Hakuna Marekebisho ya Uchaguzi au Katiba Yatakayoikomboa Tanzania
(Imetafsiriwa)
Habari:
Wakati Tanzania ikijiandaa kwa uchaguzi mkuu mnamo Oktoba 2025, kuna hali ya mgawanyiko wa kisiasa na tofauti za maoni kati ya wanasiasa na vyama vya siasa, ambayo imesababisha mjadala mkubwa katika uwanja wa kisiasa.
Maoni:
Hali ya wasiwasi wa kisiasa iliyopo kabla ya uchaguzi mkuu ujao mwaka huu nchini Tanzania, imeleta mitazamo mikuu mitatu ya kisiasa, ambayo kila moja inaungwa mkono sana na makundi mbalimbali ya watu kote nchini.
Kundi la kwanza, linawakilishwa na wale wanaotaka mageuzi ya haraka ya uchaguzi, na mwelekeo huu unaongozwa na chama kikuu cha upinzani "Chadema" chini ya kauli mbiu "Hakuna Marekebisho, Hakuna Uchaguzi". Kundi hili linaona kwamba bila mageuzi, uchaguzi hauwezi kuwa huru na wa haki, na kwa hiyo unapaswa kususwa.
Na kundi la pili, linataka mageuzi ya katiba, na linaongozwa na chama cha pili cha upinzani, Muungano wa Mabadiliko na Uwazi. Mwelekeo huu unazingatia kurekebisha katiba, lakini tofauti na "Chadema", haukubali chaguo la kususia uchaguzi.
Ama kundi la tatu, linaunga mkono hali iliyopo na linaunga mkono serikali ya sasa, kwani kundi hili halioni haja ya kufanya mageuzi katika mfumo wa usimamizi wa uchaguzi au katika katiba, bali linaunga mkono sheria na taratibu za sasa, na wameathiriwa sana na serikali ya sasa na chama tawala cha Mapinduzi.
Lakini mikondo hii mitatu, pamoja na vyama vyake na wafuasi wake, haitafanikisha mabadiliko yoyote ya kweli ambayo yanatumikia nchi au umma, kinyume na kile wanachodai.
Kwa upande wa wale wanaounga mkono mageuzi ya uchaguzi, wanapaswa kukumbuka kwamba Tanzania imeshuhudia majaribio mengi ya mageuzi ya uchaguzi hapo awali, ikiwa ni pamoja na mwaka 2010, 2019, na ya hivi karibuni zaidi mwaka 2023 wakati sheria ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi ilipopitishwa. Hata hivyo, mageuzi haya hayajazaa matunda.
Ama wafuasi wa mageuzi ya katiba wakiongozwa na Muungano wa Mabadiliko na Uwazi, ambao pia walizindua kampeni yao mwaka 2024, wanapaswa kujua kwamba Tanzania tangu ilipopata uhuru wake rasmi mwaka 1961 imeshuhudia mageuzi na marekebisho kadhaa ya katiba, ikiwa ni pamoja na mwaka 1961, 1962, 1964, 1965, na 1977. Zanzibar pia ilifanya marekebisho mwaka 1963, 1979, na 1984. Tangu wakati huo, marekebisho yameendelea katika pande zote mbili za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, bila kufikia matokeo yanayoonekana.
Ama kwa upande wa wanaounga mkono hali iliyopo kutoka kwa wafuasi wa chama tawala na serikali, pia hawako upande salama, kwani udhaifu katika sheria na katiba za sasa umekuwa wazi kwa kila mtu.
Ambacho mikondo mitatu imeshindwa kuelewa, ni kwamba kiini cha tatizo si katika sheria za uchaguzi au katiba wala hata katika upinzani - kama wafuasi wa serikali wanavyoona - lakini ni katika mfumo wa kibepari wenyewe, ambao sheria na kanuni zote zinazotumika sasa nchini Tanzania na katika nchi zinazoendelea zinatokana nao, na ambazo kimsingi ni sheria za kigeni za kikoloni.
Kupitia sheria hizi za kibepari, utawala wa kikoloni unawekwa kwa Tanzania na ulimwengu unaoendelea, ambao unawezesha mataifa ya kibepari kunyonya utajiri na rasilimali zake.
Kwa hiyo, mabadiliko ya kweli na madhubuti ya ukombozi wa Tanzania na wengineo, lazima yazingatie kuondoa kanuni hii ya kibepari iliyoharibika, na kubadilisha Uislamu chini ya uongozi wake wa ulimwengu; Khilafah, nayo.
Imeandikwa kwa ajili ya Idhaa ya Afisi ya Habari Kuu ya Hizb ut Tahrir
Saeed Baytumwa
Mwanachama wa Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir nchini Tanzania