerika? Je, Iran haitembei katika mzunguko wa Amerika, kwa hivyo Amerika ilishiriki vipi katika kushambulia vituo vya nyuklia vya Iran? Asante.
Jibu:
Ili jibu liwe wazi, tutaangalia mambo yafuatayo:
1- Ndiyo, mpango wa nyuklia wa Iran unachukuliwa kuwa hatari kubwa kwa taasisi ya Kiyahudi, kwa hivyo inataka kuiondoa kwa njia zote, na kwa sababu hiyo ilishangilia uamuzi wa Rais Trump mwaka 2018 kujiondoa kwenye makubaliano ya 2015, na msimamo wa taasisi ya Kiyahudi ulikuwa wazi kuwa inakubali tu mfumo wa Libya na Iran kuvunja mpango wake wa nyuklia, yaani, Iran kuachana na mpango wake wa nyuklia kabisa. Iliimarisha majasusi wake ndani ya Iran kwa ajili hiyo. Shambulio la taasisi ya Kiyahudi katika siku yake ya kwanza lilifichua jeshi la vibaraka ndani ya Iran ambao walikuwa wakifuatilia na kushirikiana na shirika la ujasusi la taasisi ya Kiyahudi "Mossad" kwa ajili ya kupata dirhamu chache, wanaagiza vipuri vya ndege zisizo na rubani na kuzikusanya katika warsha ndogo ndani ya Iran na kuzirusha kwenye malengo ambayo yanajumuisha nyumba za viongozi wa serikali ya Iran katika hali ambayo inafanana na kile kilichotokea kwa chama cha Iran nchini Lebanon wakati taasisi ya Kiyahudi ilipowaua viongozi wake!
2- Msimamo wa Amerika ulikuwa msaada mkuu kwa taasisi ya Kiyahudi, bali ni kichocheo chao dhidi ya mradi wa nyuklia wa Iran, lakini Trump aliweka mezani kufanikisha hilo: Suluhisho la mazungumzo na suluhisho la kijeshi. Hivyo ndivyo Amerika na Iran zilielekea Muscat-Oman mnamo Aprili 2025 kwa mazungumzo, na utawala wa Trump ulikuwa ukisifu kwa kina cha makubaliano ambayo yalikuwa yakifanyika katika mazungumzo ya nyuklia kana kwamba makubaliano mapya ya nyuklia yalikuwa karibu sana. Trump alikuwa ameweka muda wa miezi miwili kukamilisha makubaliano haya, na maafisa wa taasisi ya Kiyahudi walikuwa wakikutana na mjumbe wa Marekani katika eneo hilo na mpatanishi mkuu wa Iran, Witkov, karibu mara moja kabla ya kila mkutano na ujumbe wa Iran kumjulisha mpatanishi wa Marekani kile kilichokuwa kinaendelea katika mazungumzo...
3- Utawala wa Trump uliunga mkono maoni magumu ya baadhi ya watu wake muhimu, maoni ambayo yanaendana na taasisi ya Kiyahudi. Hiyo iliambatana na kuibuka kwa maoni magumu huko Ulaya pia, kwani nchi za Ulaya zilikasirishwa na ukweli kwamba Amerika ilikuwa ikizungumza na Iran peke yake, ambayo inamaanisha kwamba Amerika ingepata sehemu kubwa ya makubaliano yoyote na Iran, haswa kwani Iran ilikuwa ikitamanisha utawala wa Trump kwa kuzungumza juu ya mamia ya mabilioni ya dola ambazo kampuni za Amerika zinaweza kuwekeza na kufaidika nazo ndani ya Iran kama vile mikataba ya mafuta na gesi, kampuni za ndege na mengine