Pamoja na Hadithi Tukufu
Tutamjibu vipi Mtume, rehema na amani zimshukie, kwenye hodhi yake?
Tunawasalimu nyote wapenzi popote mlipo, katika kipindi kipya cha programu yenu "Pamoja na Hadithi Tukufu" tunaanza na salamu bora, Assalamu Alaikum Warahmatullahi Wabarakatuh.
Imekuja katika Fath Al-Bari Sharh Sahih Al-Bukhari na Ibn Hajar Al-Asqalani kwa muhtasari katika "Sura kuhusu Hodhi na kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu: "Hakika Tumekupa Al-Kawthar":
Na amenisimulia Amr bin Ali, ametusimulia Muhammad bin Jaafar, ametusimulia Shu'ba kutoka kwa Al-Mughira, amesema: Nilimsikia Abu Wael kutoka kwa Abdullah, Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, kutoka kwa Mtume, rehema na amani zimshukie, amesema: "Mimi ni mtangulizi wenu kwenye hodhi, na watu kutoka kwenu watainuliwa pamoja nami kisha watanyakuliwa mbali nami, nami nitasema: Ee Mola wangu hao ni masahaba zangu, itasemwa: Hakika wewe hujui walichokizua baada yako."
Enyi wasikilizaji wapenzi:
"Mimi ni mtangulizi wenu kwenye hodhi" Anayekusudiwa kuwa mtangulizi kwa fatha ya faa na raa: yaani yule anayetangulia wanaoenda kupata maji ili atengeneze mabwawa na ndoo na mfano wake, inasemwa amewatangulia watu ikiwa amewatangulia kuwaletea maji na kuwatayarishia. "Wananyakuliwa": Yaani wanavutwa na kubururwa.
Enyi Waislamu:
Hakika ni msimamo mgumu wa kutisha anasimama Mtume, rehema na amani zimshukie, kwenye hodhi, anawanywesha watu kutoka kwenye kiganja chake kitukufu na Malaika wanawazuia watu wengine, unaona ni zipi sababu za kufika kwenye hodhi na zipi sababu za kuzuiwa?
Hakika miongoni mwa sababu za kufika kwenye hodhi ni kusubiri uonevu wa watawala na dhuluma yao, bali na kufanya kazi ya kuwang'oa, na kubadilisha hali halisi ambayo imejaa maovu kwa sababu yao, kwani amebainisha hilo yeye, rehema na amani zimshukie, mahali pengine aliposema kwa Ansari: "Hakika mtaona baada yangu ubinafsi, basi subirini mpaka mnifikie kwenye hodhi", basi subira hapa haimaanishi kukubali au kuridhia hali halisi; bali subira wakati wa kufanya kazi kwa yale anayokutana nayo Muislamu ya kuzuiliwa na kuadhibiwa na kuuawa, basi tunastahiki kwa nabii wetu mtukufu, rehema na amani zimshukie, kuwa mtangulizi wetu kwenye hodhi, na anastahiki anayefanya kazi na kusubiri ili awe pamoja naye kwenye hodhi. Na kutokusubiri watawala au kwenda nao na kuwakubali na kutofanya kazi ya kuwabadilisha ni miongoni mwa sababu za kutofika kwenye hodhi. Kwa hili anaweza kila Muislamu kuchagua kufika kwenye hodhi au kuzuiwa.
Ewe Mola wetu tuharakishie ukhalifa juu ya manhaj ya utume uondoe mtafaruku wa Waislamu, uwaondolee yale waliyomo ya balaa, Ewe Mola wetu uangaze ardhi kwa nuru ya uso wako mtukufu. Ewe Mola wetu Amin Amin.
Wapenzi wetu, na mpaka tutakapokutana na hadithi nyingine ya kinabii, tunawaacha katika hifadhi ya Mwenyezi Mungu, Assalamu Alaikum Warahmatullahi Wabarakatuh.
Imeandikwa kwa ajili ya Radio na: Abu Mariam