2025-07-09
Jarida la Ar-Raya:Mada Mbalimbali za Ar-Raya – Toleo la 555
Enyi Waislamu: Hawa hapa watawala wenu wamejitokeza katika uhalisia wao, na imewadhihirikia kuwa wao wana hamu na maslahi ya maadui zenu na si maslahi yenu, bali wao wako tayari kuwatoa nyinyi kama kafara kwa maadui zenu kwa ajili ya kulinda viti vyao ambavyo nguzo zake zimepinda, na Gaza ni ushahidi mzuri, na hii hapa Iran imejitokeza mbele ya macho yenu, na imetanguliwa na Somalia, Iraq, Yemen, Libya na Syria, basi mnafanya nini, na mpaka lini mtabaki kimya juu yao?!
Umefika wakati wa kuwavua hawa watawala vibaraka, na kufanya kazi na Hizb ut-Tahrir, yenye mradi wenu halisi wa kimaendeleo, ili murejeshe heshima yenu na utukufu wenu, na murejee kuwa mabwana wa dunia, na wabebaji wa mienge ya uongofu kwa watu wote.
===
Ugonjwa wa Wanamgambo
Nchini Sudan
Unaelekea Kaskazini!
Tangu siku ya Ijumaa 27/6/2025, vyombo vya habari vimekuwa vikiripoti kwamba Rais wa Eritrea, Isaias Afwerki, amekubali kuwapa mafunzo ya kijeshi ya hali ya juu wapiganaji 50,000 kutoka jimbo la Kaskazini na Mto Nile, kufuatia ombi lililotolewa na mkuu wa shirika la Kaskazini, Muhammad Sayyid Ahmed al-Jakumi, mkuu wa njia ya Kaskazini katika mkataba wa Juba wa amani ya Sudan.
Kulingana na hayo, msemaji rasmi wa Hizb ut-Tahrir katika jimbo la Sudan, Ustadhi Ibrahim Othman (Abu Khalil) alisema katika taarifa kwa waandishi wa habari: Tulisubiri hadi Jumapili, 29/6/2025, kuona majibu ya serikali na msimamo wake juu ya habari hii mbaya, lakini majibu yalitushangaza, ambapo mkuu wa shirika la Kaskazini alieleza kwa mmoja wa vyanzo vya habari; mchunguzi, kwamba jeshi na mashirika ya usalama yamejulishwa kuhusu agizo la kuwafunza majeshi haya, na alisema: "Tunafanya kazi ya kuratibu nao, na hatuwezi kuchukua hatua yoyote isipokuwa kwa idhini yao"!
Aliongeza: Tangazo hili linakuja wakati dalili za kugawanyika kwa Sudan zinaonekana, na udhibiti wa vikosi vya msaada wa haraka juu ya majimbo ya Darfur, na kuashiria kutangaza serikali sambamba, na udhibiti wa kikabila na ubaguzi juu ya hotuba ya kisiasa, na kuimarisha hisa katika mamlaka, wakati huu al-Burhan anaendelea na kauli mbiu (wanamgambo kwa kila mkoa), ambapo wanamgambo wapya wanatengenezwa kila asubuhi mpya! Kisha, hatari zaidi ya hii, mafunzo ya wanamgambo kwa wanachama wake nje ya nchi; Eritrea, na tangazo la al-Jakumi linakuja katika muktadha huu!
Ustadhi Abu Khalil alisema: Sisi katika Hizb ut-Tahrir/Jimbo la Sudan, kulingana na habari hii ya kushtua, tunasisitiza yafuatayo:
Kwanza: Tulikuwa tumeonya mara kwa mara juu ya hatari ya kuenea kwa wanamgambo wenye silaha, kwamba wao ni nyundo za kubomoa taifa, na mlango wa kumuingiza kafiri mkoloni anayetafuta kuigawanya Sudan na kuipasua kupitia ukabila na ubaguzi wa rangi, na sasa jukwaa la upuuzi linakamilika kwa kuwa kaskazini mwa Sudan nayo pia inakuwa na wanamgambo, kama majimbo mengine ya Sudan!
