2025-09-24
Gazeti la Ar-Raya: Mada Mbalimbali za Ar-Raya – Toleo la 566
Enyi Waislamu: Umefika wakati wa kukaza mambo yenu na kufanya uamuzi wenu wenyewe mbali na hao watawala mafidhuli, ambao wamewekwa na kafiri mkoloni juu ya shingo zenu, hawawaheshimu ila na ahadi, wala hawajali masuala yenu, wala kuhifadhi maslahi yenu, na imewalazimu kuwavua, na kumweka bay'ah khalifa atakayewahukumu kwa kitabu cha Mwenyezi Mungu na sunna za Mtume wake, na aendeshe majeshi kuwanusuru Waislamu, na kuwarejeshea heshima yenu na hadhi yenu, na hamna mbele yenu ila Hizb ut-Tahrir, mwenye mradi wa uamsho wenu kwa msingi wa Uislamu, basi msaidieni Mwenyezi Mungu ili akusaidieni na athibitishe nyayo zenu.
===
Taasisi ya Kiyahudi na Wanaoiunga mkono
Ndio Tatizo la Ulimwengu
Vyombo vya habari viliripoti kauli ya Rais wa Marekani Donald Trump kuhusu Gaza, ambayo anasema: "Gaza ni tatizo kubwa kwa (Israel) na Mashariki ya Kati". Na hatukumsikia yeyote kati ya watawala mafidhuli katika nchi za Waislamu akijibu maneno yake, na kumwambia: Kwamba taasisi ya Kiyahudi inayokalia ardhi kwa mabavu ndio tatizo kubwa katika nchi za Waislamu, na nyinyi ndio mnaoipa vifaa vya kivita na msaada wa kisiasa na kiuchumi; kwa hivyo nyinyi ndio tatizo kubwa katika ulimwengu mzima, kwa sababu itikadi yenu ya kibepari ndio sababu ya dhiki ya ulimwengu, na nyinyi ndio sababu ya kuzigawa nchi za Waislamu katika nchi dhaifu na taasisi bandia zinazowategemea.
Haya yalikuja katika taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa na ofisi ya habari kuu ya Hizb ut-Tahrir, na taarifa hiyo iliongeza: Rais huyu jeuri hangeweza kutoa kauli kama hiyo lau angempata mtu mmoja tu katika watawala wa Waislamu akijibu kauli yake, na aendeshe majeshi kuiondoa taasisi ya Kiyahudi iliyoharibika, na kumrudisha huyu anayefumbia macho ukweli katika akili yake na usawa wake, na kwamba taasisi ya Kiyahudi ndio iliyokalia ardhi iliyobarikiwa, na ndio inayowatesa watu wake vibaya, bali imefikia hatua ya kiburi kwa nchi jirani na za mbali pia.
Na ikaendelea: Tatizo la nchi za Kiislamu lilianza tangu kubomolewa kwa dola la Khilafah mwaka 1924 BK, na kugawanywa kwake katika nchi ndogo na dhaifu, zinazodhibitiwa na makafiri wakoloni, kisha kukafuata kukaliwa kwa mabavu kwa Palestina na kuanzishwa kwa taasisi ya Kiyahudi iliyoharibika humo, kwa msaada wa Uingereza, kisha uangalizi wa Amerika, na usaliti wa watawala wa Waislamu, ambao waliimarisha taasisi ya Kiyahudi, kisha wakaikinga na kuwazuia Waislamu wasiikomboe Palestina, ndio hali ya watawala mafidhuli katika nchi zetu; baadhi yao wanaikinga taasisi ya Kiyahudi, na baadhi yao wamefanya nayo makubaliano na kubadilishana uhusiano wa kidiplomasia hadharani, na baadhi yao wameanzisha nayo uhusiano kwa siri, na baadhi yao wanailalamikia kwa Baraza la Usalama inapoishambulia ardhi yake na uhuru wake kwa ndege zake, na baadhi yao wanakemea mapambano ya Waislamu dhidi yake huko Palestina, na baadhi yao wanashiriki kuwazunguka watu wa Gaza, na baadhi yao wameingia katika makubaliano ya Ibrahimu, na wote wanazifunga majeshi katika kambi zao na wanayazuia kuikomboa Palestina, na wanawazuia watu wao hata wasieleze kukataa kwao mauaji ya halaiki katika Ukanda wa Gaza, hakika ni uovu ulioje wanaoufanya!
