Pamoja na Hadithi Tukufu - Mlango wa Wamezidi Kupita Kiasi Wameangamia
Pamoja na Hadithi Tukufu - Mlango wa Wamezidi Kupita Kiasi Wameangamia

    Tunawasalimu nyote wapenzi wasikilizaji kila mahali, katika kipindi kipya cha programu yenu "Pamoja na Hadithi Tukufu" na tunaanza na salamu bora, Assalamu Alaikum Warahmatullahi Wabarakatuh.              

0:00 0:00
Speed:
October 06, 2025

Pamoja na Hadithi Tukufu - Mlango wa Wamezidi Kupita Kiasi Wameangamia

Pamoja na Hadithi Tukufu 

Mlango wa Wamezidi Kupita Kiasi Wameangamia

    Tunawasalimu nyote wapenzi wasikilizaji kila mahali, katika kipindi kipya cha programu yenu "Pamoja na Hadithi Tukufu" na tunaanza na salamu bora, Assalamu Alaikum Warahmatullahi Wabarakatuh.              

    Imekuja katika Sahih ya Imam Muslim katika maelezo ya An-Nawawi "kwa muhtasari" katika "Mlango wa Wamezidi Kupita Kiasi Wameangamia"

    Ametuhadithia Abu Bakr bin Abi Shaiba, ametuhadithia Hafs bin Ghiyath na Yahya bin Saeed kutoka kwa Ibn Juraij kutoka kwa Sulaiman bin Atiq kutoka kwa Talq bin Habib kutoka kwa Al-Ahnaf bin Qais kutoka kwa Abdullah, alisema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu - rehema na amani zimshukie - "Wameangamia wazidishaji" alilisema hilo mara tatu.

    Kauli yake rehema na amani zimshukie: (Wameangamia wazidishaji) yaani wenye kupitisha mipaka katika maneno na matendo yao. Na wanachuoni wametaja mifano ya ukali na uzidishaji, ikiwa ni pamoja na mtu kujilazimisha ibada asiyoimudu, na jambo hilo humpelekea kupoteza lililo bora zaidi au humchosha na hukatika. Hiyo ni kama mtu anayejilazimisha kusimama usiku na kurefusha mpaka achoke kwa kukesha, basi macho yake humshinda na kukosa swala ya Fajr kwa jamaa, au kuitekeleza katika wakati wake bora au wa dharura, na miongoni mwa hayo ni kuchukua azma mahali pa ruhusa, kama vile mtu anayeacha ruhusa ya kufuturu katika hali ya safari au ugonjwa, au anaacha kutayamamu na anatumia maji hali yeye yanamdhuru ..... Na miongoni mwa uzidishaji ni wingi wa maswali na matawi, na Salaf wema walikuwa wanachukia maswali kuhusu yale ambayo hayajatokea, kwa hivyo wakiulizwa kuhusu jambo ambalo halijatokea walikuwa wanasema: Liacheni mpaka litokee. 

   Enyi wasikilizaji tukufu:   

    Katika kipindi hiki cha giza tunachoishi ambacho umezidi njama dhidi ya Uislamu na Waislamu, ambacho damu ya Waislamu inatiririka kama mito katika kila sehemu, katika mazingira haya makafiri wahalifu wanawatumia baadhi ya Waislamu haswa wale ambao wamepatwa na mtafaruku wa kiitikadi, iwe amepuuza miongoni mwao au amezidisha katika kuelewa dini. 

    Ama sababu ya mtafaruku huu wa kiitikadi, na upotovu katika uelewa kutoka kwa usahihi, inarejea kwa uvamizi mkubwa wa ustaarabu wa Magharibi ambao umetawala fikra zetu na ladha yetu tawala kamili, umebadilisha dhana zetu kuhusu maisha.

