2025-07-30
Jarida la Al-Raya: Mada Mbalimbali za Al-Raya – Toleo la 558
Ni wajibu kwa jeshi la Sudan kuanza mara moja kuunganisha nguvu zote za silaha zilizosambaa nchini, chini ya bendera yake pekee, ili kuifanya kuwa nguvu moja imara, yenye uwezo wa kulazimisha mamlaka ya dola, kisha kulisaidia Hizb ut-Tahrir kusimamisha Khilafah Rashidah ya pili kwa mujibu wa manhaj ya utume, na kuunganisha umma kwa msingi wa Uislamu mkuu, na kutekeleza hukumu za Kiislamu, na kung'oa ushawishi wa kafiri mkoloni kutoka nchi yetu, na kutoka nchi zote za Waislamu.
===
Matumaini hayazaliwi
Katika ulimwengu wa batili
Hakika matumaini, katika historia yote ya wanadamu, hayazaliwi katika ulimwengu wa batili, wala udanganyifu, uongo na upotoshaji, bali matumaini huzaliwa daima pamoja na haki, ukweli na uaminifu, huletwa na manabii walio tumwa kutoka kwa Mwenyezi Mungu, na akahitimisha nao Bwana wetu Muhammad ﷺ kwa ujumbe wa Uislamu mkuu, unaobeba maelezo ya kutosha katika itikadi, na mifumo ya maisha katika utawala, uchumi, jamii, sera ya elimu, na sera ya kigeni, Waislamu wenye mamlaka, au wawakilishi wao kutoka kwa watu wa nguvu na ulinzi, wanafanya katika mfumo huu bai'a kwa mtu kutoka miongoni mwao, Khalifa wa Waislamu, na hapo mfumo wa Khilafah unasimama, na matumaini huzaliwa katika maisha ya heshima chini ya Uislamu, kwa yafuatayo:
Kwanza: Khalifa atafunga ukurasa wa mwisho wa maisha ya Waislamu kwa mifumo ya kidunia iliyoletwa, yeye na wataalamu wa utekelezaji wake kutoka Magharibi kafiri, na ataanza kutekeleza mifumo ya Kiislamu, iliyochukuliwa kutoka kwa wahyi kwa nguvu ya dalili.
Pili: Khalifa ataanza mara moja kuwateua wasaidizi, magavana na viongozi wengine, au wale anaowaomba msaada, na ataanza mara moja kutatua matatizo ya raia, mbali na mgao wowote, kwa sababu mamlaka kisheria ni ya umma, sio kwa yule anayebeba silaha na kushauriana na nje.
Tatu: Khalifa wa Waislamu ataondoa ushawishi wa Magharibi kafiri kutoka nchi yetu, na atatakasa taasisi za dola kutoka kwa vyombo vyake, na atachukua utajiri wa fikra za umma, na utajiri wake wa mali, kama ngazi ya kupanda ili kuwa dola ya kwanza ulimwenguni kama ilivyokuwa hapo awali, na kwa miaka mia sita iliyopita.
Nne: Uislamu ambao unatekelezwa na Khalifa wa Waislamu, utatakasa mazingira ya kisiasa kutoka kwa vibaraka na vyombo vya Magharibi kafiri mkoloni, na kutoka kwa hotuba ya ubaguzi wa rangi, na madai ya kijahili ambayo yanawagawa raia wa dola, na hapo wazo la kuwahudumia raia wote kwa haki na ihsani litatosha kuvunja madai ya ubaguzi na istilahi zingine ambazo zimezaliwa kuishi chini ya mifumo ya Magharibi kafiri.
Tano: Khalifa wa Waislamu atafanya nguvu za silaha katika dola kuwa nguvu moja, inayoongozwa na Khalifa wa Waislamu, na atasimamisha uundaji usio na maana wa wanamgambo wapya kila asubuhi mpya, bali na mbaya zaidi, kwamba baadhi yao wanafundishwa katika nchi za nje! Kisha tunatamani matumaini na maisha ya heshima, chini ya vivuli vya nguvu hizi nyingi za silaha!
Hii ni tone kutoka bahari ya hukumu za Kiislamu, tunapozitoa kama mradi kwa umma ambao unaweza kupeleka matumaini katika maisha ya heshima, na siku itakapowekwa katika utekelezaji, maisha yetu yatageuka chini juu, na matumaini yatafuata kazi ambayo inatupeleka kwenye kilele cha utukufu kama tulivyokuwa hapo awali, na hilo si gumu kwa Mwenyezi Mungu.
===
Je, kuna usaliti mkuu kuliko kufanya hatima ya watu wa Gaza
itegemee maamuzi ya Trump na Netanyahu?!