mengi, na maoni hayo magumu yalikamilika kwa kuonekana kwa ripoti ngumu kutoka Shirika la Kimataifa la Nishati ya Atomiki: (Kwa mara ya kwanza katika karibu miaka 20, Bodi ya Magavana ya Shirika la Kimataifa la Nishati ya Atomiki ilitangaza Alhamisi hii "Juni 12/2025" kwamba Iran imekiuka majukumu yake katika uwanja wa kuzuia kuenea kwa silaha za nyuklia... Deutsche Welle ya Ujerumani, 2025/6/12), na Kiongozi Mkuu wa Iran alikuwa amekataa hapo awali kusimamisha urutubishaji: (Khamenei alisema: "Kwa kuwa mazungumzo yanaendelea, nataka kutoa onyo kwa upande mwingine. Upande wa Amerika, ambao unashiriki katika mazungumzo haya yasiyo ya moja kwa moja na unafanya majadiliano, haupaswi kusema maneno ya kipuuzi. Kusema kwao "Hatutaruhusu Iran kurutubisha uranium" ni kosa kubwa; Iran haisubiri idhini ya mtu huyu au yule"... Na Witkov, mjumbe wa Trump katika Mashariki ya Kati, alisema Jumapili kwamba Washington haitakubali kiwango chochote cha urutubishaji wa uranium katika makubaliano yanayoweza kufanyika na Tehran. Witkov aliongeza katika mahojiano na mtandao wa "ABC News": "Hatuwezi kuruhusu hata asilimia moja ya uwezo wa urutubishaji. Kila kitu kinaanzia kwa mtazamo wetu na makubaliano ambayo hayajumuishi urutubishaji." Gazeti la Iran International, 2025/5/20).
4- Kwa kukataa kwa Iran kusimamisha urutubishaji na kusisitiza kwa Amerika kusimamisha, mazungumzo ya Amerika na Iran yalifikia mwisho, hata kama mwisho wa mazungumzo haukutangazwa, lakini na kutolewa kwa ripoti ya Shirika la Kimataifa la Nishati ya Atomiki mnamo 2025/6/12, taasisi ya Kiyahudi ilikimbilia katika mpango iliyoandaliwa usiku na Amerika na ilifanya shambulio la ghafla mnamo 2025/6/13 ambapo ilishambulia kituo cha nyuklia cha Iran katika eneo la Natanz, ambalo ni kiwanda kikubwa zaidi cha Iran cha kurutubisha uranium na kina vifaa 14,000 vya centrifuges, na ilifanya mfululizo wa mauaji ya viongozi wa Jeshi na Walinzi wa Mapinduzi ya Iran, pamoja na wanasayansi wa nyuklia, na ilishambulia majukwaa ya kurusha makombora, na bila kujali uhalali wa taasisi ya Kiyahudi kwa sababu za shambulio lake kwamba Iran ilikuwa imeanza tena utafiti na maendeleo ya silaha za nyuklia, kulingana na maneno ya Netanyahu (RT, 2025/6/14), lakini haya yote yanapingwa na taarifa nyingi za Iran kwamba Iran haipangi kuzalisha silaha yoyote ya nyuklia, na kwamba inakubali kiwango chochote cha udhibiti wa kimataifa ili kuhakikisha amani ya mpango wake wa nyuklia. Lakini pia ni jambo la hakika kwamba taasisi ya Kiyahudi ilikuwa ikingojea mwanga wa kijani wa Amerika ili kutekeleza, na wakati taasisi ilipoona kwamba dirisha hili limefunguliwa na mwanga wa kijani, ilianza shambulio.