    Pale ustaarabu wa Magharibi ulipoonekana katika nchi za Kiislamu na zikaonekana aina zake za kimji, na maendeleo yake ya kimaada, zilishangaza macho ya wengi. Kwa hivyo wakaanza kuchukua aina hizi za kimji na kuiga ustaarabu wa Magharibi bila ya kubainisha tofauti kati ya ustaarabu wa Magharibi na aina za kimji, na bila ya kutambua kwamba ustaarabu unamaanisha jumla ya dhana kuhusu maisha, na kwamba ni njia maalum ya kuishi. Na kwamba ustaarabu ni aina za kimaada zinazoonekana ambazo zinatumika kama njia na zana katika maisha. Kwa hivyo tuliona fatwa ikiruhusu kuchukua ustaarabu wa Magharibi kikamilifu bila kubagua. Na kinyume chake tuliona mtu amesimama mbele ya ustaarabu huu akiukataa kwa ujumla na kwa undani, akikataa kila kilichozalishwa nao hata kama ni sayansi na maarifa ambayo hayahusiani na dhana kuhusu maisha. Kwa hivyo wakawa wakali wenye maoni haya ukali usiofaa, wakaharimisha kwa ukali wao huu kile ambacho Mwenyezi Mungu amewahalalishia, na wakatoka katika maandiko ya Qur’ani na wakazidisha.

Enyi Waislamu:

     Kwa nini na kwa maslahi ya nani mtafaruku huu wa kiitikadi? Na kwa maslahi ya nani ukali na uzidishaji? 

Hakuna shaka kwamba shambulio dhidi ya dini ni kali, ni vita dhidi ya Uislamu na fikra zake, kwa hivyo pale ambapo Magharibi iliposhindwa kuangamiza Uislamu moja kwa moja, iliamua kuangamiza uelewa sahihi wake kwa wafuasi wake. Mambo yamefika kwa baadhi ya Waislamu kukubali kusimamisha swala ya Ijumaa bila ya khatibu, ambapo walitosheka kusikiliza hotuba kupitia kifaa cha kurekodia. Ni shambulio chafu dhidi ya Uislamu na fikra zake, shambulio ambalo limewasukuma baadhi yao kuharamisha ndoa za karibu kama vile binti wa ami na binti wa shangazi kwa mfano, wakati ambapo ndoa za karibu zinaruhusiwa. Ni dini gani hii wanayoitaka kwa Waislamu? Ni dini ya ustaarabu wa Magharibi ambao haachi kutafuta njia ya kuuangamiza. Lakini tunachukua hadithi ya Mtume – rehema na amani zimshukie - "Wameangamia wazidishaji" kwa matumaini, kwa hivyo hatima ya hawa wazidishaji ni kuangamia, na hilo litakuwa pale mambo yatakapowekwa katika nafasi yake sahihi, pale itakaposimama Khilafa ya kweli nayo inakaribia kusimama kwa idhini ya Mwenyezi Mungu. Hapo ndipo hukumu sahihi zitawekwa katika utekelezaji na zitakataliwa hukumu za uzidishaji.

   Ewe Mwenyezi Mungu, tuharakishie kwa Khilafa itakayounganisha Waislamu waliotawanyika, uwaondolee yale waliyonayo ya balaa, Ewe Mwenyezi Mungu, iangaze ardhi kwa nuru ya uso wako mtukufu. Ewe Mwenyezi Mungu, Amina Amina.

   Wasikilizaji wetu wapenzi, na mpaka tutakapokutana na hadithi nyingine ya Mtume, tunawaacha katika hifadhi ya Mwenyezi Mungu, Assalamu Alaikum Warahmatullahi Wabarakatuh.

Imeandikwa kwa ajili ya Radio na: Abu Mariam

More from Sheria

Pamoja na Hadithi Tukufu - Je, mnajua ni nani mfilisi?

Pamoja na Hadithi Tukufu

Je, mnajua ni nani mfilisi?

Karibuni wasikilizaji wetu wapendwa, wasikilizaji wa redio ya Ofisi ya Habari Kuu ya Hizb ut-Tahrir. Tunakutana nanyi tena na kipindi chetu pamoja na Hadithi Tukufu, na bora tuanzie nayo kipindi chetu ni salamu ya Kiislamu, basi Assalamu Alaikum Warahmatullahi Wabarakatuh.

