Pamoja na Hadithi Tukufu
Kuanza Salama ni Mlango Miongoni mwa Milango ya Kheri
Tunawasalimu nyote wapenzi popote mlipo, katika kipindi kipya cha programu yenu "Pamoja na Hadithi Tukufu" na tunaanza na salamu bora, Assalamu Alaikum Warahmatullahi Wabarakatuh.
Kutoka kwa Abu Hurairah Radhi za Allah ziwe juu yake, alisema: Mtume wa Allah ﷺ alisema: «Mwendesha chombo amsalimie anayetembea, na anayetembea amsalimie anayeketi, na wachache wamsalimie wengi». Imesimuliwa na Bukhari namba 2160.
Enyi wasikilizaji wazuri:
Alisema Al-Hafidh katika Al-Fath: Hakika wanachuoni wamezungumza kuhusu hekima katika yale ambayo Allah Mtukufu amewaamrisha kuanza na salamu, na baadhi yao walisema: Mdogoz amsalimie mkubwa kwa ajili ya haki ya mkubwa; kwa sababu ameamrishwa kumheshimu na kumnyenyekea, na wachache wamsalimie wengi kwa ajili ya haki ya wengi; kwa sababu haki yao ni kubwa zaidi na kwa fadhila ya jamaa, na mwendesha chombo amsalimie anayetembea ili asijivune kwa kupanda kwake na arejee kwenye unyenyekevu, na kadhalika...
Enyi Waislamu:
Tunaendelea na maelezo ya haki ya jamaa juu ya watu binafsi kupitia mtazamo uliotajwa katika hadithi, au ikiwa mnataka kusema haki ya chama juu ya watu wa umma, ikiwa salamu ya wachache kwa wengi ni wajibu; basi yale yaliyo juu ya salamu ni ya lazima zaidi, basi anayesikia juu ya jamaa inayolingania kwa Allah na kubeba fiqhi, fikra na elimu anapaswa kuharakisha na kuwapa salamu kwanza, na kuuliza kuhusu da'awa yao, fiqhi na fikra zao pili, na aendelee kufanya kazi nao ikiwa yale wanayolingania yanaafikiana na neno la Allah na Mtume wake, basi huu ni mlango miongoni mwa milango ya kheri kubwa inayoanza na salamu.
Ewe Mola, tuharakishie ukhalifa ulioongoka juu ya manhaji ya utume ambao unakusanya utengano wa Waislamu, uwaondolee yale waliyomo ya balaa, Ewe Mola, uangaze ardhi kwa nuru ya uso wako Mtukufu. Ewe Mola, Amina Amina.
Wapenzi wetu waheshimiwa, na mpaka tutakapokutana nanyi na hadithi nyingine ya kinabii, tunawaacha katika hifadhi ya Allah, na Assalamu Alaikum Warahmatullahi Wabarakatuh.
Imeandikwa kwa ajili ya redio: Abu Maryam