Pili: Uislamu umeharamisha kupigana chini ya bendera za kijahiliya na upofu, Mtume (saw) amesema: «NA YULE ANAYEPIGANA CHINI YA BENDERA YA UJAHILIYA, AKIKASIRIKA KWA AJILI YA UKABILA, AU ANAITA KWENYE UKABILA, AU ANATETEA UKABILA, AKAUAWA, BASI AMEUAWA KIUJAHILIYA».
Tatu: Mazungumzo kwamba wanamgambo hawa au wale, watakuwa chini ya uongozi wa jeshi, ni kujitupa mchanga machoni, mwanzo daima huanza hivi, kisha hutokea yasiyotarajiwa, na tunalo jeshi la msaada wa haraka kama mfano mbaya zaidi wa utengenezaji wa wanamgambo.
Nne: Serikali kwa kitendo chake hiki, inatafuta kuimarisha mpango wa mipaka ya damu, kwa utekelezaji wa Sykes-Picot mpya ya Amerika kwa ajili ya kuipasua iliyobaki ya Sudan.
Mwisho, Ustadhi Abu Khalil alisisitiza kwamba wajibu kwa jeshi ni kuanza mara moja kuunganisha vikosi vyote vya silaha vilivyoenea nchini, chini ya bendera yake pekee, ili kulifanya liwe jeshi moja lenye nguvu, na lenye uwezo wa kulazimisha mamlaka ya serikali, kisha kutoa nusra kwa Hizb ut-Tahrir ili isimamishe Khilafah Rashidah ya pili kwa njia ya Utume, na kuunganisha umma kwa misingi ya Uislamu mkuu, na kutekeleza hukumu za Kiislamu, na kung'oa ushawishi wa kafiri mkoloni kutoka nchi yetu, na kutoka nchi zote za Waislamu.
Hii ndiyo mwisho wa taarifa ya waandishi wa habari ya Ustadhi Abu Khalil, akiukumbusha jeshi la Sudan na viongozi wake kauli ya Mwenyezi Mungu: ﴿ENYI MLIOAMINI! MWITIKIENI ALLAH NA MTUME ANAPOKUITENI KWENYE YALE YANAYOKUHUMISHENI﴾.
===
Hizb ut-Tahrir/Tanzania Yazindua Kampeni Maalum
Kwa ajili ya Kuilinda na Kuitetea Aqida ya Kiislamu
Hizb ut-Tahrir/Tanzania, Ijumaa 2 Muharram 1447 Hijria, 27/6/2025 Miladia, ilizindua kampeni maalum nchini kote.
Kampeni hiyo, ambayo itaendelea kwa miezi miwili; kuanzia mwezi wa Muharram hadi Safar 1447 Hijria, inalenga kulinda na kuitetea Aqida ya Kiislamu. Kampeni hii inakuja kufuatia kuongezeka na kuenea kwa harakati potofu zinazoeneza fikra potofu mbalimbali, lengo lake la mwisho lililofichika, ni kupambana na Uislamu na kuwatia Waislamu shaka katika dini yao.
Kampeni hii inalenga:
- Kupambana na fikra ya wingi wa dini
- Kupambana na fikra ya ushirikina
- Kupambana na fikra za dini za jadi na dini za Kiafrika
- Kujenga uelewa sahihi wa Aqida ya Kiislamu kwa ujumla wake
Kampeni hiyo ina kauli mbiu: "Kataeni tofauti kati ya dini, Ukristo, ushirikina, na kuabudu masanamu, na shikamaneni na Uislamu", na kampeni itatumia mbinu mbalimbali za kujitangaza na kufikisha ujumbe wake kwa umma, ikiwa ni pamoja na:
- Majadiliano ya wazi katika majukwaa ya Kiislamu
- Majadiliano ya wazi na Wakristo na pande nyinginezo zinazoamini itikadi zinazopingana na Uislamu
- Kuandika na kusambaza makala za wazi na kwenye tovuti za mitandao ya kijamii
- Kuandika na kutuma barua za wazi kwa taasisi na jumuiya mbalimbali zisizo za Kiislamu, kufichua udhaifu wa fikra zao na kueleza uhakika wa Uislamu
- Kushiriki video kwenye tovuti za mitandao ya kijamii
- Kufaidika na majukwaa ya hotuba za Ijumaa
- Kutoa taarifa kwa vyombo vya habari
- Kuandaa maandamano
- Kutangaza vipindi vya televisheni na redio kupitia mtandao, na nyinginezo
===
Katika Upeo wa Kumbukumbu ya Hijra Tukufu ya Mtume
Enyi Waislamu: Enyi mnaoishi katika kumbukumbu ya Hijra tukufu ya Mtume, ni haki yenu huku nyinyi mnafahamu ni kwa nini tarehe ya Hijra ilikuwa tukio kubwa zaidi katika historia yenu, nalo ni kuhamishwa kwa Uislamu kutoka nadharia kwenda kwenye utekelezaji, chini ya kivuli cha dola kubwa iliyoanzishwa na Mtume ﷺ Madina, na akaitakasa rasi ya Uarabuni kutokana na ushirikina wowote kwa Mwenyezi Mungu, na akaanza akiwa amebeba ujumbe wa Uislamu kwa ulimwengu, na ilifuatiwa na Khilafah Rashidah kwa njia ya Utume, ilikuwa mfumo wa kuigwa katika utawala na usimamizi ndani na nje kwa uwepo wa wasomi wa kisiasa kutoka kwa Masahaba radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao.