Enyi Waislamu: Je, mmeridhika kuwaona watoto wa Gaza wanakufa kifo cha polepole mbele ya macho ya baba zao na mama zao huku wakiwa hawana uwezo wa kufanya chochote isipokuwa kumwaga machozi na kumeza majuto?!
Je, nafsi zenu zimefurahishwa na matukio ya mauaji na ukatili?! Au je, usaliti wa watawala wenu ambao wamefanya hatima yenu na hatima ya umma wenu kuwa mikononi mwa Marekani na Wayahudi umewapendeza?!
Na je, kuna udhalilishaji mkuu kuliko kuwaacha watu wenu na ndugu zenu wachinjwe, wafe kwa njaa na kiu huku mna uwezo wa kuwasaidia?!
Enyi wana wa umma bora uliotolewa kwa watu: Msemeshe Mwenyezi Mungu kwa ukweli katika imani yenu, msemeshe Mwenyezi Mungu kwa ukweli katika msaada wenu, msemeshe Mwenyezi Mungu kwa ukweli katika msimamo wenu, kwa sababu mnafahamu kwamba hakuna njia ya kusimamisha dini yenu, na kuwasaidia ndugu zenu huko Gaza na Palestina yote, na kukomboa msikiti wenu wa Al-Aqsa, isipokuwa kwa kuangusha viti vya enzi vya watawala wenu waoga vibaraka na kuvunja mipaka na kuelekea kwenye ardhi iliyobarikiwa ya Palestina.
Kwa hiyo, hakuna chaguo lililosalia kwa umma wa Kiislamu isipokuwa kujizatiti na kuhamasisha majeshi yake, na kuangusha viti vya enzi ambavyo vinaiweka Gaza katika njaa pamoja na Wayahudi na Marekani, hakuna kilichosalia kwa umma wa Kiislamu isipokuwa kuitikia wito wa Mwenyezi Mungu: ﴿Enyi mlio amini! Mna nini mnapoambiwa: Tokeni kwenda kupigana katika Njia ya Mwenyezi Mungu, mnaelekea nchi kwa uzito? Kwani mmeridhika na maisha ya dunia badala ya Akhera? Lakini starehe ya maisha ya dunia ni ndogo ukilinganisha na Akhera. * Msipotoka kwenda kupigana atakuadhibuni adhabu chungu, na atawaleta watu wengine badala yenu, wala hamtamdhuru kitu. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye uweza wa kila kitu﴾.
===
Hizb ut-Tahrir/ Wilaya ya Uturuki
Msafara wa halaiki kuinusuru Gaza
Tangu vita vya kimbunga cha Al-Aqsa mnamo Oktoba 7, 2023 BK, shirika la Kiyahudi linalovamia linaendelea na uhalifu wa mauaji ya halaiki, na hivyo kukiuka sheria za vita na sheria zingine zote, na licha ya wito ambao tumekuwa tukitoa mara kwa mara "Majseshi kuelekea Al-Aqsa" na "Muhammadçik kuelekea Gaza", ambazo zinawahutubia viongozi kuchukua hatua madhubuti, na kutokana na ukimya wa watawala ambao majeshi chini ya uongozi wao yanangoja, shirika la Kiyahudi linaendelea kufanya uhalifu wa mauaji ya halaiki. Wakati umma unawaita watawala wake "kuhamasisha majeshi kuinusuru Gaza", wanaendelea kuikabidhi na kuifanya Gaza itumike kwa Wayahudi wauaji na wale wanaowaunga mkono kwa fedha na silaha; Marekani, Magharibi na mfumo wa kimataifa.
Kwa hiyo, Hizb ut-Tahrir/ Wilaya ya Uturuki iliratibu Jumapili, 02 Safar Al-Khair 1447 Hijria, sawia na Julai 27, 2025 BK, licha ya marufuku ya serikali ya Uturuki, msafara mkubwa wa halaiki katika ngazi ya Uturuki, wenye kichwa:
"Tunakwenda kwenye Ikulu ya Rais kwa ajili ya Gaza:
Je, mko tayari kuzungumza nasi na mwenye mamlaka?"!
Ambapo msafara ulianza kutoka makao makuu ya chama tawala cha Haki na Maendeleo huko Ankara kuelekea Ikulu ya Rais "kuzungumza na anayehusika" kwa niaba ya Waislamu huko Gaza ambao wameachwa peke yao chini ya uzito wa mauaji, kuzingirwa na njaa kwa takriban miaka miwili.
Kwa upande mwingine, serikali ya Uturuki inayoongozwa na Erdogan au serikali yoyote ya Kiarabu katika eneo hilo, haijachukua hatua zozote madhubuti za kusitisha uvamizi na mauaji ya halaiki huko Gaza, na haijafanya kazi hata kuhakikisha usafirishaji wa misaada ya kibinadamu kwa Gaza, hivyo vifo vya halaiki vimeanza kutokana na njaa na kiu.
