Pamoja na Hadithi Tukufu
Haya Ni Sehemu ya Imani
Tunawasalimu nyote wapenzi wetu popote mlipo, katika kipindi kipya cha kipindi chenu "Pamoja na Hadithi Tukufu" na tunaanza na salamu bora, Assalamu Alaikum Warahmatullahi Wabarakatuh.
Imekuja katika Sahih Muslim, katika maelezo ya Imam Nawawi "kwa muhtasari" katika "Mlango wa Mambo ya Imani".
Ametuhadithia Abdullah bin Muhammad Al-Jaafi akisema: Ametuhadithia Abu Amir Al-Aqadi akisema: Ametuhadithia Suleiman bin Bilal kutoka kwa Abdullah bin Dinar kutoka kwa Abu Saleh kutoka kwa Abu Hurairah Radhi za Allah ziwe juu yake kutoka kwa Mtume ﷺ akisema: "Imani ina matawi sitini na kitu na haya ni tawi la imani".
Enyi wasikilizaji tukufu:
Hakika imani ina daraja na vyeo, ambavyo watu wengi hawazingatii, hivyo akisali mmoja wao na kufunga anadhani amekamilisha nguzo za Uislamu, na amekuwa karibu sana na imani na kumjua Mwenyezi Mungu, na hii ni kutokana na ujinga ambao umeufunika moyo wa umma huu katika miongo ya udhaifu wa kiakili na kifikhi ulioupata. Pengine hadithi hii ina mambo ambayo kila Muislamu anapaswa kuyafahamu.
Enyi Waislamu:
Hakika haya ambayo yametajwa katika hadithi si chochote ila ni mfano wa maana ya kuwa muumini, ni ishara kuwa imani haisimami katika shahada, sala, funga na zaka pekee, bali inaashiria uhusiano wa Muislamu na Muumba wake, na nafsi yake, na wengine, hivyo Muislamu anakuwa na haya mbele ya Mwenyezi Mungu, na anakuwa na haya mbele ya nafsi yake na mbele ya wengine. Katika hili kuna maonyesho ya maadili ya hali ya juu, hivyo ikiwa tabia ya haya ni sifa inayoambatana na uhusiano wa watu baina yao, vipi kuhusu sifa nyinginezo? Hakika jamii wakati huo itapambwa na maadili haya, na itakuwa jamii inayoongozwa na ukuu, nguvu na imani. Lakini hili litatimia lini ilhali wale wanaopanda mfano wa maadili haya katika umma wamepotea? Hilo litatimia lini ilhali kichwa cha umma huu kimeharibika?!
Ee Mola wetu, tuharakishie khilafa iliyoongoka juu ya manhaji ya Utume ambayo itawaunganisha Waislamu, iondoe kutoka kwao yale waliyo nayo ya balaa, Ee Mola wetu, uangaze ardhi kwa nuru ya uso wako mtukufu. Ee Mola wetu, Amina Amina.
Wapenzi wetu, na mpaka tutakapokutana na hadithi nyingine ya Mtume, tunawaacha katika uangalizi wa Mwenyezi Mungu, Assalamu Alaikum Warahmatullahi Wabarakatuh.
Imeandikwa kwa ajili ya redio na: Abu Maryam