Imekuja katika Musnad Ahmad - sehemu iliyobaki ya Musnad ya Al-Mukthirin - Hakika mfilisi katika umma wangu ni yule anayekuja Siku ya Kiyama na funga na swala na zaka, na anakuja hali amemtukana huyu, amemsingizia huyu, na amekula mali ya huyu 

  Ametuhadithia Abdurrahman kutoka Zuhair kutoka Al-Alaa kutoka kwa baba yake kutoka kwa Abu Hurairah kutoka kwa Mtume, swallallahu alayhi wasallam, amesema: "Je, mnajua ni nani mfilisi?" Wakasema: Mfilisi kwetu, ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, ni yule ambaye hana dirham wala bidhaa. Akasema: "Hakika mfilisi katika umma wangu ni yule anayekuja Siku ya Kiyama na funga, swala na zaka, na anakuja hali amemtukana heshima ya huyu, amemsingizia huyu, na amekula mali ya huyu, basi anakaa, na huyu analipwa kutokana na mema yake, na huyu kutokana na mema yake, na yakimalizika mema yake kabla ya kulipa madeni yake ya makosa, huchukuliwa kutoka katika makosa yao na kuwekwa juu yake, kisha anatupwa motoni."

Hakika hadithi hii, kama zilivyo hadithi zingine muhimu, ni lazima ieleweke maana yake na itambulike. Kwa sababu kuna watu ambao ni mafilisi licha ya swala zao, funga zao na zaka zao, kwani huyu alimtukana huyu, akamsingizia huyu, akala mali ya huyu, akamwaga damu ya huyu, na akampiga huyu  

Na ufilisi wake ni kwamba huchukuliwa kutoka kwa mema yake ambayo ni mtaji wake na hupewa huyu na hulipa kwa huyu thamani ya kumsingizia, kumtukana na kumpiga, na baada ya mema yake kwisha kabla ya kulipa madeni yake, huchukuliwa kutoka kwa makosa yao na kuwekwa juu yake kisha anatupwa motoni. 

Na alipowauliza Mtume, rehema na amani zimshukie, masahaba zake, je, mnajua ni nani mfilisi? Maana ya je, mnajua ni kutoka katika kujua na kujua ni elimu ya mambo ya ndani, je, mnajua, yaani mnajua nani hasa mfilisi? Hili linathibitisha kauli ya Sayyidina Ali, Mwenyezi Mungu aukurimishe uso wake: "Utajiri na umaskini ni baada ya kuonyeshwa kwa Mwenyezi Mungu." Walipoulizwa swali hili, walijibu jibu kutokana na uzoefu wao, mfilisi kwetu ni yule ambaye hana dirham wala bidhaa, huyu ndiye mfilisi kwa mtazamo wa masahaba wa Mtume wa Mwenyezi Mungu, basi akasema, rehema na amani zimshukie: Hapana,... AKASEMA: HAKIKA MFILISI KATIKA UMMATI WANGU NI YULE ANAYEKUJA SIKU YA KIYAMA NA FUNGA, SWALA NA ZAKA... 

Na hili linathibitisha kauli ya Sayyidina Umar: Anayetaka afunge na anayetaka aswali lakini ni uadilifu, kwa sababu swala, funga, hijja na zaka hizi ni ibada ambazo mtu anaweza kuzifanya na katika nafsi yake kuna ikhlasi kwa ajili yake, na anaweza kuzifanya kwa unafiki, lakini kitovu cha uzito ni kujidhibiti kwa amri ya Mwenyezi Mungu 

Tunamuomba Mwenyezi Mungu atuthibitishe juu ya haki, na atufanye miongoni mwa waja wake wachaMungu, na atubadilishie maovu yetu kuwa mema, na asituhuzunishe siku ya kuonyeshwa Kwake, Ee Mwenyezi Mungu, Amina 

