Kazakhstan Inataka Kujiunga na Msafara wa Kupambana na Nikabu katika Asia ya Kati
Habari:
Baraza la Seneti katika Bunge la Kazakhstan limependekeza marekebisho ya sheria ya kuzuia uhalifu. Kulingana na marekebisho mapya, uvaaji wa burqa, nikabu na nguo zinazofunika uso mzima utapigwa marufuku katika maeneo ya umma. Hii iliripotiwa na shirika la habari la Kazakhstan Tengrinews.
Marekebisho yaliyopendekezwa yanasema kwamba uvaaji wa nikabu utaruhusiwa tu kwa dharura za matibabu, ulinzi wa raia, mahitaji ya kisheria, hali mbaya ya hewa, au wakati wa shughuli za michezo na kitamaduni.
Rais Kassym-Jomart Tokayev, alisisitiza katika Kongamano la Kitaifa lililofanyika Machi mwaka huu, umuhimu wa kukuza mavazi ya kitaifa badala ya nguo nyeusi zinazofunika uso.
Maoni:
Kama inavyojulikana, sheria za kupinga Uislamu pia zimepitishwa nchini Turkmenistan, Tajikistan, Uzbekistan na Kyrgyzstan kwa kisingizio cha nikabu. Hasa, uvamizi hufanyika mara kwa mara, nchini Uzbekistan na Tajikistan, ambapo maafisa wa polisi huwapeleka wanawake Waislamu wanaovaa nikabu na wanaume wenye ndevu wanaotembea mitaani kwenye vituo vya polisi kwa tuhuma za kufanya "itikadi kali za kidini". Maafisa wa kutekeleza sheria nchini Kyrgyzstan walifanya msako mwezi uliopita dhidi ya nikabu katika eneo la kusini. Na sasa serikali ya Kazakhstan inakaribia kujiunga na msafara wa kupambana na nikabu.
Kwa kawaida, vita vya mamlaka katika Asia ya Kati dhidi ya Uislamu havikuanza hivi karibuni, na labda ilianza baada ya kuondoa wapinzani wao na kuanzisha mifumo ya kidikteta. Kwa mfano, rais dikteta wa Uzbekistan aliyekufa Karimova, alianza vita kubwa dhidi ya Uislamu na Waislamu, baada ya kuandaa mlipuko wa Februari 16, 1999 huko Tashkent.
Pia, dikteta wa Tajikistan Imam Ali Rahmon, alipiga marufuku utoaji wa majina ya Kiislamu kwa watoto, kwa kisingizio cha kupambana na ugaidi na itikadi kali. Serikali ya Tajikistan ilinyoa ndevu za makumi ya maelfu ya wanaume, na kuondoa hijabu za maelfu ya wanawake kwa nguvu.
Nchini Turkmenistan, polisi hukagua nyumba za watu wanaowaona kuwa ni watu wa dini na wanachukua kila aina ya maandiko ya kidini isipokuwa Kurani. Turkmenistan haiko nyuma ya Uzbekistan na Tajikistan katika vita dhidi ya Uislamu na Waislamu. Kunyoa ndevu za wanaume Waislamu walio chini ya umri wa miaka 50 kwa lazima, kuwalazimisha kunywa vodka, na kuwapiga Waislamu waliokataa kutii matakwa haya kwa nguvu na kuwafunga jela kwa miaka 7-8 bila kesi au uchunguzi wowote, imekuwa jambo la kawaida! Pia, wafanyakazi wa kiraia na kijeshi wanazuiwa kufanya ibada kama vile sala, na wale wasiotii hilo hufukuzwa mara moja na wanakabiliwa na shinikizo mbalimbali za kifedha na kimwili.
Baraza la Mawaziri la Kyrgyzstan lilipitisha mwaka jana, sheria juu ya masuala ya kidini yenye lengo la kuzuia Uislamu na Waislamu. Chini ya sheria hii, dada zetu Waislamu walizuiwa kuvaa nikabu, na vita vilizidi katika vituo vya mahabusu dhidi ya ndugu zetu Waislamu waliobeba da'wa, na shughuli zisizo halali, kama vile mshtuko wa umeme na kupigwa vikali zikawa za kawaida. Kwa njia hii, serikali inajaribu kudhibiti mazingira ya Kiislamu yaliyo mizizi katika jamii.
Ama nchini Kazakhstan, mapambano dhidi ya maadili ya Kiislamu yameongezeka baada ya wanafunzi wa shule kuzuiliwa kuvaa hijabu.
Kwa hakika, kuzuia nikabu na ndevu kunapingana na maadili ya kidemokrasia ambayo mifumo hii ya kidikteta inazingatia. Kwa usahihi zaidi, uhuru wa imani na uhuru wa mtu binafsi katika demokrasia unamhakikishia mtu kufanya dini yoyote na kutumia faida yoyote. Maadili haya ni sheria ya kikatiba ya dola ya kilimwengu. Hata hivyo, Magharibi, kituo cha demokrasia, tayari imeanza kuachana na wazo lake. Kwa maneno mengine, kwa Magharibi, uhuru huu unatumika tu kwa wasio Waislamu na Waislamu. Kwa mfano, uhuru wa kidini hupewa kuabudu shetani au maovu mengine. Wasio Waislamu wanaruhusiwa kuvaa nguo wanazotaka na hata kwenda mitaani wakiwa uchi. Lakini linapokuja suala la maadili ya Kiislamu, suala hilo linaangaliwa tofauti. Hii inaonekana wazi katika kupiga marufuku uvaaji wa hijabu shuleni nchini Ufaransa mwaka 2004, kufukuzwa kazi kwa wanawake Waislamu kutoka taasisi za umma, na kupiga marufuku nikabu katika maeneo ya umma mwaka 2010!
Hii inamaanisha kwamba mfumo wa kidemokrasia na mfumo wa kiimla ni pande mbili za sarafu moja, ambayo ni kwamba zote zinaweka mapenzi yake juu ya mapenzi ya watu! Hasa, matukio yaliyotokea Turkistan Mashariki, Afghanistan, Syria, na hivi karibuni huko Gaza, yameonyesha kuwa itikadi za uhuru, haki za wanawake na watoto zilifukiwa ardhini na milipuko ya mabomu.
Kwa kweli, wanawake Waislamu hawavaa nikabu kwa sababu demokrasia mnafiki inaruhusu au kwa sababu ya uhuru wa mtu binafsi, lakini huvaa kama hukumu ya kisheria na thamani ya Kiislamu. Pia, Waislamu hawanyoi ndevu zao kwa sababu makafiri au mawakala wao wanakataza, lakini wanaziacha kwa sababu ya sunna ya Mtume ﷺ, kwa sababu katika Mtume ﷺ kuna mfano mzuri kwa kila Muislamu katika kila nyanja ya maisha, na kwa hivyo, lazima tupinge vita vya serikali za kidikteta katika Asia ya Kati dhidi ya Uislamu, kwa sababu serikali inayozuia hijabu na ndevu leo, ni kawaida kwamba itazuia kesho pia dua zetu, sala zetu na funga zetu.
Imeandikwa kwa ajili ya Radio ya Ofisi ya Habari Kuu ya Hizb ut-Tahrir
Mumtaz Mawarannahr