Maadith Sharif
Kuanza kwa Himma Kuzingatia Sharia
Tunawasalimu nyote wapenzi wetu kila mahali, katika kipindi kipya cha programu yenu "Maadith Sharif" na tunaanza na salamu bora, Assalamu Alaikum Warahmatullahi Wabarakatuh.
Imekuja katika Sahih Muslim, katika maelezo ya Imam Nawawi "kwa muhtasari" katika mlango wa kuthibitisha pepo kwa shahidi:
Ametuhadithia Said bin Amru Al-Ash'athi na Suwaid bin Said na tamko ni la Said ametueleza Sufyan kutoka kwa Amru amemsikia Jabir akisema: Alisema mtu: "Mimi niko wapi ewe mjumbe wa Allah ikiwa nitauliwa?" Akasema: "Peponi". Akazitupa tende zilizokuwa mkononi mwake kisha akapigana mpaka akauliwa.
Enyi wasikilizaji wapenzi:
Huyu ni Umair bin Al-Humam, sahaba aliyekulia mikononi mwa Mtume wa Allah صلى الله عليه وسلم, shule ya kwanza katika Uislamu na mwalimu wa kwanza. Yuko katika vita akipigania njia ya Allah, ilimjia akilini kuuliza, "Mimi niko wapi ikiwa nitauliwa na kuwa shahidi?" Naye anajua jibu mapema, na kama kwamba anataka jibu maalum kutoka kwa anaye funuliwa, kutoka kwa Mtume wa Allah صلى الله عليه وسلم, basi akapata jibu, pepo. Akasimama mara moja akazitupa tende chache zilizokuwa mkononi mwake, na akaanza kupigana mpaka akauliwa.
Enyi Waislamu:
Hili ni somo kutoka kwa masomo ya mpenzi wetu na kielelezo chetu Muhammad صلى الله عليه وسلم Mtume wetu mtukufu, kwamba enyi Waislamu anzisheni matendo mara tu mnapopata elimu, inachukua muda gani kula tende? Dakika tatu? Zaidi au chini? Umair aliona muda huu mfupi kuwa mrefu, akajikuta anapigana akiwa anatafuta malipo na anakaribia bila kukimbia mara tu alipojua jibu.
Na sisi pia; Allah سبحانه وتعالى ametuamrisha na ametukataza, basi tuko wapi kutoka kwa maamrisho na makatazo hayo? Ni kiasi gani cha kuzingatia hukumu hizi? Tunaishi katika zama ambazo Waislamu wengi wameacha hukumu za Allah, basi nani atafuata nyayo za Umair radhi za Allah ziwe juu yake? Na afanye kazi na wafanyao kazi ili kuheshimu dini hii, kwa kuanzisha ukhalifa wa Waislamu ambao utawakusanya kwa imamu mpya ambaye atatekeleza sheria ya Mola wao ndani yao.
Ewe Allah tuharakishie kwa ukhalifa ulioongoka juu ya njia ya utume ambao utakusanya waliotawanyika miongoni mwa Waislamu, uondoe kutoka kwao yale waliyo nayo ya balaa, ewe Allah uangaze ardhi kwa nuru ya uso wako mtukufu. Ewe Allah amina amina.
Wapenzi wetu waheshimiwa, na mpaka tutakapokutana nanyi na hadithi nyingine ya Mtume, tunawaacha katika ulinzi wa Allah, na Assalamu Alaikum Warahmatullahi Wabarakatuh.
Imeandikwa kwa ajili ya redio na: Abu Mariam