5- Hivyo, haiwezekani kwa mtu mwenye akili timamu kufikiria taasisi ya Kiyahudi kufanya shambulio kama hilo bila mwanga wa kijani kutoka kwa Amerika, kwani hii haiwezekani kabisa, (Balozi wa Marekani nchini Israel, Mike Huckabee, alisema Alhamisi hii kwamba hatarajii Israel kuishambulia Iran bila kupata "mwanga wa kijani" kutoka Marekani. Arab 48, 2025/6/12). Na baada ya mazungumzo ya simu ya dakika 40 kati ya Trump na Netanyahu (afisa wa Israel alifichua kwa gazeti la "Times of Israel" Ijumaa hii kwamba Tel Aviv Washington walifanya "kampeni kubwa ya kupotosha vyombo vya habari na kiusalama", kwa ushiriki mzuri kutoka kwa Donald Trump, kwa lengo la kumshawishi Iran kwamba shambulio dhidi ya vituo vyake vya nyuklia halikuwa karibu,... Alieleza kwamba vyombo vya habari vya Israel vilipokea wakati huo uvujaji unaodai kwamba Trump alikuwa ameonya Netanyahu dhidi ya kuishambulia Iran, akielezea uvujaji huo kama "sehemu ya operesheni ya udanganyifu". Al-Jazeera Net, 2025/6/13). Inaweza kuongezwa kwa hayo yote Amerika kuipatia taasisi ya Kiyahudi silaha maalum kabla ya shambulio na zilitumika katika shambulio: (Ripoti za vyombo vya habari zilifichua kwamba Marekani kimyakimya ilisafirisha takriban makombora 300 ya aina ya AGM-114 Hellfire hadi Israel Jumanne iliyopita, kulingana na maafisa wa Marekani. Kulingana na gazeti la Jerusalem Post, maafisa hao walithibitisha kwamba Washington ilikuwa na ufahamu wa awali wa mipango ya Israel ya kushambulia malengo ya nyuklia na kijeshi ya Iran alfajiri ya Ijumaa. Pia waliripoti kwamba mifumo ya ulinzi wa anga ya Marekani baadaye ilisaidia kukatiza zaidi ya makombora 150 ya balistiki ya Iran yaliyorushwa kujibu shambulio hilo. Afisa mkuu wa ulinzi wa Marekani alinukuliwa akisema kwamba makombora ya Hellfire "yalikuwa muhimu kwa Israel," akieleza kwamba Jeshi la Anga la Israel lilitumia zaidi ya ndege 100 kuwashambulia maafisa wakuu wa Walinzi wa Mapinduzi na wanasayansi wa nyuklia na vituo vya udhibiti kuzunguka Isfahan na Tehran. RT, 2025/6/14).
6- Hivyo, utawala wa Trump ulipotosha Iran ambayo inazungumza nayo ili kufanya shambulio kutoka kwa taasisi ya Kiyahudi kuwa na ufanisi na kuathiriwa na mshtuko na hofu, na taarifa za Marekani zinaonyesha hili, yaani, Marekani ilitaka shambulio kutoka kwa taasisi ya Kiyahudi liwe kichocheo kwa Iran kutoa makubaliano katika mazungumzo ya nyuklia, ambayo inamaanisha kwamba shambulio hilo lilikuwa chombo kutoka kwa vyombo vya mazungumzo ya Marekani, na hii inaambatana na utetezi wa wazi wa Marekani kwa shambulio la taasisi ya Kiyahudi kwamba ni kujilinda, kuiunga mkono taasisi na silaha na kuendesha ndege za Marekani na mifumo ya ulinzi wa anga ya Marekani ili kuzuia majibu ya Iran, yote hayo yanafikia kuwa shambulio la Marekani lisilo la moja kwa moja, na kutoka kwa taarifa hizo za Marekani ni kauli ya Trump, wakati wa taarifa zake kwa waandishi wa habari, Jumapili, alipokuwa akielekea kwenye mkutano wa G7 nchini Kanada, kwamba ("Vita zingine haziepukiki kabla ya kufikia makubaliano".. Katika mahojiano na mtandao wa "ABC" Trump alionyesha uwezekano wa Marekani kuingilia kati kuisaidia Israel kuondoa mpango wa nyuklia wa Iran.. Arab 48, 2025/6/16).
