2025-07-16
Jarida la Ar-Raya: Mada Mbalimbali za Ar-Raya – Toleo la 556
Ukandamizaji wa Waislamu kote ulimwenguni unatokana na kukosekana kwa mlinzi wa kweli wa umma wa Kiislamu, ambaye ni Khilafa. Mtume wa Mwenyezi Mungu ﷺ amesema: «Hakika Imamu ni ngao, anapiganiwa nyuma yake na watu wanajikinga kwake». Kwa hivyo, tunapaswa kuungana ili kuianzisha, bila kujali hao watawala vibaraka. Na tunapaswa kutoa wito kwa watoto waaminifu wa umma katika majeshi, ili wampe nusra chama chaaminifu katika umma huu; Hizb ut-Tahrir, ili kuianzisha Khilafa Rashidah ya pili kwa njia ya Utume.
===
India na Taasisi ya Kiyahudi
Ni Wenza Katika Uhalifu
Serikali ya Kihindu ya Modi "Hindutva" inaendelea kuongeza kiwango cha ukandamizaji na mateso dhidi ya Waislamu wa India, kuanzia kubomoa nyumba zao, hadi kuwafukuza kwa nguvu na dhuluma kutoka nchi yao. Na katika hilo, inafuata nyayo za taasisi ya Kiyahudi inayonyakua ardhi huko Palestina. Hivi karibuni, mfumo wa India umeanza kuwatendea Waislamu wa India kama wanyama, kwa kuwaita "wahamiaji haramu," na kuwafukuza mamia yao kwenda Bangladesh chini ya tishio la bunduki, na bila kuzingatia hatua zozote za kisheria "za kitaifa" au za kimataifa. Mwanamke anayeitwa Rahima Khatun alisema: "Walitutendea kama wanyama. Tuliwaambia sisi ni Wahindi, kwa nini tunaingia Bangladesh? Lakini walituelekezea bunduki na kututishia: (Ikiwa hamfuati njia nyingine, tutawapiga risasi)." Aliongeza: "Baada ya kusikia milio minne ya risasi kutoka upande wa India, tuliingiwa na hofu, tukavuka mpaka kwa miguu."
Kwa hivyo, taarifa ya vyombo vya habari kutoka Ofisi ya Habari ya Hizb ut-Tahrir katika jimbo la Bangladesh iliuliza, kwa nini serikali ya Kihindu inathubutu kufanya hivi? Jibu ni:
Kwanza: Ingawa Waislamu katika eneo hili wameungana katika dini na damu, ukoloni kafiri wa Uingereza uliwagawanya na kuwadhoofisha kwa msingi wa utaifa (Mhindi, Mbangali, Mpakistani ...), na ukaweka juu yao watawala vibaraka ambao hawawalindi Waislamu, wala hawajali hatima yao. Kwa sababu hii, mshauri wa usalama wa serikali ya mpito ya Bangladesh alisema: "Ikiwa itathibitika kuwa wao ni raia wa Bangladesh, tutawakubali", na kiongozi wa chama kikubwa zaidi cha kilimwengu nchini alisema: "Hakuna Delhi wala Rawalpindi, wala nchi nyingine yoyote, Bangladesh kwanza"! Ama wanasiasa na wasomi wa kilimwengu, wao ni wanafiki na wachukia Waislamu, kwani wananguruma kama simba dhidi ya ukandamizaji wa Wahindu huko Bangladesh, na wananong'ona kama paka waoga mbele ya ukandamizaji wa Waislamu nchini India. Mtume wa Mwenyezi Mungu ﷺ amesema: «Si katika sisi anayeita kwenye ushabiki, na si katika sisi anayepigana kwa ajili ya ushabiki, na si katika sisi anayefia katika ushabiki» Imepokewa na Abu Daud.
Pili: India ni chombo cha Marekani kafiri ya kikoloni katika eneo hilo, na mwanachama wa muungano wa kijeshi wa "Quad" katika eneo la Bahari ya Hindi na Pasifiki. Kama vile Marekani inavyotumia taasisi ya Kiyahudi katika Mashariki ya Kati kuukandamiza umma wa Kiislamu, ndivyo inavyotumia serikali ya Kihindu katika Asia ya Kusini kwa madhumuni yale yale.
Taarifa ya vyombo vya habari ilitoa wito wake kwa Waislamu ikisema: Enyi Waislamu, Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema: ﴿Na wakiomba msaada kwenu katika dini, basi ni juu yenu kuwasaidia﴾ Ikiwa Waislamu watashambuliwa popote, basi kuwasaidia ni lazima kwa Waislamu wengine. Na mmeona jinsi watawala wa kitaifa na wa kilimwengu wa Kiislamu hawawatumi majeshi kuwasaidia watu wa Palestina au Kashmir au Arakan, huku wakiwatuma chini ya bendera ya Umoja wa Mataifa na kwa amri ya Marekani kuwaua Waislamu na kumwaga damu yao!
