Pamoja na Hadithi Tukufu - Furahini Enyi Mnaopenda Kukutana na Mwenyezi Mungu
Tunawasalimu nyote wapenzi wetu popote mlipo, katika kipindi kipya cha programu yenu "Pamoja na Hadithi Tukufu" na tunaanza na salamu bora, Assalamu Alaikum Warahmatullahi Wabarakatuh.
Imekuja katika Fath Al-Bari Sharh Sahih Al-Bukhari ya Ibn Hajar Al-Asqalani "kwa ufupi" katika mlango wa Anayependa Kukutana na Mwenyezi Mungu, Mwenyezi Mungu Hupenda Kukutana Naye:
Muhammad bin Al-Alaa ametuhadithia, Abu Usama ametuhadithia kutoka kwa Bureid, kutoka kwa Abu Burda, kutoka kwa Abu Musa, kutoka kwa Mtume صلى الله عليه وسلم amesema: "Anayependa kukutana na Mwenyezi Mungu, Mwenyezi Mungu hupenda kukutana naye, na anayechukia kukutana na Mwenyezi Mungu, Mwenyezi Mungu huchukia kukutana naye."
Enyi wasikilizaji wapenzi:
Hakika muumini anaamini yale yaliyoko kwa Mwenyezi Mungu سبحانه وتعالى, na anaamini yale ambayo Mwenyezi Mungu amemuandalia katika Pepo ya kheri tele, na anaamini yale ambayo mpenzi صلى الله عليه وسلم amembashiria ya kheri, basi unamuona anapenda kukutana na Mwenyezi Mungu na anaharakisha, na badala yake Mwenyezi Mungu anapenda kukutana naye. Ama kafiri hamuamini Mwenyezi Mungu تعالى, wala haamini yale ambayo Mwenyezi Mungu amemuandalia ya adhabu kubwa, kwa hivyo hapendi kukutana na Mola wake wala haharakishi, na badala yake Mwenyezi Mungu hapendi kukutana naye.
Enyi Waislamu:
Ni wangapi kati yetu leo wanapenda kukutana na Mwenyezi Mungu? Yule ambaye matendo yake mema yako mbele yake anapenda kukutana na Mwenyezi Mungu, yule ambaye amesimama sawasawa juu ya amri ya Mwenyezi Mungu anapenda kukutana na Mwenyezi Mungu, yule ambaye hamu yake ni Mwenyezi Mungu na Mtume wake anapenda kukutana na Mwenyezi Mungu, yule anayejali masuala ya Waislamu anapenda kukutana na Mwenyezi Mungu, yule anayefanya kazi ya kurejesha hukumu za Mwenyezi Mungu zitekelezwe katika ardhi ya Mwenyezi Mungu anapenda kukutana na Mwenyezi Mungu, yule ambaye dunia imekuwa ndogo machoni pake na imekuwa rahisi, na nafsi yake imekuwa duni kwa ajili ya kumridhisha Mwenyezi Mungu anapenda kukutana na Mwenyezi Mungu, yule anayefanya kazi na wafanyakazi wa kusimamisha Khilafa Rashidah ya pili juu ya manhaj ya Utume kwa kutimiza ahadi ya Mwenyezi Mungu na bishara ya Mtume wake صلى الله عليه وسلم anapenda kukutana na Mwenyezi Mungu, basi furahini enyi mnaompenda Mwenyezi Mungu, kwa mapenzi ya Mwenyezi Mungu سبحانه وتعالى kwenu.
Ewe Mola wetu, tuharakishie Khilafa Rashidah juu ya manhaj ya Utume itakayokusanya misukosuko ya Waislamu, iondolee yale waliyo nayo ya balaa, Ewe Mola wetu, ing'arisha ardhi kwa nuru ya uso wako mtukufu.
Ewe Mola wetu, Amin Amin.
Wapenzi wetu, na mpaka tukutane nanyi na hadithi nyingine ya Mtume, tunawaacha katika ulinzi wa Mwenyezi Mungu, Assalamu Alaikum Warahmatullahi Wabarakatuh.
Imeandikwa kwa ajili ya redio na: Abu Maryam