Wasikilizaji wetu wapendwa, na mpaka tukutane nanyi na hadithi nyingine ya Mtume, tunawaachia amana kwa Mwenyezi Mungu ambaye haipotezi amana zake, na Assalamu Alaikum Warahmatullahi Wabarakatuh 

Nimeiandika kwa ajili ya redio 

Afraa Turab

Pamoja na Hadithi Tukufu - Wanafiki na Matendo Yao Maovu

Pamoja na Hadithi Tukufu

Wanafiki na Matendo Yao Maovu

Tunawasalimu nyote wapenzi mahali popote mlipo, katika kipindi kipya cha programu yenu "Pamoja na Hadithi Tukufu" na tunaanza na salamu bora, Assalamu Alaikum Warahmatullahi Wabarakatuh.

Imepokewa kutoka kwa Buraida Radhi za Allah ziwe juu yake kwamba Mtume ﷺ amesema: “Usimwite mnafiki bwana, kwa sababu ikiwa yeye ni bwana, basi mmemkasirisha Mola wenu Mlezi.” Imepokewa na Abu Daud kwa isnadi sahihi.

Enyi wasikilizaji wapenzi

Hakika maneno bora ni maneno ya Mwenyezi Mungu, na uongofu bora ni uongofu wa Nabii wake Muhammad bin Abdullah, rehma na amani zimshukie, Ama baada ya hayo, 

Hakika hadithi hii tukufu inatuongoza jinsi ya kushughulika na wanafiki tunaowajua, kwani Mtume ﷺ alikuwa ndiye pekee anayewajua wanafiki wote kwa majina yao, lakini tunaweza kuwajua baadhi yao kutokana na sifa zao, kama wale ambao Qur'ani imewaelekeza kuwa wanafanya faradhi kwa uvivu na kwa kulazimishwa, na kama wale wanaowafanyia vitimbi Uislamu na Waislamu, wanahamasisha fitina, wanafanya uharibifu katika ardhi, wanapenda uovu uenee kwa kuualika, kuutetea na kuuchunga, na kama wale wanaosema uongo juu ya Uislamu na Waislamu ... na wengineo walio na sifa za unafiki. 

Kwa hivyo, lazima tutambue kile ambacho sheria imeona ni kizuri na kile ilichoona ni kibaya, ili tumjue mnafiki kutoka kwa mkweli, na tuchukue hatua inayofaa dhidi yake. Hatupaswi kuamini upande wa mtu ambaye anafanya kinyume na sheria na anaonekana kuwa anafanya anachokifanya kwa sababu ya bidii yake kwa Uislamu na Waislamu, na hatupaswi kumfuata au kumunga mkono, au hata chini ya hapo kwa kumuelezea kama bwana, vinginevyo Mwenyezi Mungu atatukasirikia.

Sisi Waislamu lazima tuwe watu wenye bidii zaidi kwa Uislamu na Waislamu, na tusimruhusu mnafiki yeyote kuingilia dini yetu na familia zetu, kwani wao ndio hatari zaidi tunayoweza kukumbana nayo siku hizi kwa sababu ya wingi wao na nyuso zao nyingi. Lazima tukumbuke mizani ya kisheria ya kupima matendo ya anayedai Uislamu, kwani Uislamu kwetu ni kinga dhidi ya watu hawa waovu. 

Tunamuomba Mungu aulinde umma wetu kutokana na wahalifu kama hao, na atuongoze kwenye njia iliyonyooka na mizani sahihi ambayo tunapima tabia za watu nayo, ili tujiepushe na wale ambao hawapendwi na Mungu, Aamin. 

Wapenzi wetu, na hadi tutakapokutana nanyi na hadithi nyingine ya kinabii, tunawaacha katika uangalizi wa Mungu, Assalamu Alaikum Warahmatullahi Wabarakatuh.

Imeandikwa kwa ajili ya redio na: Dkt. Maher Saleh