7- Marekani inatumia vita kama chombo cha kuinyenyekeza Iran kama ilivyo katika taarifa ya awali ya Trump kwamba (baadhi ya vita haziepukiki kabla ya kufikia makubaliano), na kinachothibitisha hilo ni maelezo ya Trump kwa shambulio hili kwa kusema "Shambulio la Israel dhidi ya Iran ni bora," na alisema "Alipa Wairani fursa na hawakuitumia na walipokea pigo kali sana, akithibitisha kwamba kuna zaidi katika siku zijazo"... ABC ya Marekani 2025/6/13). Trump alisema ("Wairani" wanataka kufanya mazungumzo, lakini walipaswa kufanya hivyo hapo awali nilikuwa na siku 60, na walikuwa na siku 60, na katika siku ya 61 nilisema hatuna makubaliano"... CNN ya Marekani, 2025/6/16). Taarifa hizi ni wazi kwamba Marekani ndiyo iliyoruhusu taasisi ya Kiyahudi kuzindua uchokozi huu, bali iliielekeza kufanya hivyo. Trump aliandika kwenye jukwaa la "Truth Social": ("Iran ilipaswa kusaini "makubaliano kuhusu mpango wake wa nyuklia" ambayo niliwaomba wasaini..." Aliongeza: "Kwa kifupi, Iran haiwezi kumiliki silaha za nyuklia. Nilisema hivyo mara kwa mara." RT, 2025/6/16). Afisa kutoka taasisi ya Kiyahudi alieleza kuhusu ushiriki wa Marekani katika kulipua tovuti ya Fordow iliyohifadhiwa chini ya ardhi nchini Iran (kwamba Marekani inaweza kujiunga na operesheni ya kijeshi dhidi ya Iran, akieleza kuwa Trump alionyesha wakati wa mazungumzo na Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu kwamba atafanya hivyo ikiwa ni lazima. Al-Arabiya, 2025/6/15).
8- Hivi ndivyo ilivyotokea kweli, Trump alitangaza alfajiri ya Jumapili 2025/6/22 (kulenga vituo 3 vya nyuklia vya Iran akithibitisha mafanikio ya shambulio la Marekani, na Trump alieleza kulenga maeneo ya Fordow, Natanz na Isfahan ya nyuklia akihimiza Iran kufanya amani na kumaliza vita, kwa upande wake Waziri wa Ulinzi wa Marekani Bert Hegeeset alithibitisha kwamba shambulio la Marekani limeondoa matarajio ya nyuklia ya Iran. BBC, 2025/6/22) na kisha (mtandao wa CNN ulifichua jioni ya Jumatatu kwamba Iran ilishambulia kambi ya Al-Udeid ya Marekani nchini Qatar na makombora ya balistiki ya masafa mafupi na ya kati, ikionyesha kwamba ndege za kijeshi za Marekani zilizokuwa zimeegeshwa kwenye kambi ya ndege zilihamishwa mwishoni mwa wiki iliyopita.. Shirika la habari la Reuters pia lilisema: "Iran iliarifu Marekani saa kadhaa kabla ya kuzindua mashambulio dhidi ya Qatar na pia iliarifu Doha". Sky News Arabia, 2025/6/23) Trump alisema Jumatatu ("Ningependa kuishukuru Iran kwa kutuarifu mapema, ambayo iliruhusu kutokuwa na majeruhi." Sky News, 2025/6/24).
9- Kisha baada ya mashambulio haya ya Marekani na taasisi ya Kiyahudi na majibu ya Iran ambapo hasara za mali zilikuwa kubwa pamoja na hasara za watu: (Msemaji wa Wizara ya Afya ya Iran alisema kuwa mashambulio ya Israel yalisababisha mashahidi 610 na majeruhi wengine 4,746 tangu mwanzo wa mzozo. Kulingana na Wizara ya Afya ya Israel.. idadi ya vifo tangu Juni 13 imeongezeka hadi watu 28.. BBC News, 2025/6/25), baada ya mashambulio haya, Trump kama alivyoanza kwa kuishinikiza taasisi ya Kiyahudi kufanya uchokozi dhidi ya Iran na yeye alishiriki ndani yake, anarudi sasa kutangaza kusitisha mapigano na Wayahudi na Iran wanakubali, kana kwamba Trump ndiye anayeendesha vita kati ya pande hizo mbili na pia ndiye anaihusisha! (Trump alitangaza kuanza kutumika kwa usitishaji mapigano aliyopendekeza kati ya Iran na taasisi ya Kiyahudi). (Netanyahu alisema kuwa alikubali pendekezo la Trump. Shirika la habari la Reuters pia lilimnukuu afisa mkuu wa Iran akisema kwamba Tehran ilikubali kusitisha mapigano kupitia usuluhishi wa Qatar na pendekezo la Amerika. Al-Jazeera, 2025/6/24). Hii inamaanisha kwamba vita hivi ambavyo Trump alizianzisha na kuzisimamisha zilikuwa za kufanikisha malengo yake ya kuondoa ufanisi wa silaha za nyuklia na makombora kutoka Iran (Katika hotuba yake kwa waandishi wa habari kabla ya kuondoka kwenda kuhudhuria mkutano wa kilele wa Jumuiya ya Atlantiki ya Kaskazini "NATO" huko The Hague, Trump alisema ("Uwezo wa nyuklia wa Iran umekwisha na haitajenga tena mpango wake wa nyuklia kamwe" na akaendelea "Israel haitaishambulia Iran. Usitishaji mapigano unaanza kutumika." Al-Jazeera, 2026/6/24).