Watawala hawa si walinzi wa umma, bali ni wasaliti wanaopanga njama dhidi yake. Mtume wa Mwenyezi Mungu ﷺ amesema: «Hakika Imamu ni ngao, anapiganiwa nyuma yake na watu wanajikinga kwake» Sahih Muslim. Na kinachowatokea Waislamu kila mahali kutokana na dhuluma ni matokeo ya kukosekana kwa mtawala wa kweli wa umma; Khalifa. Kwa hiyo, hatuna njia nyingine ila kuungana ili kuianzisha dola ya Khilafa Rashidah, badala ya kutegemea watawala hawa vibaraka. Wito wetu lazima uende kwa watoto waaminifu wa umma katika majeshi, ili wampe nusra Hizb ut-Tahrir kuianzisha Khilafa kwa njia ya Utume. Kumbukeni kuwa hii ni wajibu wenu kama Waislamu.
===
Njaa Inaenea huko Gaza
Na Nyinyi Mmechukuliwa kwa Uovu Wake Enyi Waislamu
Magharibi kafiri ya kikoloni, ikiongozwa na Marekani na taasisi ya Kiyahudi inayonyakua ardhi, pamoja na wasaidizi wao kutoka tawala zilizopo katika nchi za Waislamu, na taasisi, mashirika na vyama vya kimataifa, inajitahidi kuwaangamiza watu wa Gaza na kuwahamisha na kuwanyenyekeza kwa njia na njia mbalimbali, ikiwa ni pamoja na njaa hii inayoenea huko Gaza ambayo imetengenezwa na mikono yao na mikono ya washirika wao katika nchi za Kiislamu na ulimwengu mzima. Njaa hii haisababishwi na uhaba wa asili wa rasilimali, bali ni kwa sababu ya unyonge na uajibishaji wa watawala wa Kiislamu ambao wameweka utajiri wote wa umma mikononi mwa maadui zake wanaoudhibiti, na hawawaruhusu hata kuwapa watoto wenye njaa wa Gaza kile kinachoweza kukidhi uhai wao, na kuwaacha wanakufa kwa njaa mbele ya macho yao bila hisia wala hofu ya Mwenyezi Mungu Mtukufu, wakitekeleza maagizo ya mabwana zao makafiri wakoloni ili kulinda viti vyao vilivyopotoka na viti vyao vya enzi vya karatasi vilivyochakaa.
Kuwaokoa watu wa Gaza; watoto wao, wanawake, wazee na watu wao wote, na kukomboa ardhi iliyobarikiwa ya Palestina na nchi nyinginezo za Kiislamu zilizokaliwa hakutakuwa ila kwa kuwang'oa watawala hawa roibadhi vibaraka wasaliti wasaliti, na kumpa utawala Imamu mchungaji anayezikomboa nchi na kuwaokoa watu kutokana na dhuluma yao na udhibiti wa Magharibi juu ya utajiri wao na uwezo wao, kwa kuianzisha Khilafa Rashidah ya pili kwa njia ya Utume, ﴿Na kwa Mwenyezi Mungu wategemee waumini﴾.
===
Ziara za Kamati Kuu ya Mawasiliano ya Hizb ut-Tahrir/ Jimbo la Lebanon kwa Wabunge
Kwa mujibu wa Ofisi ya Habari ya Hizb ut-Tahrir/ Jimbo la Lebanon, ujumbe kutoka Kamati Kuu ya Mawasiliano ya chama huko, ulioundwa na Dkt. Muhammad Jabir na Mhandisi Saleh Salam, kama sehemu ya kampeni yake ya kuwatembelea wabunge, walimtembelea Mbunge Dkt. Imad Al-Hout huko Beirut. Ujumbe huo ulisisitiza mambo yafuatayo, ambayo yanahitaji msimamo na hatua kutoka kwa wabunge katika Bunge la Lebanon:
1- Umuhimu wa kupinga mradi wa utambuzi rasmi wa taasisi ya Kiyahudi, ambao unaandaliwa kwa kasi kati ya wanasiasa na vyombo vya habari kwa kisingizio cha shinikizo la Marekani, ambalo linadai ushirikiano.
2- Kwamba majeshi yatekeleze wajibu wao wa kisheria katika kutumia silaha dhidi ya adui wa umma, Wayahudi, na kwamba viongozi katika majeshi haya wanapaswa kujua kwamba ikiwa hawatatimiza hayo, silaha zao zitachukuliwa kutoka kwao au zitaharibiwa, kwa kushirikiana na tawala zao zinazotawala zilizo na uhusiano na Magharibi na zinazilinda taasisi hiyo.
