Pamoja na Hadithi Tukufu - Ghadhabu kwa Ajili ya Mwenyezi Mungu
Pamoja na Hadithi Tukufu - Ghadhabu kwa Ajili ya Mwenyezi Mungu

Tunawasalimu nyote wapenzi wasikilizaji kila mahali katika kipindi kipya cha programu yenu: Pamoja na Hadithi Tukufu, na tunaanza na salamu bora, Amani iwe juu yenu pamoja na rehema na baraka za Mwenyezi Mungu.

0:00 0:00
Speed:
June 29, 2025

Pamoja na Hadithi Tukufu - Ghadhabu kwa Ajili ya Mwenyezi Mungu

Pamoja na Hadithi Tukufu

Ghadhabu kwa Ajili ya Mwenyezi Mungu

Tunawasalimu nyote wapenzi wasikilizaji kila mahali katika kipindi kipya cha programu yenu: Pamoja na Hadithi Tukufu, na tunaanza na salamu bora, Amani iwe juu yenu pamoja na rehema na baraka za Mwenyezi Mungu.

Kutoka kwa Aisha ambaye alisema: "Mtume wa Mwenyezi Mungu ﷺ hajawahi kumpiga mtu kwa mkono wake, wala mwanamke, wala mtumishi, isipokuwa alipokuwa akipigania njia ya Mwenyezi Mungu. Na hakuna kitu kilichowahi kumfika akalipiza kisasi kwa aliyemdhulumu, isipokuwa pale lilipovunjwa jambo katika matukufu ya Mwenyezi Mungu, ndipo hulipiza kisasi kwa ajili ya Mwenyezi Mungu Mtukufu." Imepokewa na Muslim.

Ibn Taymiyyah, Mwenyezi Mungu amrehemu, alisema: [Watu wamegawanyika katika sehemu tatu: Sehemu ya watu wanaghadhibika kwa ajili ya nafsi zao na kwa ajili ya Mola wao, na sehemu ya watu hawaghadhibiki kwa ajili ya nafsi zao wala kwa ajili ya Mola wao, na sehemu ya watu wanaghadhibika kwa ajili ya Mola wao wala si kwa ajili ya nafsi zao, na hii ndiyo tabia ya Mtume wa Mwenyezi Mungu ﷺ. Ama yule anayeghadhibika kwa ajili ya nafsi yake wala si kwa ajili ya Mola wake, au anachukua kwa ajili ya nafsi yake wala hamupi mwingine, hao ndio viumbe wabaya zaidi, hawafai kwa dini wala dunia].

Wasikilizaji wetu wapenzi

Hakika watawala wabaya katika zama hizi wamefanya sababu za ghadhabu kuwa nyingi na za kudumu. Miongoni mwa sababu hizo ni kutohukumu kwa yale aliyoyateremsha Mwenyezi Mungu, na kupuuza matukufu ya Mwenyezi Mungu na kuyavunja, na kufuata sera zinazopelekea umaskini, udhalili, kunyimwa, na kushindwa umma, na wao wanakesha kwa upotevu na ujinga, na wanalinda ucheleweshaji katika nyanja zote, na wanawazuia kutekeleza ibada kama alivyoamrisha Mwenyezi Mungu. Na sababu hazimaliziki, na ni lazima kuwe na ghadhabu, ghadhabu ya kudumu na endelevu, ghadhabu kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, na kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, na kwa ajili ya dini yake na Mtume wake ﷺ. Ghadhabu ambayo inaambatana na kufanya kazi ili kubadilisha sababu za ghadhabu. Yeyote asiyeghadhibika kwa ajili ya Mwenyezi Mungu na akaghadhibika kwa ajili ya nafsi yake, basi amestahiki aliyo nayo. Na yule aliyegadhibika kwa kupanda kwa bei na hakugadhibika kwa kukosekana kwa hukumu ya Mwenyezi Mungu, basi amestahiki alicho nacho. Yule aliyegadhibika kwa kutukanwa nafsi yake na hakugadhibika kwa kutukanwa Nabii wake, basi amestahiki alicho nacho. Watu wema ndio wale wanaotekeleza wajibu na kuacha yaliyoharamishwa, na wanaghadhibika kwa ajili ya Mola wao ikiwa matukufu yake yamevunjwa. Hizi ndizo tabia za Mtume wa Mwenyezi Mungu ﷺ katika kutoa na kulipa, na ndizo mambo kamili zaidi, hivyo ni lazima kuwe na ghadhabu kwa ajili ya Mwenyezi Mungu na kufanya kazi ya kuleta ukhalifa ambao utaondoa sababu zake na kuacha sababu za radhi na utulivu.