10- Kuhusu mzunguko wa Iran katika mzunguko wa Amerika, ndiyo, Iran ni nchi inayozunguka katika mzunguko wa Amerika, inatafuta kufanikisha maslahi yake kupitia kufanikisha maslahi ya Amerika. Kwa hivyo ilisaidia Amerika katika uvamizi wake wa Afghanistan na Iraq na kuimarisha uvamizi wake ndani yake. Pia ilingilia kati Syria kulinda wakala wa Amerika Bashar al-Assad, na mfano kama huo huko Yemen na Lebanon. Kwa hivyo inataka kufanikisha maslahi yake katika nchi hizi na kuwa nchi kubwa ya kikanda katika eneo hilo hata kwa kuzunguka katika mzunguko wa Amerika! Lakini walisahau kwamba Amerika ikiwa itaona kwamba maslahi yake yamekwisha kutoka kwa nchi ya mzunguko na inataka kupunguza jukumu na nguvu yake, basi inafanya shinikizo la kidiplomasia, na ikiwa ni lazima kijeshi, kama inavyotokea na Iran katika mashambulio ya hivi karibuni, ili kurekebisha mdundo kwa nchi inayozunguka kwenye mzunguko. Kwa hivyo, kupitia shambulio hili ambalo lilikuwa kwa amri yake na utekelezaji wa taasisi ya Kiyahudi na kwa msaada wake, inafanya mauaji ya uongozi wa kijeshi, hasa sehemu ya nyuklia na washauri ambao walijaribu katika kipindi cha hivi karibuni kuwa na maoni katika kushughulika na taasisi ya Kiyahudi kinyume na matakwa ya Amerika, na haijali nchi hizi kwa sababu inatambua kwamba nchi hizi mwishowe zitakubali suluhisho ambalo Amerika inatengeneza!
11- Hili ndilo limeanza kuonekana waziwazi katika mpango wa Marekani baada ya kusitisha mapigano ili kukomesha silaha za kijeshi za nyuklia za Iran: (Vyanzo 4 vya kuaminika vilisema kuwa utawala wa Rais Donald Trump ulijadili uwezekano wa kuisaidia Iran kupata hadi dola bilioni 30 ili kujenga mpango wa nyuklia wa kuzalisha nishati kwa madhumuni ya kiraia, na kupunguza vikwazo na kuachilia mabilioni ya dola za fedha za Iran zilizozuiliwa, na yote hayo ni sehemu ya jaribio kubwa la kuirudisha Tehran kwenye meza ya mazungumzo, kulingana na mtandao wa CNN wa Marekani. Vyanzo viliripoti kwamba wahusika wakuu kutoka Marekani na Mashariki ya Kati walifanya mazungumzo na Wairani nyuma ya pazia hata katikati ya wimbi la mashambulio ya kijeshi dhidi ya Iran na Israel katika wiki mbili zilizopita. Vyanzo viliongeza kwamba mazungumzo haya yaliendelea wiki hii baada ya kufikiwa kwa makubaliano ya kusitisha mapigano. Maafisa wa utawala wa Trump walithibitisha kuwasilisha mapendekezo kadhaa, ambayo ni mapendekezo ya awali na yaliyokuzwa na kipengele kimoja kisichobadilika ambacho hakiwezi kujadiliwa ambacho ni "kusimamisha kabisa urutubishaji wa uranium wa Iran"... Al-Arabiya, 2025/6/27).