3- Ni lazima kila mtu aepukane na fitna ya kimadhehebu na kile kinachoilisha au kuichochea kati ya Waislamu; kwa sababu hii inamtumikia adui tu, na inawagawa Waislamu ambao wanapaswa kukusanywa na dola moja, ambayo ni dola ya Khilafa, licha ya tofauti za kifiqhi na ijtihadi ya kisiasa kati yao.
4- Umuhimu wa kutangaza waziwazi mradi wa dola ya Kiislamu yenye kuunganisha ambayo tunabeba, ambao ni mradi wa dola ya Khilafa, na watu wote, bungeni, katika kila mkutano wa kisiasa na katika matukio yote, na Waislamu na wasio Waislamu, kama vile Hizb ut-Tahrir inavyofanya bila aibu yoyote, bali kwa furaha na bashasha yote kwa uhakika wake kwamba hiyo ndiyo suluhisho pekee kwetu na kwa wengine kutokana na hali hii ngumu.
Pia, ujumbe huo huo, wiki iliyopita, ulimtembelea Mbunge Nabil Badr huko Beirut kujadili mambo yale yale, na kuweka wabunge wa watu wa Lebanon mbele ya majukumu yao, haswa katika kuwasilisha suluhisho la msingi, na katika kuwawajibisha watawala.
===
Mahakama ya Juu ya Kenya
Inalinganisha Zinaa na Ndoa
Mahakama ya Juu ilihukumu kwamba watoto waliozaliwa kutokana na zinaa kwa wazazi Waislamu wana haki ya kurithi kutoka kwa urithi wa baba yao, ambayo inawakilisha maendeleo muhimu katika tafsiri ya sheria ya Kiislamu ya masuala ya kibinafsi nchini Kenya. Hii ilikuja baada ya Mahakama ya Juu, siku ya Jumatatu, Juni 30, kukataa rufaa iliyowasilishwa na Fatima Othman Aboud Faraj, ambaye alitaka kuwatenga watoto wa mume wake marehemu, Salim Juma Hakim Kitindo, kutoka kwa urithi wake kwa madai kwamba walizaliwa nje ya mfumo wa ndoa ya Kiislamu inayotambulika.
Katika suala hili, Mwakilishi wa Habari wa Hizb ut-Tahrir nchini Kenya, Ustadhi Shaaban Mwalimu, alisema katika taarifa ya vyombo vya habari:
Kuimarisha na kulinda "haki" za watoto waliozaliwa kutokana na zinaa ni sehemu tu ya kampeni kubwa iliyoanzishwa na mataifa makubwa ya Magharibi dhidi ya Uislamu. Dhamana za kisheria na propaganda zinafanywa katika matabaka yote ya jamii ili kuhalalisha zinaa, ambayo imesababisha kuongezeka kwa idadi ya watoto waliotelekezwa mitaani, ambayo imekuwa hatari katika vituo vya mijini.
Kinyume chake, Uislamu unawalazimisha watu wa familia na dola kutunza masuala ya watoto. Ama kwa urithi, Uislamu unatoa haki hiyo kwa watoto halali tu, huku watoto waliozaliwa kutokana na zinaa na watoto wasiojiweza, serikali ndiyo inayowajibika kwao, Mtume ﷺ amesema: «Mimi nina haki zaidi kwa waumini kuliko nafsi zao, atakayeacha mali, basi ni ya watu wake, na atakayeacha deni au kupoteza, basi ni juu yangu».
Hatimaye, tunawahimiza Waislamu kutochukulia suala hili kirahisi, kwani ni sehemu muhimu ya vita vya kimataifa dhidi ya Uislamu... Kwa hiyo, tunawaomba Waislamu wote wenye ushawishi nchini Kenya, wakiwemo wanachuoni na wanasiasa, kuinuka kutetea Uislamu.
===
Amkeni Enyi Watu wa Yemen
Waziri wa Masuala (ya Kijamii) na Kazi, Samir Baja'ala, alifanya mkutano huko Sana'a Jumapili, 2025/06/29, na kamati za maandalizi ya Mkutano wa Vyama vya Ushirika kwa Mwaka 2025, uliohudhuriwa na Naibu Waziri wa Sekta ya Maendeleo, Ali Al-Razami, na Mkurugenzi wa Ofisi ya Masuala (ya Kijamii) na Kazi katika Sekretarieti Kuu ya Mji Mkuu, Nasser Al-Kahali.