Na taarifa kwa vyombo vya habari ilihitimisha kwa kusema: Na sisi katika ofisi kuu ya habari ya Hizb ut-Tahrir tunampongeza Trump na viongozi wa taasisi ya Kiyahudi iliyoharibika, kwamba hali hii haitaendelea, na mmeyaona mabadiliko katika maoni ya umma wa kimataifa kuhusu uhalifu wa taasisi ya Kiyahudi huko Gaza, na umma wa Kiislamu umeelewa suala lake, na unaenda kwa hatua za haraka kuelekea kuanzisha dola yake, dola ya Khilafah ambayo inajaza mioyo yenu hofu na uoga, na wakati huo hamtasikia jibu kutoka kwa khalifa wa Waislamu; bali mtaona majeshi makubwa ambayo mwanzo wake uko kwenu na mwisho wake uko kwake, na Hizb ut-Tahrir unaongoza umma kwa hatua za haraka kufikia lengo hili, basi furahieni kwa yale ambayo yanawaudhi, na hakika kesho inamngojea anayeingojea.
===
Hizb ut-Tahrir/ Wilaya ya Sudan
Watekeleza Msimamo Mashariki ya Nile
Vijana wa Hizb ut-Tahrir/ Wilaya ya Sudan mashariki ya Nile siku ya Jumatano 25 Rabi'ul Awwal 1447 Hijria sawa na 17 Septemba 2025 BK baada ya swala ya adhuhuri, katika msikiti mkubwa katika soko la sita Al-Wahda, walifanya msimamo ambao ndani yake kulikuwa na mabango yanayowataka Waislamu kusimama kwa nguvu, kuzuia mpango wa kuigawa Sudan kwa kuitenga Darfur.
Na katika msimamo ilisomwa hotuba iliyowataka Waislamu kutekeleza wajibu wao, wa kuzuia mpango huo, na msimamo ulikumbana na maingiliano kutoka kwa hadhira iliyokuwepo, ambapo idadi yao walisimama kusikiliza hotuba.
===
Wasaidieni Watu wa Gaza
Kabla Mayahudi Hawajawafutilia Mbali Kabisa
Taasisi ya Kiyahudi inaendeleza vita vya mauaji ya halaiki dhidi ya Ukanda wa Gaza ikilenga kwa mashambulizi ya anga na makombora makali sehemu mbalimbali za Ukanda huo, ambayo husababisha vifo vya makumi ya mashahidi na majeruhi kila siku. Na kwa wiki chache, inazidisha mashambulizi yake dhidi ya mji wa Gaza ulijaa watu wake na wakimbizi kutoka kaskazini mwa Ukanda huo, ikiwa inajiandaa kuukalia tena, ambapo inalenga shule na vituo vya makazi, na inafanya operesheni kubwa za kulipua nyumba za makazi nzima, na kuharibu majengo ya makazi ikifuatiisha kwa kuwapa watu maonyo ya ulazima wa kuondoka kuelekea kusini mwa Ukanda huo.
