2025-09-10
Gazeti la Ar-Raya: Tofauti Kubwa Kati ya Taarifa ya Istanbul
na Fatwa Zilizotangulia!
Wanazuoni walikusanyika katika ukarimu wa Erdoğan mwishoni mwa kongamano lao walilo liita "Gaza ni jukumu la Kiislamu na kibinadamu" lililo fanyika Istanbul kwa muda wa siku sita, walitoa taarifa ya mwisho ambayo waliifungua kwa aya za maandalizi na jihadi katika njia ya Mwenyezi Mungu mpaka yule anaye soma alidhani kwamba yale yatakayo kuja baada ya hapo kutoka kwa vifungu na maamuzi hayatakuwa ila ni taarifa ya kivitendo ya jinsi ya kujihusisha mara moja katika jihadi ambayo haimuokoi Gaza tu bali inakomboa Palestina na Msikiti wa Al-Aqsa. Lakini hali ilikuwa kinyume na hayo, kwani maamuzi, mapendekezo na wito zili kuja kana kwamba zimeandikwa kwa lugha ya mfumo wa kimataifa unao kubaliana na sheria za kimataifa na kwa kile ambacho mifumo inayo muunga mkono Amerika na Magharibi inasema, na kwa kile kinacho weza kuelezewa kama jaribio baya la kuosha aibu ya watawala na haswa Erdoğan baada ya ulegevu wao na kushirikiana kwao juu ya kuisaidia Gaza, na baada ya kuizuia umma kwa kila njia kutimiza wajibu wake.
Na sisi hatuwazuli hatia wanazuoni hawa tunapo sema kwamba hatujui ni lipi kati ya haya mawili ni hatari zaidi: Kile kilicho kuja katika taarifa ya Istanbul au kile kilicho kosa kuja ndani yake?! Ili kufafanua hilo, sisi, kutokana na kupima jambo kwa mfano wake, tuna fanya hapa ulinganisho rahisi wa haraka kati ya kile kilicho kuja katika taarifa ya Istanbul na kile kilicho kuja kabla yake cha fatwa haswa tangu operesheni ya Tufani ya Al-Aqsa, ambayo ni, kwa muda wa miaka miwili ya mwisho, na tutaita kwa ufupi "Fatwa Zilizotangulia", ambazo ni fatwa zilizo thibitishwa na taasisi zake na wanazuoni na tarehe za kutolewa kwake na zimechapishwa na kuandikwa na inawezekana kuzirejelea, na huu ni ulinganisho wa haki: Kwa upande wa taarifa ya Istanbul iliyo tolewa na wanazuoni, hizo pia ni fatwa zilizo tolewa na wanazuoni lakini zimejengwa juu yake misimamo na matendo tofauti na kile kinacho weza kujengwa juu ya taarifa ya Istanbul.
Ama fatwa zilizotangulia, iwe zimekuja kwa mpango kutoka kwa wanazuoni au kujibu wito na kilio cha msaada kutoka kwa watu wa Gaza na wapiganaji wake ambao walihutubia umma na majeshi yake na wanazuoni wake kwa kujihusisha katika vita vya Tufani ili iwe vita vya ukombozi kamili, fatwa hizo zilizotangulia zimekuja na kwa kuzingatia kile kilicho katika Kitabu cha Mwenyezi Mungu na Sunnah za Mtume wake ﷺ kueleza juu ya ulazima wa kuhamasisha majeshi kwa ajili ya jihadi katika njia ya Mwenyezi Mungu ili kukomboa Palestina ukombozi kamili, na kwamba faradhi hii ni wajibu kwa umma wa Waislamu wote, na kwamba watu wanaostahiki zaidi ni majeshi kwa sababu ya silaha na nguvu zilizo mikononi mwao na kwa sababu ya askari walio funzw katika safu zao, na fatwa za wanazuoni zimeeleza juu ya uharamu wa utii wa wanajeshi kwa viongozi wao katika kukaa juu ya hilo, kama vile baadhi ya fatwa zimeeleza juu ya ulazima wa kuwapinga watawala kwa sababu imethibitika ushirikiano wao na ulegevu wao na kuuzuia umma kuisaidia Gaza na kukomboa Palestina, na fatwa zimeeleza kwamba kile kinacho fanywa na watawala na wasaidizi wao cha ushirikiano na ulegevu kinasababisha ghadhabu ya Mwenyezi Mungu na adhabu yake katika dunia na akhera, na kwamba hilo linavunja vifungo vya uaminifu na kutengana, na wanazuoni wameita umma kuvunja vizuizi kwa nguvu na jihadi katika njia ya Mwenyezi Mungu kuisaidia Gaza na watu wake na kutokusubiri ruhusa kutoka kwa watawala, na zimeeleza kwamba wito ulio elekezwa kutoka kwa wanazuoni kwenda kwa serikali na watawala ni kwa ajili ya kujitetea kwa Mwenyezi Mungu na kwamba watawala hawatafanya chochote baada ya ushirikiano huu wote. Hii ni pamoja na kile ambacho fatwa hizo zimejumuisha cha maneno ya haki ambayo miili ya waumini husisimka kama vile kwamba umma na wanazuoni wake hawawezi kuvumilia kusimama mbele ya Mwenyezi Mungu siku ya Kiyama kama wapinzani wa watu wa Gaza kutoka kwa wapiganaji na walinzi mipaka, na kwamba kifo ni rahisi kwao kuliko ugomvi huu.