===
Miongoni mwa sababu za kuangamia kwa mataifa
Ni kuwatii mabwana na viongozi wakuu katika upotevu wao
Enyi watu wa Misri ya Kinana! Hakika miongoni mwa sababu za kuangamia kwa mataifa ni kuwatii mabwana na viongozi wakuu katika upotevu wao na kutowashika mikono na kuwarejesha kwenye njia ya haki na usawa, na ujasiri wa watawala wenu dhidi ya Mwenyezi Mungu na kuendelea kwao katika kuwadhalilisha nyinyi ni matokeo ya ulegevu wenu, ukimya wenu na kunyamaza kwenu, hivyo ukatili wao unaongezeka kila inapokua ndani yenu ukuta wa hofu ambao wanautengeneza kwa mauaji, kupondwa, kufungwa, na vitisho, na lau wangeona msimamo kutoka kwenu dhidi yao kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, mkikasirika kwa yale aliyoyaharamisha yanavunjwa, hawangezidi katika upotevu wao na hawangeendelea katika ukatili wao kwenu, na watu wana nguvu zaidi kuliko watawala na majeshi yao, haijalishi mamlaka yao inafikia wapi, jeshi ni sehemu ya watu, halitengani nao, wao ni ndugu zenu, watoto wenu na familia zenu, na juu ya hayo, miisho yenu na riziki yenu iko mikononi mwa Mwenyezi Mungu pekee, hivyo mfumo na vibaraka wake hawamiliki kuwazuia riziki wala kuwapa, wala kuwanyima maisha yenu ambayo Mwenyezi Mungu ameyafanya kuwa mikononi mwake, hivyo kifo hakimtishi mja ambaye ameiuza nafsi yake kwa Mwenyezi Mungu kwa bei nafuu, bali itakuwa njia ya neema ya kudumu Peponi.
Kwa ajili hiyo enyi watu wa Kinana na kwa ajili ya neema ya utukufu wa dunia na neema ya kudumu Akhera, ziwepo nia zenu na msemesheni Mwenyezi Mungu Azza wa Jalla kwa ukweli na washikeni mikono watawala wenu, na waombeeni watoto wenu katika majeshi wakate kamba zote zinazowaunganisha na Magharibi na vibaraka wake na waunganishe kamba zao na wakweli wanaounganisha usiku wao na mchana wao ili isimamishwe ndani yenu na kwa ajili yenu na kupitia nyinyi Khilafah kwa mujibu wa manhaj ya utume; ndugu zenu katika Hizb ut-Tahrir, kwa sababu kupitia wao na yale wanayobeba kuna ukombozi wenu na ukombozi wa umma wenu kutoka katika yale ambayo unaelea na kurudi kwake kuwa bibi wa dunia kama ilivyokuwa.
===
«KILA MMOJA WENU NI MCHUNGAJI NA KILA MMOJA WENU ATAULIZWA KUHUSU UCHUNGAJI WAKE»
Enyi Waislamu: Mtume wa Mwenyezi Mungu ﷺ anasema: «KILA MMOJA WENU NI MCHUNGAJI NA KILA MMOJA WENU ATAULIZWA KUHUSU UCHUNGAJI WAKE; KIONGOZI ALIYE JUU YA WATU NI MCHUNGAJI NA ATAULIZWA KUHUSU UCHUNGAJI WAKE...», wamekubaliana. Na kutoka kwa Mama wa Waumini Aisha, Mwenyezi Mungu awe radhi naye, amesema: Nimemsikia Mtume wa Mwenyezi Mungu ﷺ akisema katika nyumba yangu hii: «EWE ALLAH, YOYOTE ANAYESHIKILIA JUKUMU LOLOTE KATI YA MAMBO YA UMMATI WANGU AKAWASHINDA, BASI MSHINDE, NA YOYOTE ANAYESHIKILIA JUKUMU LOLOTE KATI YA MAMBO YA UMMATI WANGU AKAWALAINISHA, BASI MLAINISHE», amesimulia Muslim, na hii ni dua kutoka kwa Mtume ﷺ kwa yule anayeshughulikia mambo ya Waislamu ya kibinafsi na ya umma, na kwamba kulainisha ni kuendesha watu kulingana na amri ya Mwenyezi Mungu na Mtume wake, na yeyote anayewaendesha watu bila mwongozo wa Muhammad ﷺ basi amewashinda.
Kwa hiyo, uongozi na kuwahudumia watu ni mzigo mzito na amana ambayo Mwenyezi Mungu atauliza, hivi ndivyo ilivyokuwa jibu la Mtume wa Mwenyezi Mungu ﷺ katika yale aliyosimulia Abu Dharr: Nikasema: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, je, huniteui? Akasema: Akapiga kwa mkono wake kwenye bega langu, kisha akasema: «EWE ABU DHARR, WEWE NI DHAIFU, NA HII NI AMANA, NA HII SIKU YA KIYAMA NI MADHARAU NA MAJUTO, ILA YULE ANAYEICHUKUA KWA HAKI YAKE, NA AKATIMIZA YALE ALIYOWAJIBIKA NAYO» amesimulia Muslim.