Enyi Waislamu: Iwapo kweli mnataka utukufu, heshima, ushindi na ukombozi kutoka kwa ukoloni na kutoka kwa watawala wenu madikteta na kutoka kwa sheria za kimataifa za taghuti, basi hamna budi ila kufanya kivitendo yale ambayo Hijra ilikuwa kwa ajili yake, nayo ni kusimamisha dola ya Kiislamu, na Hizb ut-Tahrir imeonyesha jinsi ya kuisimamisha, basi fanyeni kazi nayo ili kuisimamisha, na kwa hili tu ndipo Hijra itakuwa na maana halisi ya kivitendo, basi hivi ndivyo inavyozaliwa dola kubwa, ambayo inapambana na nguvu za ukafiri na uadui na inakuwa mshindani mkuu ambaye ameandikiwa ushindi juu yao kwa idhini ya Mwenyezi Mungu, kama ilivyozaliwa dola kubwa iliyoanzishwa na nabii wa uongofu na rehema ﷺ, ﴿NA TUNATAKA KUWAFADHILI WALE WALIODHOOFISHWA KATIKA ARDHI NA KUWAFANYA VIONGOZI NA KUWAFANYA WARITHI﴾.
===
Uhalifu wa Mauaji Mikononi mwa Polisi
Akili ya Kibepari Inayoonyeshwa na Ukatili na Kutokujali Adhabu
Maafisa watatu wa polisi nchini Kenya wameshtakiwa kwa mauaji ya mwanablogu mwenye umri wa miaka 31, ambaye alifariki akiwa kizuizini mwezi uliopita.
Taarifa kwa vyombo vya habari kutoka kwa mwakilishi wa vyombo vya habari wa Hizb ut-Tahrir nchini Kenya, Ustadhi Shaban Muallim, ilieleza mambo yafuatayo:
Vyombo vya usalama chini ya mfumo wowote wa kilimwengu wa kiliberali, kama vile Kenya, ni muendelezo wa mfumo wa kikoloni uliotumiwa na Waingereza kudhibiti watu na kukandamiza upinzani. Katika miaka ya 1950, Wakenya walipoanza kusisitiza haki yao ya kujitawala, polisi na vyombo vingine vya usalama vya Uingereza viliwakamata makumi ya maelfu yao na zaidi ya elfu walinyongwa. Inaonekana kwamba vikosi vya polisi vinawaona watu wa kawaida kama tishio linalowezekana kwa utawala, mbinu ambayo ilitengenezwa hapo awali kulazimisha utawala wa kikoloni, na si kuwalinda.
Alisisitiza kwamba chini ya Khilafah Rashidah kwa njia ya Utume itakayosimama karibuni kwa idhini ya Mwenyezi Mungu, vikosi vya polisi vitakuwa na jukumu la kudumisha utulivu wa umma, kutekeleza sheria, na kuchunguza uhalifu. Foleni ni haramu kabisa, na afisa yeyote wa polisi atakayepatikana na hatia ya kufanya shambulio la kimwili au mateso dhidi ya mtu yeyote, Muislamu au asiye Muislamu, atawajibishwa. Kwa hivyo, vikosi vya polisi vitajitolea kikamilifu kudumisha sheria na utulivu na kwa hivyo kulinda maisha na mali ya raia.