Enyi Waislamu: Mayahudi wamezidi katika uovu wao na wanaendelea katika kutekeleza mipango yao ya kuwaua idadi kubwa ya watu wa Gaza na kuwahamisha wale waliosalia kati yao, ili waendelee katika kufanikisha ndoto zao za kitorati za kuanzisha dola yao kutoka Nile hadi Frati kama viongozi wao wanavyotangaza kwa ujasiri wote, nao wanaitegemea Amerika na rais wake mhalifu jeuri Trump, bali ukatili wao na uhalifu wao umevuka ardhi iliyobarikiwa hadi kufikia Syria, Lebanon, Yemen, Iran na Qatar, na kamba inaendelea kubururwa, nao katika uhalifu wao huu wanategemea usaliti na njama za watawala wenu haswa watawala wa nchi zinazowazunguka ambao wanawaikinga na wanawabana watu wa Gaza na wanazuia harakati yoyote ya kuwanusuru, basi hadi lini kukaa kimya huku dhidi ya watawala hawa wasaliti wahalifu?! Je, haujafika wakati wa kuhamasisha wivu, hamasa na ujasiri katika mioyo na akili za watiifu katika majeshi ya Waislamu?! Je, hamuwahisi ndugu zenu kabla hawajafutiliwa mbali kabisa?! Je, hamuwaokoi na kujiokoa kabla haijawashukia hasira ya Mwenyezi Mungu na adhabu yake kutokana na ukimya huu na udhalilishaji?! Mwenyezi Mungu anasema: ﴿NA MKIGEUKA YEYE ATALETA WATU WENGINE WASIO KUWA NYINYI, KISHA HAWATAKUWA MFANO WENU﴾.
===
Hizb ut-Tahrir/ Wilaya ya Sudan
Yakutana na Sheikh Farouk Al-Hajj Abdullah Sheikh Dafa Allah
Jumanne 2025/9/16 ujumbe wa kamati ya mawasiliano kuu ya Hizb ut-Tahrir katika wilaya ya Sudan, kwa kushiriki kwa Ustadh Abdullah Hussein mratibu wa kamati, na Sheikh Abdul Qadir Abdul Rahman mwanachama wa Hizb, walikutana na Sheikh Farouk Al-Hajj Abdullah Sheikh Dafa Allah, katibu wa uaminifu wa Da'wah na Utamaduni wa kabila la Al-Kalaklat.
Mkutano huo ulizungumzia mpango wa nchi za Magharibi kwa ujumla, na haswa Amerika, katika juhudi za kugawanya lililogawanyika katika Sykes-Picot mpya na mipaka ya damu, na huu ndio mpango wake nchini Sudan baada ya kuitenga kusini kwake, inataka kuitenga Darfur, na kinachotakiwa kutoka kwa watu wote wa nchi ni kufanya kazi ya kushindwa mpango huu, haswa wanazuoni ambao wana ulazima wa kusema ukweli, na kuwafahamisha watu kuhusu mpango huu na ulazima wa kufanya kazi kwa ajili ya umoja wa nchi, bali na kufanya kazi ya kuziunganisha nchi za Waislamu kwa ujumla kwa kumpa bay'ah khalifa wa Waislamu.
Sheikh Farouk Al-Hajj Abdullah alilishukuru ujumbe huo kwa ziara hii akisema, Mwenyezi Mungu abariki juhudi na jitihada za Hizb ut-Tahrir, na alimrehemu Sheikh Ali Saeed msemaji mkuu wa zamani wa Hizb, na alisisitiza mawasiliano na ushirikiano katika yale yanayoboresha hali ya umma, na alitupatia maono ya uaminifu wa Da'wah na Utamaduni kwa ajili ya kuyasoma na kuyajibu.
===
Watoto wa Gaza wenye Ulemavu
Ndio Waathirika Zaidi wa Vita Wanateseka
Vita vya maafa vinavyoendelea huko Gaza tangu tarehe saba ya Oktoba 2023 vimeathiri nyanja zote za maisha humo, za watu, miti, mawe na rasilimali, na kifo na uharibifu vimeenea kila mahali.