12- Mwishowe, janga la umma huu liko katika watawala wake, kwani Iran inatishiwa kushambuliwa na haichukui hatua ya kushambulia kujitetea, na shambulio ni njia bora ya kujilinda dhidi ya Wayahudi, bali ilibaki kimya hadi vituo vyake viliposhambuliwa na wanasayansi wake waliuawa, kisha ikaanza kujibu, na vivyo hivyo kwa shambulio la Amerika. Kisha Trump anatangaza kusitisha mapigano na Wayahudi na Iran wanakubali. Baada ya hapo, Amerika inaendesha majadiliano na kuweka mapendekezo, na inasema kuhusu "kusimamisha kabisa urutubishaji wa uranium wa Iran" kwamba ni jambo lisilobadilika ambalo haliwezi kujadiliwa! Tunaonya kwamba vita hivi vinaweza kusababisha amani yoyote na taasisi ya Kiyahudi, au kuondolewa kwa silaha za Iran. Kuhusu watawala wengine katika nchi za Waislamu, hasa wale walio karibu na taasisi ya Kiyahudi, ndege za adui zinapita juu ya vichwa vyao na kushambulia nchi za Waislamu na kurudi salama bila kurushiwa risasi! Wao ni laini kwa Amerika. Wanatafsiri kujizuia na kutukuza mipaka, na wamesahau au wamejifanya kusahau kwamba nchi za Waislamu ni moja, iwe iko mbali zaidi au karibu zaidi! Na usalama wa waumini ni mmoja, na vita yao ni moja, haifai kuwatenganisha madhehebu yao mradi tu ni Waislamu. Watawala hawa ni wameharibiwa kwa kile walichomo wanafanya wanafikiri kwamba kwa kunyenyekea Amerika wataokoka, na hawajui kwamba Amerika itawatawala na kuwaondoa silaha zao ambazo zinaweza kuwa tishio kwa taasisi ya Kiyahudi, kama ilivyofanya huko Syria wakati iliporuhusu taasisi ya Kiyahudi kuharibu vituo vyake vya kijeshi, na hivyo ndivyo inavyofanya huko Iran, na kisha itawarithisha watawala hawa wadogo juu ya wadogo duniani na akhera ﴿UTAWAPATA WALE WALIOFANYA MAKOSA DHIKI MBELE YA ALLAH NA ADHABU KALI KWA SABABU YA HILA ZAO﴾ Je, wanaelewa? Au wao ni ﴿VIZIWI, BUBVU, VIPOFU, HAWAELEWI﴾, Je?
Enyi Waislamu: Mnaona na mnasikia kile ambacho watawala wenu wamewafanyia cha unyonge, udhalili na utegemezi kwa makafiri wakoloni, hata Wayahudi ambao wamepigwa na udhalili na unyonge wanazikalia ardhi iliyobarikiwa!.. Na bila shaka mnajua kwamba hakuna heshima kwenu ila kwa Uislamu na dola ya Uislamu, Khilafa Rashidah, mnangozwa ndani yake na Khalifa Rashid ambaye anapigana kutoka nyuma yake na anakingwa naye, na bila shaka itakuja kwa idhini ya Mwenyezi Mungu mikononi mwa waumini wakweli na inatimiza kauli yake ﷺ: «MTAWAPIGA VITA WAYAHUDI NA MTAWAUA..» Na kisha ardhi huangaza kwa ushindi wa Mwenyezi Mungu Mwenye nguvu, Mwenye uweza, Mwenye hikima...
Na mwishowe, Hizb ut-Tahrir, kiongozi ambaye watu wake hawadanganyi, inakualika kuinusuru na kufanya kazi nayo kurejesha Khilafa Rashidah tena ili Uislamu na watu wake uwe na nguvu na ukafiri na watu wake udhalilike na huo ndio ushindi mkuu; ﴿NA SIKU HIYO WATAWA FURAHIA WA