Sio nguvu zenu nyinyi vibete
bali ni uungwaji mkono wa wachungaji wenu wahalifu na unyonge wa mifumo yetu
Habari:
Kituo cha televisheni cha Al Jazeera kimeripoti matamshi ya waziri mkuu wa utawala haramu wa kiyahudi Netanyahu akisema: Tulipokea tarehe 7 Oktoba 2023 msiba mbaya zaidi katika historia yetu lakini tulilipa kisasi mara mbili. Alinukuliwa akisema: Tumefika Tehran na tumeharibu mhimili wa uovu wa Iran kwa gharama kubwa iliyolipwa na ngome yetu ya ndani.
Maoni:
Ukweli ambao Waislamu wameanza kuutambua, na labda ulimwengu mzima unauona, ni kwamba utawala haramu hautapona, haijalishi utafanya nini, kutokana na kuvunjika kwa picha bandia ambayo ilichorwa kwake kwamba ni utawala haramu ambao hauwezi kuguswa na kwamba jeshi lake haliwezi kushindwa.
Wale waliofanya tarehe saba Oktoba 2023 enyi huyu walikutana na askari wenu waliokimbia huku wakilia, na wao ndio askari wale wale ambao vilio vyao vilirekodiwa katika shambulio la kuvizia la hivi karibuni, wanajua kuwa nyinyi sio watu wa kupigana. Na tarehe saba Oktoba 2023, Marekani haikuwa ikiwalinda dhidi yao na watawala hawakuwa wakitoa mazingira na usambazaji kwenu, mlikuwa nyinyi na askari wenu peke yenu ardhini.
Lakini baada ya hapo, ulimwengu mzima ulianza kutazama kwa chuki majibu ambayo utawala wenu haramu unafanya katika jaribio la kurejesha sura yake jinsi yalivyolenga mauaji ya kimbari, ulipuaji, uharibifu, na vita vya njaa ambavyo unavianzisha dhidi ya watu wa Gaza mbele ya macho na masikio ya ulimwengu unaotazama kimya kimya uhalifu mbaya zaidi ambao mtu anapaswa kuaibika nao.
Huyu anayejigamba kulipa kisasi mara mbili anajua zaidi kuliko wengine kuwa yeye na utawala wake haramu hawangeweza kutenda uhalifu huu bila msaada kamili wa Magharibi wanaopokea, na bila njama za tawala vibaraka zilizopo katika nchi za Waislamu, ambazo zimetoa msaada na usambazaji kwake na zimeshiriki katika kuzingira Gaza na kuizuia umma usiwasaidie ndugu zao.
Huyu anayejigamba kulipa kisasi mara mbili anajua kuwa hangekuwa na uwezo wa kufanya fujo katika nchi za Waislamu na kuvunja heshima ya miji yao mikuu bila ya nchi hizi kutawaliwa na tawala dhaifu zilizotengwa na umma, masuala yake, na mradi wake, kwani mradi wa umma ni mradi wa uamsho, ukhalifa, na ukombozi kamili, lakini mradi wa tawala ni kuhifadhi viti vyao vya enzi kwa kutekeleza amri za Magharibi, ambazo ni pamoja na kudumisha usalama wa utawala huu haramu mbaya wa saratani.
Huyu anayeomboleza gharama ambayo ngome yake ya ndani imelipa katika vita vyake dhidi ya Iran na wengineo, ambavyo anavianzisha kwa msaada, ufadhili, ushawishi, na silaha kutoka Ulaya na Marekani, ajue vita hivi vingekuwaje ikiwa angekuwa anavipigana dhidi ya dola inayowakilisha umma wa Kiislamu kweli, dola ambayo hairidhiki na chochote pungufu ya makabiliano kamili na vita vya ukombozi si tu dhidi ya utawala wake, bali dhidi ya mhimili halisi wa uovu ambao umepanda utawala wake katika ardhi iliyobarikiwa, na anajua vizuri ni gharama gani atalipa katika makabiliano haya yajayo hivi karibuni bila shaka.
﴿Waambie wale walio kufuru, mtashindwa na mtakusanywa kwenda Jahannamu, na ni makao maovu mno.﴾
Imeandikwa kwa ajili ya Idhaa ya Ofisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir
Abdullah Hamad Al-Wadi