Na kwa mujibu wa kile ambacho kamati teule ya Umoja wa Mataifa iliripoti hivi karibuni kwamba iliarifiwa kuwa watu 157,114 kati ya tarehe saba ya Oktoba 2023 na tarehe 21 Agosti mwaka huu wamepata majeraha, 25% kati yao wanakabiliwa na hatari ya kupata ulemavu ambao utaendelea maisha yao yote. Na ilitangaza kuwa takriban watoto 40,500 walipata majeraha yanayohusiana na vita katika kipindi cha miaka miwili ambayo imepita tangu kuzuka kwa vita, na kwamba zaidi ya nusu yao wanasumbuliwa na ulemavu. Hivyo basi zaidi ya watoto 21,000 huko Gaza wamekuwa wenye ulemavu!!
Idara ya wanawake katika ofisi kuu ya habari ya Hizb ut-Tahrir ilisema katika taarifa kwa vyombo vya habari: Yote haya na zaidi yanatendeka mbele ya masikio na macho ya ulimwengu mzima na taasisi na mashirika yake ambayo yanadai ubinadamu na haki, na haizidi kile wanachokifanya maandamano ya kimaumbo hapa, au kuwasilisha ripoti kule, au kujaribu kuingiza misaada ambayo haitoshelezi na haiondoi njaa! Na watawala wa Waislamu wamejishughulisha na kuhifadhi viti vyao na viti vya enzi vyao juu ya vipande vya miili na damu za Waislamu na mateso yao haswa huko Gaza, wamesahau wameghafilika na kauli yake ﷺ: «HAJALINDA MTU MUSLIMU KATIKA MAHALI AMBAO UTAKIIUKWA UTUKUFU WAKE NA KUPUNGUNZWA HESHIMA YAKE ILA MWENYEZI MUNGU ATAMTOSA KATIKA MAHALI ANAPOPENDA USHINDI WAKE NA HAJAMSIDIA MTU MUSLIMU KATIKA MAHALI AMBAO UTAPUNGUNZWA UTUKUFU WAKE NA KUTOSWA HESHIMA YAKE ILA MWENYEZI MUNGU ATAMSIDIA KATIKA MAHALI ANAPOPENDA USHINDI WAKE», na hakika siku ya kulipiza kisasi kutoka kwao inakaribia kwa idhini yake Mwenyezi Mungu.
===
Amerika Inasisitiza Kuondoa Mapinduzi Kutoka Yaliyomo Yake
Na Kuiimarisha Mfumo wa Kisekula nchini Syria
Mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa nchini Syria Geir Pedersen, siku ya Jumamosi 9/6 katika Damascus, alikutana na Waziri wa Mambo ya Nje katika Serikali ya Mpito nchini Syria Asaad Al-Shaibani, na alijadili naye mchakato wa mpito wa kisiasa nchini humo na mwelekeo wake wa kikanda na kimataifa.
Pia mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa alisisitiza kwamba Umoja wa Mataifa utaendelea kuunga mkono serikali na watu wa Syria ili kufikia amani na utulivu wa kudumu, kupitia mchakato wa mpito wa kisiasa jumuishi, wa uwazi na wa kuaminika, kwa mujibu wa azimio la Baraza la Usalama nambari 2254 la mwaka 2015. (Shirika la Habari la Hawar)
Ar-Raya: Hakika huyu muovu Pedersen alijitahidi sana katika miaka ya hivi karibuni ya mapinduzi kuokoa serikali katili na kuihuisha na kutekeleza suluhisho la kisiasa la Amerika, lakini kwa fadhila za Mwenyezi Mungu kisha kwa bidii ya wakweli kutoka kwa wana wa mapinduzi alikatishwa tamaa na alishindwa katika makusudio yake, na watu wa mapinduzi waliweza kumuondoa Bashar licha ya Amerika na washirika wake.