===
Tofauti Iliyoje Kati ya Utukufu Chini ya Uislamu
Na Kati ya Udhalili Chini ya Mfumo Tabi'a
Kamati Kuu ya Mitihani ya Shahada ya Sudan ilitoa wito kwa jumuiya ya kimataifa na mashirika yanayohusika kuendelea kusaidia juhudi za Wizara ya Elimu na kuwezesha wanafunzi wote wa Sudan kufanya mitihani, haswa maeneo yaliyoathiriwa na vita, na hali ngumu ya kibinadamu. (SUNA, 26/06/2025)
Ar-Raya: Ukombozi wetu uko mikononi mwetu na si mikononi mwa maadui zetu wanaotuvizia; iwe ni wale waliotuonesha uadui, au wale wanaovaa kinyago cha unafiki kama marafiki, na vazi la "washirika" (wafadhili).
Kuhusisha masuala ya elimu; ambayo ni muhimu zaidi katika malezi na utengenezaji wa vizazi kupitia hiyo, na mashirika haya yenye shaka ni kujinyonga kisiasa, na ni maangamizi makubwa, ambayo athari zake za uharibifu kwa jamii zinaonekana mapema au baadaye.
Elimu inawakilisha nguzo muhimu katika uamsho wa Waislamu, na ili iwe hivyo, lazima kuwe na mfumo wa kisiasa unaotegemea Aqida ya Uislamu mkuu, mfumo unaojumuisha maono tofauti ya kisiasa, na ya juu, na ya kujitegemea kwa taifa lake, kuchukua ubinadamu kutoka kwenye giza la ukafiri, upotovu na ujinga, hadi kwenye nuru ya Uislamu na uadilifu wake, ambao unauletea ubinadamu katika nyanja zote za maisha; kiroho, kiakili, kimaadili, kisiasa, kiuchumi, na nyinginezo, na katika sayansi na teknolojia. Mfumo huu wa kisiasa bila shaka ni mfumo wa Khilafah Rashidah kwa njia ya Utume, ambayo inatekeleza Uislamu na mifumo yake kikamilifu, ambayo iliongoza ulimwengu kwa karne kadhaa katika ubora wa taasisi zake za kitaaluma, na uvumbuzi wake wa hali ya juu, na uvumbuzi, pamoja na mchango wake mkubwa katika maendeleo ya binadamu, basi ni umbali gani uliopo kati ya utukufu katika kivuli cha Uislamu, na udhalili katika kivuli cha mifumo tabia.
===
Inukeni Enyi Wanyoofu
Na Jueni Kwamba Mwisho Mwema Ni kwa Wachamungu
Hakika umma katika Sham haukutoa kafara na kutoa kila kitu cha thamani ili mfumo wa Bashar uzalishwe tena kwa sura ya rangi, kwa ndevu au bila ndevu, na damu ya watoto na mateso ya wakimbizi na wapiganaji, bado wanapaza sauti: Iko wapi dola mliyotuahidi?! Hakika umma bado unawatazamia wenye ikhlasi, walio thabiti juu ya misingi, ambao hawakuuza dini yao wala damu za umma wao, ambao wanakataa kusalimu amri kwa hali mbovu ya kimataifa, na wanaamini kwamba ukombozi wa kweli hauwezi kuwa ila kwa kusimamisha Khilafah Rashidah ya pili kwa njia ya Utume.
Enyi wenye ikhlasi huko Sham: Hakika mwelekeo wa mapinduzi umegeuka kwa kiwango hatari, na lazima urekebishwe kabla ya kuchelewa, na hakuna wakati wa kujuta. Na lazima kuwe na uongozi wenye akili na ikhlasi, ambao haumtii ila Mwenyezi Mungu, na hauchukui maelekezo yake ila kutoka kwa sheria yake, na hairidhiki na udhalili katika dini yake, na haachilii mbali lengo lake la kusimamisha utawala wa Kiislamu na kuangusha mifumo yote ya ukafiri, si kufanya mazungumzo nayo au kutafuta nguvu kutoka kwake. Basi hiyo hapo Hizb ut-Tahrir kiongozi ambaye hawadanganyi watu wake, fanyeni kazi naye na mpeni nusra yenu, na mumbadilishe na uongozi wa sasa ambao umeshindwa