Wasikilizaji wetu wapenzi

Na mpaka tutakapokutana nanyi na hadithi nyingine ya Nabii, tunawaacha katika uangalizi wa Mwenyezi Mungu, na Amani iwe juu yenu pamoja na rehema na baraka za Mwenyezi Mungu.

More from Sheria

Pamoja na Hadithi Tukufu - Je, mnajua ni nani mfilisi?

Pamoja na Hadithi Tukufu

Je, mnajua ni nani mfilisi?

Karibuni wasikilizaji wetu wapendwa, wasikilizaji wa redio ya Ofisi ya Habari Kuu ya Hizb ut-Tahrir. Tunakutana nanyi tena na kipindi chetu pamoja na Hadithi Tukufu, na bora tuanzie nayo kipindi chetu ni salamu ya Kiislamu, basi Assalamu Alaikum Warahmatullahi Wabarakatuh.

Imekuja katika Musnad Ahmad - sehemu iliyobaki ya Musnad ya Al-Mukthirin - Hakika mfilisi katika umma wangu ni yule anayekuja Siku ya Kiyama na funga na swala na zaka, na anakuja hali amemtukana huyu, amemsingizia huyu, na amekula mali ya huyu 

  Ametuhadithia Abdurrahman kutoka Zuhair kutoka Al-Alaa kutoka kwa baba yake kutoka kwa Abu Hurairah kutoka kwa Mtume, swallallahu alayhi wasallam, amesema: "Je, mnajua ni nani mfilisi?" Wakasema: Mfilisi kwetu, ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, ni yule ambaye hana dirham wala bidhaa. Akasema: "Hakika mfilisi katika umma wangu ni yule anayekuja Siku ya Kiyama na funga, swala na zaka, na anakuja hali amemtukana heshima ya huyu, amemsingizia huyu, na amekula mali ya huyu, basi anakaa, na huyu analipwa kutokana na mema yake, na huyu kutokana na mema yake, na yakimalizika mema yake kabla ya kulipa madeni yake ya makosa, huchukuliwa kutoka katika makosa yao na kuwekwa juu yake, kisha anatupwa motoni."

Hakika hadithi hii, kama zilivyo hadithi zingine muhimu, ni lazima ieleweke maana yake na itambulike. Kwa sababu kuna watu ambao ni mafilisi licha ya swala zao, funga zao na zaka zao, kwani huyu alimtukana huyu, akamsingizia huyu, akala mali ya huyu, akamwaga damu ya huyu, na akampiga huyu  

Na ufilisi wake ni kwamba huchukuliwa kutoka kwa mema yake ambayo ni mtaji wake na hupewa huyu na hulipa kwa huyu thamani ya kumsingizia, kumtukana na kumpiga, na baada ya mema yake kwisha kabla ya kulipa madeni yake, huchukuliwa kutoka kwa makosa yao na kuwekwa juu yake kisha anatupwa motoni. 

Na alipowauliza Mtume, rehema na amani zimshukie, masahaba zake, je, mnajua ni nani mfilisi? Maana ya je, mnajua ni kutoka katika kujua na kujua ni elimu ya mambo ya ndani, je, mnajua, yaani mnajua nani hasa mfilisi? Hili linathibitisha kauli ya Sayyidina Ali, Mwenyezi Mungu aukurimishe uso wake: "Utajiri na umaskini ni baada ya kuonyeshwa kwa Mwenyezi Mungu." Walipoulizwa swali hili, walijibu jibu kutokana na uzoefu wao, mfilisi kwetu ni yule ambaye hana dirham wala bidhaa, huyu ndiye mfilisi kwa mtazamo wa masahaba wa Mtume wa Mwenyezi Mungu, basi akasema, rehema na amani zimshukie: Hapana,... AKASEMA: HAKIKA MFILISI KATIKA UMMATI WANGU NI YULE ANAYEKUJA SIKU YA KIYAMA NA FUNGA, SWALA NA ZAKA... 