Juu ya hayo, tiba ya majanga yanayowapata Waislamu haitakuwa kwa maombolezo na kupiga mashavu, huku msingi wa ugonjwa na msingi wa balaa ukiendelea kuwepo, ambayo ni mifumo mibovu, matokeo ya asili ya matatizo haya, bali tiba itakuwa kwa kufanya kazi kwa bidii kuiondoa, na kusimamisha mfumo unaotawala kwa sheria ya Mwenyezi Mungu na kuhudumia maslahi ya watu kulingana na hukumu zake, na kumfanyia bai'a imamu mwadilifu anayepiga kwa mkono wa chuma aina zote za ufisadi, akikausha vyanzo vyake na kukata mizizi yake, lengo lake katika hayo yote ni radhi ya Mwenyezi Mungu.
===
﴿ENYI MLIO AMINI! ITIKIENI WITO WA MWENYEZI MUNGU NA MTUME ANAPOKUITENI KWENYE YALE YANAYOKUHUISHENI﴾
Enyi Waislamu: Nyinyi pekee kwa itikadi yenu na sheria ya Mola wenu mna uwezo wa kuwalisha watu na kutosheleza njaa yao na kuondoa haja yao na umaskini wao, na yale ambayo ulimwengu na wafuasi wake wanawaahidi si chochote ila udanganyifu, hivyo endeni katika njia yenu mpaka itimie mikononi mwenu ahadi ya Mwenyezi Mungu ambayo inawakasirisha makafiri na kuponya vifua vya waumini wenye subira, na iwe ndani yenu Khilafah kwa mujibu wa manhaj ya utume inayowasahihisha hawa waliopotoka wasiwasi wa shetani na inawafahamisha watu wote Uislamu ni nini katika sura yake halisi wanapoiona kama hali halisi ya utendaji inayotekelezwa katika dola inayosimamisha na kuitekeleza na kuichunga na kuibeba kwa ulimwengu kwa da'wa na jihad, mbali na utawala wa watawala wasaliti na madai ya elimu vibaraka, hivyo watu wanaingia katika dini ya Mwenyezi Mungu kwa wingi na Mwenyezi Mungu anawaandikia furaha na mafanikio.
Hivyo msihuzunike kwa yale wanayoyafanya enyi Waislamu, kwa sababu wao ni kama yule anayejaribu kuzuia mwanga wa jua kwa mkono wake au kuzima nuru yake kwa kuipulizia, na hawatafikia lengo lao la hila zao na vitimbi vyao, kwa sababu hila zao zinaondoka na vitimbi vyao vinaelekea kuangamia, kwa sababu Mola wao na mlinzi wao na kibla chao kiko Magharibi na Mola wenu na msaidizi wenu ni Mwenyezi Mungu na Yeye ndiye Mola bora na msaidizi bora, na amewaahidi ushindi na Mwenyezi Mungu havunji ahadi yake, hivyo jizatiti na ombeni yale aliyowaahidi na nyoosheni na karibieni na lindasheni na mcheni Mwenyezi Mungu na msimwangalie yule anayeanguka njiani na msifanye haraka na ushindi, hauzuii ushindi isipokuwa Mwenyezi Mungu mpaka safu zitenganishwe na barakoa zianguke kutoka kwa wanafiki na wanafiki na wasaliti wazihirike hivyo ushindi wa Mwenyezi Mungu uteremke na mwe na utukufu katika dunia na akhera, na mtakumbuka yale ninayowaambia na namkabidhi Mwenyezi Mungu jambo langu.
===
Enyi watu wa Misri ya Kinana
Tahadhari isije ikawafika desturi ya uingizwaji
Enyi watu wa Kinana! Ukombozi wenu pekee unaolinda heshima yenu na kurejesha haki zenu na ambao unawahakikishia uadilifu, usalama na huduma kwa njia sahihi ni kusimamishwa ndani yenu Khilafah kwa mujibu wa manhaj ya utume.
Na huyo hapo Hizb ut-Tahrir hivyo fanyeni haraka kufanya kazi pamoja naye na mkishwe kile kilichosalia cha utajiri wenu, kishieni heshima yenu ambayo inadhalilishwa usiku na mchana kwenye foleni za mikate na zinginezo, kishieni wanawake wenu na familia zenu, kishieni vizazi vyenu na msiwarithishe utegemezi huu ambao umelemaza mabega yenu, kishieni kwa kusimamisha kwa ajili yao dola inayowalisha, kuwapa makazi, ku