Kwa hiyo, taarifa ya vyombo vya habari iliyotolewa na Ofisi ya Habari ya Hizb ut-Tahrir/ Jimbo la Yemen ilisema: Mkutano huu unaonyesha dalili wazi isiyo na utata, kwamba wizara hii haina maono ya awali, wala mipango iliyoandaliwa tayari inayongoja utekelezaji! Bali wito wa kufanyika mkutano huu ulikuja kujibu na sanjari na maadhimisho ya kila mwaka ya Siku ya Kimataifa ya Vyama vya Ushirika inayoadhimishwa na Muungano wa Kimataifa wa Ushirika, ambayo huangukia Jumamosi ya kwanza ya Julai ya kila mwaka.
Taarifa hiyo pia iliuliza: Ni nini kinatokea, Wizara ya Ujenzi na Mabadiliko?! Je, ujenzi wenu huu unakuja kutoka Umoja wa Mataifa kwa mafuta na nyama yake?! Na mabadiliko yako wapi?! Hii bado ni tabia ya wizara zilizokutangulia kwa miongo sita, zikifadhiliwa na kuelekezwa na Umoja wa Mataifa kwa matendo yanayomkasirisha Mwenyezi Mungu na hayampendezi, na zinatoa wito kwa mawazo ambayo si ya asili ya itikadi ya Kiislamu, wala hatuna bata wala mafuta! Mnavuvia katika kiriba kilichotoboka, na uzoefu wa ushirika nchini Yemen umeshindwa, kwa sababu si wa aina ya mawazo ya Uislamu.
Taarifa hiyo ilihitimisha: Uharibifu wa watu na udhalilishaji wao unatokana na kukiuka mifumo ambayo inatumika kwao, kwa asili ya itikadi yao, bali kuipinga waziwazi. Je, vipi wale wanaokiuka amri za Mwenyezi Mungu na kufanya maasi yake, wafuasi wa kila mpiga kelele, watafanikiwa katika maisha na kufurahi?!
===
Watawala Wanagombania Madaraka
Na Wanawaruhusu Makafiri Kutunza Masuala ya Watu wao
Mapigano yamewachosha watu wa Sudan, na kuharibu miundombinu mingi nchini. Umoja wa Mataifa unasema kuwa eneo la Darfur linakabiliwa na mgogoro mkubwa, ambapo 79% ya watu wake wanahitaji misaada ya kibinadamu na ulinzi. Badala ya serikali kujaribu kukomesha fitina hizi, misiba na maangamizi, na kutangaza kusitisha mapigano haraka iwezekanavyo, inashughulika na mapigano juu ya viti vya madaraka vilivyochakaa, na haijalishi hata kuwatibu wagonjwa, wala kutoa usalama na utulivu, badala yake imegeuza nchi kuwa jukwaa la kuingiliwa kwa nchi zenye tamaa na makampuni makubwa ya ukiritimba ili kuiba utajiri wa umma. Watu wengi wa Sudan wamehamishwa, na wamekimbilia nchi jirani, baada ya wengi wao kupoteza kila kitu walichokuwa nacho, hivyo mashirika ya kimataifa na ya kikanda yanahesabu maskini na yanazungumzia njaa na ugonjwa na kumwaga machozi ya mamba, labda yatapata njia ya mabwana zao kuingilia kati katika usimamizi wa masuala ya Sudan.
Inasikitisha sana kwamba watawala wa nchi yetu wanagombania madaraka, na wanatoa fursa kwa mashirika ya ukafiri kutunza masuala yetu, kuingilia kati katika sera zetu, bali wanakubali maamuzi ambayo yanawezesha ushawishi wao katika nchi yetu, na wanatamani kukata rufaa kwa kile kinachoitwa sheria ya kimataifa, huku umma, unapokosana na ugomvi, unatamani hukumu za Kiislamu ambazo zinautoa kutoka gizani hadi kwenye nuru ya Uislamu. Je, hakupatikana katika jeshi anayemtakasia Mwenyezi Mungu, na anaitetea dini na kusimamisha sheria ya Mola wa walimwengu?!
===
Watawala wa Waislamu ni Vibarakala
Na Walinzi wa Maslahi ya Kafiri Mkoloni
Waziri wa Mambo ya Ndani wa Iraq alitoa uamuzi wa kuwaondoa vyeo maafisa watano wakuu wa usalama katika wilaya ya Tuzkhurmato, baada ya kukanyaga bendera ya Marekani wakati wa sherehe za Ashura, na picha zao zilienea katika vyombo kadhaa vya habari na mitandao ya mawasiliano.
Ar-Raya: Hatua hii inavutia sana katika pande mbili; ya kwanza: kwamba inamaanisha kujitolea kwa vyombo vya serikali kwa mbinu ya Marekani ya kunyakua zulia kutoka chini ya miguu ya Iran na wafuasi wake kutoka watu wa Iraq. Na ya pili: ni ujumbe kwao kwamba jambo hilo ni la kweli na si mzaha, na kwamba yeyote atakayejipa ujasiri wa kuipinga atapata kufuk