Na hili linathibitisha kauli ya Sayyidina Umar: Anayetaka afunge na anayetaka aswali lakini ni uadilifu, kwa sababu swala, funga, hijja na zaka hizi ni ibada ambazo mtu anaweza kuzifanya na katika nafsi yake kuna ikhlasi kwa ajili yake, na anaweza kuzifanya kwa unafiki, lakini kitovu cha uzito ni kujidhibiti kwa amri ya Mwenyezi Mungu 

Tunamuomba Mwenyezi Mungu atuthibitishe juu ya haki, na atufanye miongoni mwa waja wake wachaMungu, na atubadilishie maovu yetu kuwa mema, na asituhuzunishe siku ya kuonyeshwa Kwake, Ee Mwenyezi Mungu, Amina 

Wasikilizaji wetu wapendwa, na mpaka tukutane nanyi na hadithi nyingine ya Mtume, tunawaachia amana kwa Mwenyezi Mungu ambaye haipotezi amana zake, na Assalamu Alaikum Warahmatullahi Wabarakatuh 

Nimeiandika kwa ajili ya redio 

Afraa Turab

Pamoja na Hadithi Tukufu - Wanafiki na Matendo Yao Maovu

Pamoja na Hadithi Tukufu

Wanafiki na Matendo Yao Maovu

Tunawasalimu nyote wapenzi mahali popote mlipo, katika kipindi kipya cha programu yenu "Pamoja na Hadithi Tukufu" na tunaanza na salamu bora, Assalamu Alaikum Warahmatullahi Wabarakatuh.

Imepokewa kutoka kwa Buraida Radhi za Allah ziwe juu yake kwamba Mtume ﷺ amesema: “Usimwite mnafiki bwana, kwa sababu ikiwa yeye ni bwana, basi mmemkasirisha Mola wenu Mlezi.” Imepokewa na Abu Daud kwa isnadi sahihi.

Enyi wasikilizaji wapenzi

Hakika maneno bora ni maneno ya Mwenyezi Mungu, na uongofu bora ni uongofu wa Nabii wake Muhammad bin Abdullah, rehma na amani zimshukie, Ama baada ya hayo, 

Hakika hadithi hii tukufu inatuongoza jinsi ya kushughulika na wanafiki tunaowajua, kwani Mtume ﷺ alikuwa ndiye pekee anayewajua wanafiki wote kwa majina yao, lakini tunaweza kuwajua baadhi yao kutokana na sifa zao, kama wale ambao Qur'ani imewaelekeza kuwa wanafanya faradhi kwa uvivu na kwa kulazimishwa, na kama wale wanaowafanyia vitimbi Uislamu na Waislamu, wanahamasisha fitina, wanafanya uharibifu katika ardhi, wanapenda uovu uenee kwa kuualika, kuutetea na kuuchunga, na kama wale wanaosema uongo juu ya Uislamu na Waislamu ... na wengineo walio na sifa za unafiki. 

Kwa hivyo, lazima tutambue kile ambacho sheria imeona ni kizuri na kile ilichoona ni kibaya, ili tumjue mnafiki kutoka kwa mkweli, na tuchukue hatua inayofaa dhidi yake. Hatupaswi kuamini upande wa mtu ambaye anafanya kinyume na sheria na anaonekana kuwa anafanya anachokifanya kwa sababu ya bidii yake kwa Uislamu na Waislamu, na hatupaswi kumfuata au kumunga mkono, au hata chini ya hapo kwa kumuelezea kama bwana, vinginevyo Mwenyezi Mungu atatukasirikia.

Sisi Waislamu lazima tuwe watu wenye bidii zaidi kwa Uislamu na Waislamu, na tusimruhusu mnafiki yeyote kuingilia dini yetu na familia zetu, kwani wao ndio hatari zaidi tunayoweza kukumbana nayo siku hizi kwa sababu ya wingi wao na nyuso zao nyingi. Lazima tukumbuke mizani ya kisheria ya kupima matendo ya anayedai Uislamu, kwani Uislamu kwetu ni kinga dhidi ya watu hawa waovu. 

Tunamuomba Mungu aulinde umma wetu kutokana na wahalifu kama hao, na atuongoze kwenye njia iliyonyooka na mizani sahihi ambayo tunapima tabia za watu nayo, ili tujiepushe na wale ambao hawapendwi na Mungu, Aamin. 

Wapenzi wetu, na hadi tutakapokutana nanyi na hadithi nyingine ya kinabii, tunawaacha katika uangalizi wa Mungu, Assalamu Alaikum Warahmatullahi Wabarakatuh.

Imeandikwa kwa ajili ya redio na: Dkt. Maher Saleh