Wayahudi na wanaowaunga mkono hawatazuiliwa kwa kulaani, kukemea na kufanya mazungumzo
Habari:
Mashambulizi ya kundi la Wayahudi yanaendelea na ndege zake haziondoki katika anga ya Lebanon, na wanatishia vita vikali baada ya Gaza.
Maoni:
Kundi la Wayahudi linaendelea kushambulia maeneo mengi ya Lebanon, likiua, kuharibu na kuwafukuza watu, na pia linatishia vita vikali, kuivamia Lebanon na kuwahamisha watu wake. Kinyume chake, mataifa ya ulimwengu yamenyamaza, na mamlaka ya Lebanon inatosheka na wito wa mazungumzo na kujisalimisha ili kusitisha mashambulizi na uhamishaji, na kuomba mataifa makubwa, haswa Amerika, kusimamisha mashambulizi hayo, ikijua kuwa kundi la Wayahudi linatumia silaha za mataifa hayo katika mashambulizi yake na linapokea msaada usio na kikomo kutoka kwao!
Kuhusiana na mashambulizi hayo, tunasisitiza yafuatayo:
- Kinachotokea sio tu mgogoro wa mpaka, au mashambulizi ya muda mfupi, lakini ni sehemu ya mradi wa uvamizi wa Wayahudi dhidi ya umma wa Kiislamu ili kukalia nchi za Sham na Misri na kutimiza ndoto ya Wayahudi ya "Israeli Kubwa", wakati mamlaka ya Lebanon haina uamuzi wa kweli na inatosheka na kulaani, wasiwasi na kukemea, na inawashambulia kwa ukali wale wanaokosoa msimamo wake na usaliti wa wanasiasa wake.
- Wito unaorudiwa wa mazungumzo au majadiliano ni kukimbia kutoka kwa wajibu wa kisheria na wa jihadi, kwa sababu inawakilisha kukubalika kwa msingi wa ukweli wa mkaazi na mipaka iliyo hatarini.
- Kuunganisha safu chini ya bendera ya jihadi na kuanzisha upya maisha ya Kiislamu katika kivuli cha dola ya Khilafa kwa misingi ya unabii ndio suluhisho badala ya kutegemea mataifa makubwa au Umoja wa Mataifa au kuomba "mazungumzo" na adui.
- Kuendelea kwa mashambulizi na uhamishaji kunaonyesha kuwa kundi la Wayahudi halijioni limefungwa na vizuizi vyovyote vya kweli mradi tu hakuna majibu ya Kiislamu ya kutisha ambayo yanamtisha na kumzuia.
Na tunatumai kwa Mungu kwamba atatimiza ahadi yake kwetu; kwa kuondoa kundi la Wayahudi na kuanzisha dola ya Khilafa ambayo inaondoa mipaka na vizuizi bandia kati ya nchi za Waislamu ﴿NA MWENYEZI MUNGU NI MSHINDI JUU YA MAMBO YAKE, LAKINI WATU WENGI HAWAJUI﴾.
Imeandikwa kwa ajili ya redio ya Ofisi ya Habari Kuu ya Hizb ut-Tahrir
Sheikh Dk. Muhammad Ibrahim
Mkuu wa Ofisi ya Habari ya Hizb ut-Tahrir katika Jimbo la Lebanon