Na kwa mtazamo wa haraka mfupi, kile kinacho jengwa cha matendo juu ya fatwa zilizotangulia kinausukuma umma kuvunja mnyororo wake na kuondokana na watawala wake na kurejesha udhibiti wa nguvu zake na majeshi yake na kuandamana ili kutimiza wajibu wake na kufanya faradhi ya Mola wake mpaka kukomboa Palestina yote licha ya pua za serikali na wasaidizi wake.
Ama taarifa ya Istanbul, ilikosa wito huu wote: Haikutoa wito wa kuhamasisha majeshi, wala kuandamana, wala kuvunja mnyororo wa umma kutoka kwa watawala wake, wala haikutoa wito hata wa kukomboa Palestina! Na badala ya hayo yote, ilikubali wito wa Erdoğan wa kuunda muungano wa Kiislamu aliouelezea kama "wa kibinadamu" na kuweka lengo lake "kusimamisha uchokozi na kuwafuatilia wahalifu"! Taarifa ya Istanbul iliyo funguliwa kwa kutaja "ukimya wa kimataifa na ushirikiano wa kikanda" iliendelea katika kuelekeza wito kwa washirika kutoka nchi za dunia na kutoka nchi zilizo katika nchi za Waislamu, na ilitoa wito wa umuhimu wa kuwasiliana nao ili kuwashinikiza kuchukua misimamo, na ilitoa wito pia wa muungano wa kimataifa wa haki za binadamu na bunge, na ilitoa wito kwa taasisi za Wakristo na haswa Papa wa Vatikani, na ilitoa wito hata kwa taasisi za Wayahudi kuokoa Gaza!!! Na ilitoa wito wa kuamilisha maamuzi ya Mahakama ya Kimataifa ya Haki na Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu, badala ya kutumia sheria ya Mwenyezi Mungu na hukumu Yake kwa yule anayepigana na Waislamu na kukalia ardhi yao kwa mabavu.
Ama kwa Waislamu, taarifa ya Istanbul ilizuia wajibu wao katika kutenga michango na nusu ya zaka ya mwaka ujao kwa ajili ya kusaidia Gaza na kuijenga upya baada ya kumalizika kwa vita badala ya kutoa wito wa kutangaza vita vya ukombozi, na wakati wa kuzungumza juu ya kuvunja mzingiro ilizuia wito kwa njia zinazopatikana ikiwa ni pamoja na kuunga mkono msafara wa uhuru kwa meli badala ya kutoa wito wa kuendesha meli za kivita na majeshi.
Na taarifa ya Istanbul iliunganisha kati ya sheria ya Kiislamu na sheria ya kimataifa kama rejea wakati wa kutoa wito wa kukata uhusiano na shirika la Kiyahudi badala ya kutoa wito wa kuondoa uvimbe mbaya. Kisha baada ya hapo ilisisitiza juu ya utakatifu wa sanamu ya utaifa wakati ilibeba jukumu la kukabiliana na mipango ya "Israeli Kubwa" kwa nchi zinazo lengwa pekee.
Kisha taarifa ya Istanbul ilihitimisha kwa ushahidi wa uongo mbele ya umma kwa shukrani na kutambua kwa Erdoğan akielezea serikali yake kama yenye busara.
Kwa muhtasari huu, matendo ambayo yanaweza kujengwa juu ya taarifa ya Istanbul yanaonekana wazi, haya hayazidi kukusanya michango na kuelekeza wito kwa maadui kusimamisha vita, na zaidi ya hayo inawaondolea hatia watawala na serikali ya uhalifu wa ushirikiano na ulegevu na inafanya utekelezaji wa maamuzi yake na wito wake ukabidhiwe kwa watawala hawa licha ya ukweli unao ng'aa wa njama zao na ushirikiano wao.
Ilistahili "wanazuoni wa Istanbul" walio chini ya Umoja wa Kimataifa wa Wanazuoni wa Kiislamu na chini ya Wakfu wa Wanazuoni wa Kiislamu nchini Uturuki ambao walikusanyika kwa mamia kwenye meza ya Erdoğan wawe na misimamo ya kivitendo ambayo inafanya umma wote na majeshi yake wajihusishe katika hatua ya haraka ambayo haisababishi tu kuisaidia Gaza na kusimamisha vita bali pia kukomboa ardhi yote ya Palestina, na iliwastahili misimamo yao iwe ya wito wa watu na askari kuacha shughuli zao wakati vyombo vya habari vinatangaza taarifa zao wakisubiri kusikia maelekezo ya kivitendo ambayo watauelekeza umma kwayo, na iliwastahili ulimwengu uzuie pumzi zao na kwamba mioyo ya makafiri wote itetemeke kwa kutaja tu mkutano wao, lakini ole wao walikataa kuwa na uwezo wa hilo!
Hatimaye, maswali mawili ambayo yanastahili kuulizwa katika mazingira ya matokeo haya ya kongamano la Istanbul, ni: Je, kweli kongamano hili lilifanyika kwa ajili ya kuisaidia Gaza? Au lilifanyika ili kujaribu kuzuia kitendo chochote muhimu ambacho kinaweza kujengwa juu ya fatwa za wanazuoni zilizotangulia??
Na baada ya taarifa ya Istanbul, mnataka adui yetu mwovu aelewe nini kutoka kwetu? Mauaji zaidi, uharibifu, vipande vya viungo, na uhamaji? Je, ataelewa zaidi ya kwamba hii ndiyo kiwango cha juu ambacho umma wa mabilioni mawili unaweza kufanya au hata kufikiria?!
Imeandikwa na: Profesa Abdullah Hamad Al-Wadi - Ardhi Iliyobarikiwa (Palestina)
Chanzo: Gazeti la Ar-Raya