Na leo Pedersen anarudi tena kugonga milango iliyofungwa na anatumia vibaya udhaifu wa utawala mpya, na kujisalimisha kwake kwa Amerika na kutekeleza mipango yake kwa kuiacha mfumo wa kisekula ukiendelea kutumika nchini Syria, na kuijenga upya jeshi na usalama ili kulinda maslahi ya Amerika, na ili Syria iendelee kuwa koloni la kisiasa la Amerika, na chini ya mfumo wa kimataifa.
Kwa hivyo ni lazima kwa watu wetu waasi katika Sham kuwa waangalifu na hila zinazowazunguka, na watambue kwamba hakuna ukombozi kwao ila kwa kutumia sheria ya Mwenyezi Mungu na kukamilisha mapinduzi kwa utawala wa Uislamu katika dola ya Khilafah Rashidah ya pili kwa njia ya Utume, na katika hilo kuna utukufu wa dunia na neema ya akhera kwa idhini ya Mwenyezi Mungu.
===
Uislamu Bila Mengineyo
Unaweza Kuwachanganya Watu Katika Umma Mmoja
Hakika Uislamu mkuu ndio pekee katika historia ya mwanadamu ambao ulichanganya watu, rangi na makabila tofauti katika umma mmoja, haukuwa umefungwa katika Madina bali ulienea katika kisiwa chote na yalifanyika mapinduzi ya Kiislamu kwa ajili ya kueneza Uislamu, hivyo Waislamu waliifungua Iraq, na ilikuwa inakaliwa na Wakristo, Wamazdakia na Wazoroasta kutoka kwa Waarabu na Waajemi, na waliifungua Uajemi na ilikuwa inakaliwa na Wajemi, Mayahudi na Warumi, na waliifungua Sham na ilikuwa mkoa wa Kirumi unaokaliwa na Wasiria, Waarmenia, Warumi na Waarabu, na waliifungua Afrika Kaskazini ambapo kuna Waberber, na waliifungua Sindh, Khwarazm, Samarkand na Andalusia, na wakawachanganya watu hao wote katika umma mmoja, hakuna ubaguzi kati yao, hivyo nuru ya Uislamu ilienea katika pembe za dunia katika kipindi kifupi; hiyo ni kwa sababu amri za Uislamu zinahitaji kuangalia raia kwa mtazamo wa kibinadamu, sio mtazamo wa kibaguzi, au wa kimadhehebu, au wa kimashirika, kwani hukumu za Uislamu zilitumika kwa wote, hivyo watu wote wakawa raia wa dola ya Kiislamu hakuna tofauti kati ya Muislamu na asiye Muislamu wala hakuna anayemdhulumu mwingine na ikitokea basi Uislamu unamkemea na kumzuia, Mwenyezi Mungu anasema: ﴿WALA KUCHUKIANA NA WATU KUSIWAFANYE MUWE SI WAADILIFU. FANYENI UADILIFU. HUKO NDIO KUKARIBIA ZAIDI UCHAMUNGU﴾, na watu wote wako sawa katika hukumu mbele ya mahakama, na mfumo wa utawala unahukumu kwa umoja kati ya sehemu za dola, kama unavyohukumu kwa kuhakikisha mahitaji ya kila wilaya bila kujali mapato yake kwa hazina, ambayo inafanya mchanganyiko kuwa wa lazima kati ya wana wa wilaya zote za dola.
Kwa hivyo ilikuwa wajibu kwa kila Muislamu na Muislamu kufanya kazi ya kusimamisha faradhi hii kuu iliyo ghaibu, jumba la Khilafah Rashidah kwa njia ya Utume. ﴿HII DINI YENU NI DINI MOJA, NA MIMI NDIYE MOLA WENU, BASI NIABUDUNI﴾.
===
Njia Pekee ya Ukombozi wa Umma Kutoka Kwa Adhabu Zake
Hakika njia pekee ya ukombozi wa umma kutoka kwa adhabu zake ni kurejesha utukufu wake na heshima yake, ili utoke kutoka katika makucha ya utumwa kwa Magharibi, na urudi kwenye sheria ya Mola wake.